Banner
FOLLOW US FACEBOOK
propertyfinder.co.tz
Saturday, June 30, 2012
YANGA YAICHAPA EXPRESS YA UGANDA 2-1 KWENYE UWANJA WA TAIFA...!
Mechi kati ya Yanga
na Express ya Uganda,mpira umekwisha ambapo wenyeji Yanga wameshinda
magoli 2-1, mabao yote yakitiwa kimiani na
Jerry Tegete kipindi cha kwanza. Katika kipindi cha kwanza Yanga
ilitawala mchezo kwa
asilimia 60 dhidi ya Express hata hivyo katika kipindi cha pili mambo
yamebadilika ambapo timu ya Express ya Uganda imefanikiwa kupata goli
moja la kufutia machozi na kufanya matokeo kubaki hayohayo 2-1.
Kikosi
kilichoanza Yanga, kutoka kulia waliosimama Ally Mustafa 'Barthez',
Athumani Iddi 'Chuji', Said Bahanuzi, Oscar Joshua, Jerry Tegete na
Nizar Khalfan. Walioinama kutoka kulia ni Kelvin Yondan, Nadir
Cannavaro, Juma Abdul, Frank Damayo na Simon Msuva.
Wachezaji wa timu ya Yanga wakiingia uwanjani tayari kwa kumenyana na
timu ya Express ya Uganda kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa wajaa uwanjani kushuhudia wachezaji wapya wa timu hiyo kwenye uwanja wa Taifa.
RAIS KIKWETE AKUTANA NA WATENDAJI WAKUU WA MAKAMPUNI MBALIMBALI YA KIMAREKANI WANAOTEMBELEA TANZANIA...!
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi wa
Kimarekani na waalimu wao pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe John Haule, Balozi wa Marekani nchini,
Mhe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar.
Wanafunzi hao wanachukua masomo ya lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu
cha Zanzibar ( SUZA). Walikuwa wameongozana na Watendaji Wakuu wa
Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Rais Kikwete Ikulu
jijini Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa
ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour iliyoandaliwa na
ubalozi wa Tanzania Marekani
MUