Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 30, 2012

TANZANIA YA TANGAZA VITA NA KITUO CHA MAREKANI CHA CNN...!

 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Tanzania Assah Mwambene 

Serikali ya Tanzania imekitaka kituo cha televisheni cha Kimataifa cha CNN kusahihisha taarifa potofu ilizotoa kuhusu mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa upo kwenye ufukwe wa Pwani ya Tanzania jambo ambalo Serikali imesema siyo sahihi.

Akiongea na waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene amesema Serikali ya Tanzania imesikitishwa sana na taarifa hiyo na kuitaka CNN kuisahihisha mara moja.

“Tumesikitishwa sana na taarifa hiyo na tunashangaa kuona chombo kikubwa kama CNN wanaweza kutoa taarifa za uongo kwa kiasi hicho” amesema Bw. Mwambene.

Amesema ukweli ni kwamba unapozungumia eneo la Tanzania kilometa za mraba 947,300 (947,300 sq km) ikiwa ni pamoja na nusu ya eneo la ziwa kaskazini mwa mpaka wa Tanzania na Msumbiji na kwamba mpaka upo katikati ya ziwa kama ilivyo kwa mpaka wa Malawi na Msumbiji.

Kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 24 Novemba, 2012, CNN International yenye makao yake Makuu nchini Marekani imekuwa ikiendesha kipindi kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi na kuonyesha kwamba mpaka uko pembezoni mwa ufukwe wa Tanzania.

Bw. Mwambene amesema kuwa suala hilo hivi sasa linatarajiwa kupelekwa katika Baraza la Marais wastaafu wa Nchi za Umoja wa SADC kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9 mwaka huu.

Kauli mbiu za sherehe za uhuru mwaka huu ni uwajibikaji , uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo ya Taifa letu.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI

HIVI NDIO VIFAA VYA MAREHEMU SHAROMILIONARE VILIVYOPATIKANA...!

JESHI la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kukamata baadhi ya vitu vilivyoporwa kufuatia ajali iliyosababisha kifo cha msanii wa maigizo na muziki wa kizazi kipya nchini hapa, Hussein Ramadhani Mkiety maarufu kama Sharo Milionea ambaye alikufa baada ya gari aliyokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe amesema kuwa vifaa hivyo vimepatikana kumetokana na jeshi la Polisi kufanya msako mkali kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Songa Maguzoni.
Kamanda Massawe amesema msakohu umefanikiwa kukamatwa kwa vitu hivyo mbalimbali, zikiwemo nguo alizokuwa amevaa marehemu Sharomilionea.
Massawe alivitaja miongoni mwa vitu vilivyokamatwa ni Betri ya gari na Redio ya gari vilikuwa katika gari la marehemuj pamoja na tyrebegi lililokuwa na nguo alizovuliwa marehemu siku ya ajali ambazo inadhaniwa kuwa ndizo alizokuwa amezivaa, ikiwemo sambamba na mkanda,suruali na saa ya mkononi.
Aidha alisema kwamba watuhumiwa walioiba vifaa hivyo walimtumia mtu mmoja ambaye alikwenda kuvisalimisha kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho cha songe, Abdi Zawadi ambapo wengine wanaotuhumiwa kuhusika na wizi huo wakihama kaya zao wamekimbia.
Alisema kuwa Polisi walifanikiwa kuikamata simu hiyo ya mkononi ya marehemu aina ya Blackberry ambayo tayari ilikuwa katika mikono ya mnunuzi na ilishaondolewa chipu kwa lengo la kuuzwa.
“Baada ya kuweka mtego wa kuinunua tumeikuta tayari imeshaondolewa chipu sasa sijui ilikuwa na hela lakini vitu vingine vimesalimishwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji “,alisema Kamanda huyo.
Hata hivyo alisema kuwa licha ya watuhumiwa wa wizi huo kufahamika lakini wamekimbia makazi yao tangu kuanza kwa msako huo na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta.
Marehemu Sharo Milionea aliiaga dunia usiku wa kuamkia Novemba 27 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku eneo la Songa-Maguzoni wilayani Muheza mkoani Tanga katika barabara Kuu ya Segera kwenda Tanga baaada ya gari alilokuwa akiendesha kuacha njia na kupinduka.
Sharo Milionea alizikwa Novemba 28 mwaka huu huko Kijijini kwao Lusanga wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Credit kwa rockersports

Thursday, November 29, 2012

PICHA ZA DIAMOND AKIWA KATIKA KIPINDI CHA THE MBONI SHOW KILICHORUSHWA NA CHANEL YA EATV LEO SAA TATU YA USIKU...!


Hapa Diamond akiwa amefika eneo la tukio....akiwa na Mose Iyobo pamoja na Romy J
kwaajili ya kurecord kipindi cha The Mboni Show




Diamond akisalimiana na George Tyson Director wa Kipindi cha The Mboni Show


Kila wakati Diamond huanza na kumuomba Mungu kabla hajafanya jambo lolote kwa kua huwa anaamini pasipo kumuomba Mwenyzi Mungu kabla hawezi kufanya vizuri wala kutimiza malengo yake.


Hapa Mboni Masimba akipitia baadhi ya mambo kabla ya kuanza kipindi...


Diamond na Mboni wakiwa kwenye kipindi...




Mboni akilainisha koo kidogo

Diamond naye akipata kinywaji ili kulipooza koo..



Picha ya Pamoja Diamond, Mboni na Rj


Baada ya show kumalizika hali ilikuwa hivi....















Wednesday, November 28, 2012

Angalia PICHA ....MAZIKO YA SHARO MILIONEA,MAJUTO AKOSA NGUVU KWA MAJONZI,MAMIA WAFURIKA KUMUAGA..!




 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.

Tuesday, November 27, 2012

HAWA NDIO MABILIONEA WATANO TANZANIA...!

WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.

Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).

Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali. Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.

Soma zaidi...http://www.mwananchi.co.tz/habari

HIVI NDIVYO JINSI YA KUVUNGA TAI....!

Watu walio wengi hasa mijini hupenda sana kuvaa tai na kuonekana Nadhifu. Ofisi kaka Mabenki, Idara ya Kodi ndio wanaongoza hivi sasa kwa uvaaji wa tai na viongozi mbalimbali wa Serikali. Lakini ni Ukweli usio fichika kuwa katika kila kundi la watu 10 unaopishana nao wamevaa tai basi huenda ni wawili au mmoja ndie anajua kufunga tai kisasa na kitaalam. Nasema hivi kutokana na vile ilivyo kuwa wengi hufungiwa tai hizo na pindi ikifungwa haifunguliwi hadi ichakae.

Kawaida Tai ikifungwa na ukavuta ulimi mdogo haipaswi kuweka fundo, na pindi ikiweka fundo basi ujue hujafunga vyema. Leo Hii Father Kidevu Blog imeona bora itoe somo hilo la ufungaji tai, ili wewe msomaji uweze kujifungua mwenyewe tai yako na si kwa domu au mtaalam mmoja wa hapo ofisini kwenu, naka siku hayupo basi huwi smat.

Chanzo: mroki

Monday, November 26, 2012

"BREAKING NEWZ" SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI HUKO MUHEZA TANGA...!

Msanii aliyekua anakuja juu kwa kasi katika muziki, ucheshi na pia matangazo ya biashara likiwemo la Airtel Money la kampuni ya simu ya Airtel aliyejulikana kwa jina la Hussein Ramadhani Mtioeti (27) maarufu kama SHARO MILIONEA amefariki dunia katika ajali ya gari jijini Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe, amethibitisha kutokea kwa ajali na kusema kuwa marehemu amefikwa na umauti baada ya gari lake aina ya Toyota Haria lenye namba za usajili T478DVR kuacha njia na kupinduka.

Hili ni pigo jingine kwa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania, hasa ukizingatia kuwa juma lililopita alifariki msanii Mlopelo na wakati Sharo Milionea anafariki tayari tasnia hiyo ya bongo Move ipo katika Msiba mwingine mzito wa Mcheza Filamu John Steven anaetarajiwa kuzikwa kesho.

Kamanda Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku wa Novemba 26, 2012 katika kijiji cha Maguzoni Soga Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.

Akisimulia zaidi RPC Massawe anasema kuwa marehemu alikuwa akiendesha gari hilo na alikuwa peke yake bila abiria mwingine na ajali kumfika akiwa katika kijiji hicho kilichopo kati ya segera na Muheza.

“Marehemu ndie alikuwa akiendesha gari lile, na lililopopinduika yeye alirushwa nje lkupitia kiooo cha mbele na umauti kumfika hapo hapo” alisema Kamanda Massawe.

Aidha Kamanda Massawe amesema msanii huyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam na alikuwa akienda nyumbani kwao Muheza.

Inakumbukwa kuwa Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa staili yake ya utembeaji na uongeaji alipata al;inusurika katika ajali nyinge mapema mwaka huu baada ya basi alilokuwa akisafiria la Taqwa kutoka nchi jirani ya Burundi kupata ajali Mikese mjini Morogoro Januari 5 mwaka huu akirejea Dar es Salaam.

Habari zaidi zitakuja kadri zitavyotufikia.
Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - Amina




Thursday, November 22, 2012

UKISHAMPENDA, MUOE UMMILIKI LA SIVYO KAA TAYARI KUSALITIWA ...!

WIKI iliyopita utakumbuka nilianza kuzungumzia mbinu sahihi ya kukabiliana na tabia iliyoshimiri huko mtaani ya wapenzi kusalitiana.
Nikasema kama unatokea kumpenda mtu, kisha ukajiridhisha mtu huyo ni chaguo sahihi la moyo wako, unatakiwa kufanya jitihada za haraka kumuoa na kumuweka ndani.
Nilisema hivyo nikimaanisha kwamba, ukishamuoa unampunguzia yeye vishawishi mbalimbali vya wanaume.
Pia kwa kufanya hivyo utakuwa unajipa imani ya kwamba, wanaume wakware hawawezi kukutibulia licha ya kwamba wakiamua pia wanaweza kama huyo uliyemuoa atakuwa hajatulia.
Katika kuliweka sawa hilo, nikamtolea mfano kijana mmoja aliyebahatika kumpata msichana ambaye alimpenda sana lakini katika chelewachelwa ya kumuoa, akashindwa kumzuia na vishawishi na matokeo yake akajikuta anashea penzi na wanaume wengine.
Hebu msikilize huyu kijana kisha tuendelea, anasema: “Nilipobahatika kupata kazi nzuri niliapia kuoa mke mzuri. Katika pitapita yangu nikakutana na binti mmoja mzuri sana ambaye tulianzisha uhusiano.
“Binti huyo alionesha kunipenda sana, majina ya baby, sweetie, honey ndiyo aliyokuwa akiyatumia kuniita, hata siku moja hakuwahi kuniita jina langu.
“Kilichokuwa kinaniumiza kichwa ni kwamba, alikuwa na simu tatu na kila simu ilikuwa na line mbili. Sikujua ni za nini namba zote hizo na zaidi ya yote, alikuwa hapendi niguse simu zake.
“Siku moja tukiwa chumbani, alibanwa na kifua. Akazidiwa na kuwa na hali mbaya iliyonilazimu nimkimbize hospitalini. Siku hiyo ndiyo nilijua uozo wake wote.
“Yaani kila simu alikuwa akiwasiliana na wanaume wingine.”
Ushuhuda huu unatupa fundisho kubwa sana. Wasichana wengi wa mjini ni wazuri na wanayajua mapenzi kweli lakini wengi wao wametawaliwa na utapeli.
Unaweza kutokea kumpenda sana lakini kumbe yeye ana lake jambo, anakuchukulia kama wa kukuchuna tu na nyuma yako unachangia penzi na wenzako kibao.
Kikubwa ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na msichana yeyote na ukaona anafaa kuwa mkeo hata kama utabaini kuwa ni mapepe, fanya haraka umuoe.
Ukishamuoa angalau unaweza kuwa na imani kwamba hawezi kutoa ‘sukari’ yako kwa mtu mwingine licha ya kwamba, hata ukimuoa akiamua kukusaliti anaweza.
Kinachosaidia ukishamuoa ni kwamba, atatakiwa kufanya kazi ya ziada sana kukusaliti bila ya wewe kujua na hata akikusaliti haitakuwa kwa kiwango kikubwa kama akiwa mbali na wewe.
Tukae tukijua kwamba ulimwengu umeoza, kuna wanaume wapo tu na siku zote mitego yao ni kwa wake na wapenzi wa watu.
Lakini pia kuna wasichana ambao wana pepo wa ngono kiasi kwamba, mwanaume yeyote atakayemtokee ni saizi yake. Hali hii inamfanya kila aliye kwenye ulingo wa mapenzi kuwa makini ni mtu wake.
Chanzo:GPL

Wednesday, November 21, 2012

HIVI ndivyo DI MATTEO ALIVYO FUKUZWA CHELSEA.na UWEZEKANO wa BENITEZ KUJA CHELSEA ...!

Di Matteo aliiwezesha Chelsea kuwa mshindi wa klabu bingwa barani Ulaya, na vile vile kupata Kombe la FA msimu uliopita, na mwezi Juni, alitia saini mkataba wa miaka miwli.
Lakini kufuatia Chelsea kuzabwa magoli 3-0 na Juventus usiku wa Jumanne, inaelekea timu hiyo itakuwa na kibarua kigumu sana cha kufanikiwa kuendelea katika michuano ya klabu bingwa, na kwa hiyo wasimamizi wa klabu wameonelea ni vyema kumtimua kutoka Stamford Bridge.

Kulingana na taarifa katika mtandao wa Chelsea, "klabu kitatoa taarifa kamili hivi karibuni kuhusiana na meneja wa timu".
Roman Abramovich, tajiri anayemiliki klabu ya Chelsea, sasa atakuwa anamtafuta meneja wa tisa, tangu kumiliki klabu mwaka 2003, na kwa muda mrefu, inaaminika amekuwa akizitamani sana huduma za aliyekuwa meneja wa Barcelona ya Uhispania, Pep Guardiola.
Lakini vile vile amewasiliana na aliyekuwa kocha wa Liverpool ya Uingereza, Rafael Benitez, na kuna uwezekano huenda akashikilia hatamu kwa muda mfupi.
Abramovich, raia wa Urusi, tayari alikuwa amewasiliana na Benitez hata kabla ya Chelsea kushindwa nchini Italia.

WATEJA 42 WA TIGO LEO KUIBUKA WASHINDI KATIKA DROO YA PILI YA SMARTCARD...!


Meneja Intaneti wa Tigo Titus Kafuma (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tigo kuchagua washindi wengine 42 leo mbele ya Revenue Assurance na Bodi ya Usimamizi wa Michezo ya Bahati Nasibu katika droo ya pili ya mwezi ya Jumuiya ya Tigo SmartCard itakayofanya washindi waliochaguliwa mpaka sasa kufikia 84.

MFUNGWA KUKUTWA URAIANI NA SMG: Polisi, Magereza wakinzana kwa kauli ...!

 
Sakata la mfungwa aliyekutwa uraiani akiwa na bunduki na risasi, limeingia katika hatua mpya baada ya Jeshi la Polisi na Magereza kutoa kauli zinazokinzana.Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limeendelea kuthibitisha kuwa mtuhumiwa aliyekamatwa nyumbani kwake Novemba 16, mwaka huu akiwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), risasi 31 na magazini tatu, Masanja Maguzu (42), ni mfungwa ambaye hajamaliza kutumikia kifungo cha miaka 15 jela na kuwa alitoka gerezani katika mazingira ya kutatanisha.

Wakati Jeshi la polisi likisisitiza hivyo, Jeshi la Magereza limetoa taarifa inayoeleza kuwa mtu huyo alishamaliza kifungo.

Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi, amekanusha madai ya Jeshi la Magereza kwamba mfungwa huyo alishamaliza kutumikia adhabu yake ya kifungo cha miaka mitano jela na kwamba hata kama alikuwa akitumikia adhabu ya miaka mitano muda huo bado haujatimia.

Kamanda huyo alifafanua jana kuwa hata kama kuna tetesi za mfungwa huyo kuachiwa kwa msamaha wa Rais, makosa yaliyompeleka gerezani kwa mujibu wa Sheria ya Msamaha hayana msamaha.

Alisema mfungwa huyo alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela mwaka 2010 baada ya yeye na mwenzake, Japhet Sylivester, kupatikana na hatia ya kukamatwa na SMG, risasi 622 na nyara za serikali (nyama ya nyati) akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa).

Kamanda Msangi aliiambia NIPASHE kwa njia ya simu kuwa leo atatoa taarifa kamili ya jinsi mfungwa huyo alivyotoka gerezani baada ya Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina na kubaini ukweli wa mazingira yaliyosababisha kuwa uraiani.

Alifafanua kuwa wafungwa hao walikuwa wakiitumia bunduki hiyo kufanyia vitendo vya uhalifu ukiwamo ujambazi na ujangili na siku hiyo walikamatwa nayo ndani ya hifadhi hiyo na risasi 74 na baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi na wa wanyamapori aliwapeleka nyumbani kwake kuwaonyesha alipokuwa ameficha nyingine 548.

Alidai kuwa wafungwa hao walikamatwa katika msako wa pamoja wa kukabiliana na vitendo vya uhalifu na kukabiliana na ujangili uliokuwa ukiendeshwa kwa pamoja kati ya askari wa Jeshi la Polisi na Wanyamapori mkoani Shinyanga kwa wakati huo.

Alisema baada ya kufunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Shinyanga, watuhumiwa hao walipatikana na hatia na hivyo kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 15 jela kila mmoja.

“Kesho (leo), nitatoa picha kamili ya jinsi mfungwa huyo alivyotoroka gerezani na kumuacha mwenzake waliyehukumiwa naye kifungo, hii ni baada ya kufanya uchunguzi wetu wa kina na kumhoji mfungwa mwenyewe na kubaini mambo kadha wa kadha yaliyosababisha yeye kuwa uraiani na kuendelea kufanya vitendo vya uhalifu na ujangili kwa kutumia silaha za kivita,” alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi, wafungwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi ambayo ni kupatikana na bunduki, risasi, nyara za serikali na kuingia na kuwinda ndani ya hifadhi bila kibali na baada ya kupatikana na hatia na kuhukumiwa kwenda gerezani, hayawezi kutolewa msamaha.

“Watuhumiwa hawa walipatikana na makosa ya kupatikana na bunduki ya kivita, kupatikana na risasi, kupatikana na nyara za serikali na kuingia kuwinda ndani ya hifadhi na kuwinda bila kibali nyume cha sheria makosa yote haya yanaangukia kwenye makosa ya uhujumu uchumi ambayo hayana msamaha kisheria,” aliongeza.

Alisema siku 10 kabla ya kumkamata mfungwa huyo akiwa uraiani na SMG hiyo, risasi 31 na magazini tatu, moja hutumika katika bunduki aina ya Uzi gun ya Kiisraeli, jeshi hilo lilikuwa limemkamata mke wake, Holo Mabuga (30), akiwa na bunduki ya kivita aina ya G3, risasi zake 36 pamoja na risasi nyingine zinazotumika kwenye bunduki aina ya SMG inayodaiwa pia kutumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu na ujangili katika Senapa na Pori la Akiba la Maswa.

TAARIFA YA MAGEREZA
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Kamishna wa Magereza, Deonice Chamulesile, ilisema Maguzu alikuwa anatumikia kifungo cha miaka mitano, lakini Aprili 26, mwaka huu alikuwa ameachiliwa.

“Mfungwa aliyekuwa na Namba 250/2010, Masanja Maguzu, alipokelewa Gereza la Wilaya ya Shinyanga tarehe 3 Novemba, 2010 baada ya kuhukumiwa na Mahakama ya wilaya hiyo kwa makosa mbalimbali ya uhujumu uchumi,” alisema.

Aliongeza: “Alianza kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani kuanzia Novemba 3, 2010 na kufikia Aprili 26, 2012 aliachiliwa baada ya kutimiza masharti ya kifungo na kutoka gerezani kwa mujibu wa sheria, hivyo ifahamike kwamba hakutoka katika mazingira ya utata kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari.”

Taarifa hiyo iliyataja makosa aliyohukumiwa kuwa ni kuingia kinyume cha sheria katika hifadhi, kuwinda kunyume cha sheria na kumiliki kinyume cha sheria nyara za serikali.

Taarifa hiyo ya Chamulesile ilieleza kuwa katika kosa la kwanza, Maguzu alihukumiwa miaka miwili jela, kosa la pili miaka mitano jela na la tatu miaka mitano jela.

Alisema hukumu iliyotolewa iliamuru adhabu hizo zitumikiwe kwa pamoja kwa kufungwa miaka mitano jela.
 
Chanzo: Nipashe


HOW TO KEEP YOURSELF & YOUR BABY HEALTHY...!

Well, as you suspected, your pregnancy test is positive. Congratulations! Pregnancy can be an exciting time, and a really wonderful experience.
Of course, now that you’re expecting, you probably have lots of questions, some of which relate to how your HIV-positive status will impact your pregnancy and your baby.
The goal in every pregnancy is to keep both mom and baby healthy, and I’m happy to say that this is a goal that’s well within your reach. Just because you have HIV does not mean you can’t have a happy, healthy pregnancy, and a happy, healthy baby. Basically, the same things that keep you healthy will keep your baby healthy. Risks of transmitting the virus to your baby decrease as your own viral load decreases.
So let’s talk about what you need to do to keep both you and your little one healthy. Many women wonder how HIV can be transmitted to the baby. HIV can be transmitted during pregnancy, during labor and delivery, or by breastfeeding. We’ll talk about what you can do during pregnancy, during labor, and after your baby is born to decrease the chances of transmitting the virus.
THE RIGHT DOCTOR AND THE RIGHT TESTS
It can be very helpful to have an obstetrician with experience treating HIV-positive women, in part because the decisions regarding whether to use certain “invasive” genetic tests can be difficult. Many pregnant women undergo a variety of screening tests
Because these tests are invasive, they involve at least a theoretical increased risk of transmitting the virus to the baby. To date, there have been 159 reported invasive procedures on HIV-positive moms with no transmission of HIV to the baby. In all cases, women were on HAART (highly active antiretroviral therapy) with undetectable viral loads and though no transmissions of HIV have occurred, a small increase in risk can’t be ruled out. Therefore, any HIV-positive woman undergoing any invasive procedure should be on HAART and have an undetectable viral load at the time of the procedure.
Some experts consider CVS too risky to offer to their HIV-positive patients and recommend limiting invasive procedures to amniocentesis only, but existing data on transmission risk associated with these procedures are limited. Invasive testing procedures should be discussed thoroughly with your OB and between you and your partner. Your OB (or genetic counselor) will discuss the pros and cons of invasive testing with you. But ultimately, whether to test (or not to test) is a personal decision.
HOW TO REDUCE THE RISK OF TRANSMITTING HIV TO YOUR BABY DURING PREGNANCY
Keeping your viral load low is important during pregnancy to reduce the risk of transmission. Regardless of what is recommended based solely on your CD4+ and VL levels, you may want to start taking HIV meds as soon as you learn you are pregnant. Yes, there are guidelines from the Department of Health and Human Services (DHHS) that recommend when to start treatment based on CD4+ and VL, but there are groups of people for which treatment is recommended no matter what. Pregnant women are one of those groups. We are trying to prevent your baby from becoming infected.
Earlier and sustained control of HIV viral replication is associated with decreased residual risk of transmission and favors initiating HAART drugs as early in pregnancy as possible for all women.” In other words, starting HAART (highly active antiretroviral therapy) drugs early to control the viral load as much as possible decreased the chances that the virus would be transmitted to the baby. In fact, we know that having an undetectable viral load substantially lowers the risk of transmission of HIV to the fetus and lessens the need for consideration of cesarean delivery (C-section). That’s why it is always suggested that my patients start HAART immediately after learning about their pregnancy.
So, if you are not currently taking HIV medications (whether you are treatment-naive or have taken them in the past), tell your HIV specialist about what medications you’ve taken in the past and provide all laboratory tests (genotypes, phenotypes, HLA B*5701) and be honest about any adherence issues that you’ve had in the past. Also talk about any tolerability issues and drug allergies you have had with any old regimen(s).
As soon as you learn that you’re pregnant, you should contact your HIV specialist to discuss your options for medication and to review what you’re currently taking to make sure your medications are safe for the baby. If you are taking HIV medication, like HAART, your clinician will likely continue your treatment.
So there is a lot to consider here, and you should have discussions with both your obstetrician and HIV specialist to help determine what is best for you and your baby. Assuming that you have an HIV specialist, your specialist will refer you to an obstetrician who has experience with HIV-positive mothers. If you don’t have a specialist, now might be a good time to seek one out.
LOWERING THE RISK DURING LABOR AND DELIVERY
Again, the goal is to limit the baby’s exposure to the virus. So it’s probably not surprising that your options for labor and delivery depend upon your viral load (another important reason to take your HIV meds as prescribed). It is also recommended for women who did not receive HIV medication during pregnancy. In these situations, ACOG recommends a scheduled C-section at 38 weeks’ gestation in order to decrease the likelihood of onset of labor or rupture of membranes before delivery.
To help prevent transmission, your baby will be given liquid AZT immediately after birth and this will be continued (by you at home) twice a day for six weeks, HIV can also be transmitted to a baby through food that was pre-chewed by an HIV-positive mother (or caretaker). To be completely safe, babies should not be fed pre-chewed food.
DOES THE BABY HAVE HIV?
There are two types of tests that will be performed on your baby to find out if he or she has HIV. The first is the HIV antibody test. All babies born to a mom with HIV will test positive for the first several months of their lives. This does not mean that they have HIV. Rather, it means that the baby has simply been exposed to his/her mother’s HIV. The second test, PCR testing, looks for the virus and not just the antibodies to the virus. It is this test that can tell whether the baby has HIV or not. This test will be done during the first few days of his/her life.
The PCR test will be repeated several times on your baby. To know for certain that your baby is not infected with HIV, the baby must not be breastfeeding and must have two negative PCR tests, the first at one month (or older) and the second at four months (or older). Many experts confirm the HIV-negative status of the baby with an HIV antibody test at age 12 to 18 months. To be diagnosed with HIV, a baby must have two positive PCR tests.
Again, just because you have HIV does not mean you can’t have a healthy pregnancy and baby. In fact, obstetrician from Regency Medical Centre confirmed to serve an HIV-positive patient who followed her regimen and had a healthy pregnancy, and an uncomplicated vaginal birth. She and her husband welcomed a healthy HIV-negative baby into the world. It can be done, and it is done by lots of women.

WAASI WATEKA UWANJA WA NDEGE GOMA, CONGO, MJI WARINDIMA MILIO YA RISASI...!


Msemaji wa kundi la M23, Kanali Vianney Kazarama ameliambia shirika la habari la AP kwa njia ya simu kwamba sasa waasi wanapambana kuudhibiti mji wote wa Goma, baada ya kufanikiwa kuudhibiti uwanja wa ndege na kwamba sasa wako ndani ya mji wa Goma.
Pia akizungumza leo, Mbunge wa jimbo la Kivu Kaskazini, Mayombo Omary Bin Fikira amethibitisha kwamba waasi wameutwaa uwanja huo wa ndege. Mbunge huyo anasema kwa sasa hali ni ya kutatanisha katika mji wa Goma na milio ya risasi imekuwa ikisikika.

KILIMANJARO STARS WAJINOA KWENYE TUSKER CHALLENGE CUP...!





Wachezaji wa Kilimanajro Stars inayoiwakilisha Tanzania Bara wakiwa mazoezini katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Kombe la Tusker CECAFA Challenge yanayotarajiwa kuanza Jijini Kampala, Uganda Jumamosi hii. Timu hii inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

VODACOM YAICHANGIA HOSPITALI YA CCBRT SH. BILIONI NANE ...!

 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akionesha cheki ya Shilingi bilioni nane iliyotolewa na Kampuni ya VODACOM Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa hospitali maalumu itakayo shughulika kutibu wanawake walioathirika na Ugonjwa wa Festula pamoja na ulemavu mwingine. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe.Janet Mbene, Mkurugenzi Mtendaji VODACOM Tanzania Bwana Rene Meza, Ofisa mtendaji Mkuu Hospitali ya CCBRT Bwana Telemans Erwin na kulia ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik

Picha na Freddy Maro Ikul.

BARCA NDANI 16 BORA ZA UEFA, MESSI AJIONGEZEA REKODI...!


Jumanne ya jana, tarehe 20, timu ya Barcelona ilifuzu kuingia mzumguko wa pili wa hatua ya timu 16 bora zitakazo cheza kwa mtoano katika UEFA Champions League,

Barca ilifuzu kwa kuifunga Spartak Moscow kwa goli 3-0, magoli mawili yakiwekwa kimiani na Lionel Messi.

Magoli hayo yamemwezesha Messi kufikia rekodi ya Ruud van Nistelrooy ya kuwa na magoli 56 barani Ulaya kwa pamaja wakiwa nafasi ya pili huku No 1 akiwa ni Raul kutoka Uhispania.

Rekodi nyingine ni kuweza kufunga magoli 19 katika miji tofauti tofauti barani Ulaya.

Tuesday, November 20, 2012

HIVI NDIVYO VINYWAJI NANE AMBAVYO NI HATARI KWA AFYA YAKO....!

Whether you’re trying to lose weight, maintain weight loss or adopt a healthier lifestyle, watching your beverages is a must.

Because it doesn’t involve sitting down at a table or chewing, most of us don’t pay much attention to the liquids we pour into our bodies, but we should!

Here is a list of eight of the worst offenders:

1. Juice drinks – Most are loaded with sugar; choose only those labeled 100% juice.

2. Soda – The overconsumption of sodas has been linked to obesity. Occasional diet sodas are OK, but there are better choices for filling up your daily beverage intake.

3. Frozen mixed drinks – The mixers are the culprit here, usually filled with artificial colors, flavors and sweeteners.

4. “Healthy” fruit smoothies – Premade fast-food smoothies don’t always have real fruit and are loaded with sugar. For a healthier option, make your own so you can control the ingredients.

5. Hard liquor – After 2 drinks, your risk of obesity and other health problems increases. If you’re going to indulge, keep it limited.

6. Lemonade – Skip the ready-made lemonades and make your own minus the preservatives and artificial coloring. Opt for either less sugar or try honey to sweeten.

7. Sports drinks – The electrolytes are good when you’re sweating, but most drinks also have a lot of sugar and preservatives you don’t need.

8. Energy drinks –You may get an energy burst, but it will be a short-term fix because it’s from an overload of caffeine and sugar.

The best bet for quality beverages still includes natural water and herbal teas based on their nutritional values and calories.


 Source: www.fredynjeje.blogspot.com

WANAFUNZI WA ST. AUGUSTIN TAWI LA SONGEA WATISHIA KUGOMA...!

Wanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Cha St Augustin tawi la Songea wakilaumu chuo hicho kwa kutotoa ushirikiano kwa wanachuo hao kwa sera yao inayosema kuwa hawashughuliki na mikopo ya wanafunzi.
Kwani sera hiyo imepelekea hadi kutaka kuandamana kwa wanachuo hao kutokana na chuo kuchelewesha kutoa matokeo yao na kuyapeleka bodi ya mikopo ikiwa pamoja na majina ili waweze kupata mikopo .

Mmoja wa wanafunzi wa chuoni hapo amedai hadi sasa bado kuna matokeo amabayo hawaja yapata kutokana na mkufunzi ambaye ameyazuia kwa sababu hajalipwa mshahara wake. Vilevile ameshangazwa kwa sela hiyo ya chuo wakati baadhi ya matawi kama Tabora, Bukoba na Mwanza ambapo ni makao makuu ya Chuo wanaushirikiano na wanafunzo wa vyuo vyao pia wameshapata mikopo.
Kutokana na hali hiyo iliwabidi wanafunzi wa mwaka wa pili wachange elfu tano kwa kila mmoja aliwamkabidhi mmoja wa wahusika wa bodi ya mikopo ambaye pia ni mwanafunzi akashughulikie mikopo yao lakini bado iliwawia ngumu kutokana na kucheleweshwa kupelekwa kwa majina na matokeo yao.

Akiendelea kuzungumza mwanafunzi huyo amesma Naye Profesa Donatus Komba mbaye ni mkuu wa chuo aliondoka na majina pamoja na matokeo hayo ya wananchuo wa mwaka wa pili na kuyapeleka bodi ya Mikopo wakati yeye akielekea mwanza katika kikao, lakini pamoja na kupeleka majina na matokeo hayo kapeleka muda umekwenda cha ajabu hadi sasa mambo bado ni bilabila .


Chanzo: DEMASHONES BLOG

WALIOMUUA FUNDIKIRA WAHUKUMIWA KIFO ...!

Marehemu Swetu Fundikira





Watuhumiwa waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya Fundikira.

WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT - Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi leo wamehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam


Chanzo: globalpublishers

KESI YA LULU YAENDELEA KUPIGWA KALENDA...!

KESI ya msanii wa fani ya filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, imeendelea kupigwa kalenda kutokana na upelelezi wake kutokukamilika.Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwa marehemu Aprili 7, mwaka huu. Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Agustina Mmbando, jana ilitajwa mahakamani hapo lakini kwa mara nyingine upande wa mashtaka uliendelea kudai kuwa upelelezi haujakamilika.Wakati kesi hiyo ilipotajwa Novemba 5, mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilisha ili hatua nyingine ziweze kufuata, Wakili wa Serikali, Seth Sekwao alidai upelelezi haujakamilika.

Kutokana na taarifa hiyo ya upande wa mashtaka, mmoja wa mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Peter Kibatala alitaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo, ili iweze kusonga mbele.

Wakili Kibatala, ambaye pia ni Makamu Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alidai kila mara upande wa mashtaka umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika, jambo ambalo linaifanya kesi hiyo ishindwe kuendelea katika hatua nyingine.

“Ni muda mrefu sasa, kesi hii imekuwa ikitajwa mara kwa mara upande wa mashtaka umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika. Hivyo tunawakumbusha upande wa mashtaka ujitahidi kuharakisha upelelezi ili iweze kusonga mbele,” alidai Wakili Kibatala.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 3, mwaka huu itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.Lulu alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili 11, mwaka huu na kusomewa shtaka moja la mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.

Akimsomea shtaka hilo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Elizabeth Kaganda alidai Aprili 7, mwaka huu eneo la Sinza Vatcan alimuua msanii, Steven Kanumba. 


Chanzo: Mwananchi

JK AZINDUA MKAKATI WA MASWALA YA SIASA, ULINZI NA USALAMA MJINI ARUSHA...!


VIONGOZI WA SADC wakiongozwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya mrisho kikwete katika picha pamoja

Muheshimiwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania akifafanua jambo katika mkutano wa SADC uliofanyika leo katika hotel ya ngorudoto

kikundi cha ngoma kikitumbuiza nje ya hotel ya ngorodoto
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho kikwete leo amezindua rasmi mkakati wa pili utakao shirikisha nchi za SADC utakao shughulikia maswala ya Siasa,Ulinzi pamoja na usalama .

Akizindua mkakati huo wa nchi za SADC leo katika hotel ya Ngurudoto iliopo nje kidogo ya jiji la Arusha alisema kuwa huu ni mkakati wa pili kuzinduliwa kwani mnamo mwaka 2004 mkakati wa kwanza wa ushughulikiao maswala ya siasa ,ulinzi na usalama katika nchi za SADC ulizinduliwa ila ulikuwa haujitoshelezi kutokana na kuwepo kwa mapungufu mengi .

Aidha alibainisha kuwa mara baada ya nchi hizo kubaini kuwa mkakati huo unamapungufu waliamua kufanya tasmini upya kuanzia mwaka 2009 na nchi zote zilitoa maoni upya na kurekebisha sehemu ambazo zina mapungufu ambapo alibainisha kuwa katika mkakati uliopita kuna mambo mengi yalikuwa hayajaingizwa ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na mtikisiko wa uchumi hivyo kurekebisha na mara baad aya kukamilika waliamu kuupitisha upya na jana (leo) ndo wamezindua rasmi na umeanza kufanya kazi rasmi.

Alisema kuwa shughuli moja wapo ambayo mkakati huu wa SIPO utaanza nao ni pamoja na kutatua matatizo yaliyopo DRC kongo ambapo alisema kuwa nchi hii inakabiliwa na mapigano makali yanayowahusisha wahasi wa kikundi cha M23 ambapo inapigana kwa mda mrefu na serekali ya kongo hivyo wao kama umoja wa nchi za SADC wameshauriana na viongozi kuona ni namna gani wanaweza kuzuia mapigano hayo yasiendelee na si hivyo tu bali wanaangalia ni jinsi gani wataweza kuwasaidia wananchi wanaoteseka nchini kongo.

Kikwete alisema kuwa katika kutatua tatizo hili nchi za SADC kwa kushirikiana na nchi za jumuiya ya maziwa makuu walishakaa kuongelea tatizo hili na walishakaa nchini Adis ababa kuongelea tatizo hili pamoja na kampala hii yote ni kutafuta jawabu la kutatua mgogoro wa nchini kongo katika eneo la Gomu .

Adha kwa upande wa mgogoro wa nchi ya Malawi na Tanzania kama utaweza kutatuliwa na SADC alisema kuwa mgogoro huo bado haujafikia katika kiwango cha dunia kwani mapaka sasa bado nchi yetu inamazungumzo na malawi na iwapo muhafaka hautapatikana basi watapeleka huko ila ni mapema sana kwa sasa kupeleka swala hilo wakati mazungumzo bado yanaendelea.

"hili swala la malawi bado alijaletwa katika nchi za sadc kwani bado tupo katika mazungumzo na naamini kabisa tutaelewana ila ikishindikana basi tutaleta huku ili muafaka upatikane maana kazi ya mkakati huu au chombo hichi cha tulichokizundua leo ndo kinashughulikia maswala hayo "alisem kikwete

Aimalizia kwa kusema kuwa anaimani kuwa mkakati huu uliozinduliwa leo utaweza kusaidia nchi hizi zilizopo katika jangwa la sahara kwa kiasi kikubwa katika kupunguza mambo mbalimbali kama uhalifu.

Katibu mkuu wa SADC Tomaz Augusto Salomao alisema kuwa mkakati huo utaweza kusaidi nchi hizi zilizopo katika jagwa la sahara katika mambo mengi yakiwemo ya kiuchumi ,utamaduni,siasa pamoja na ulinzi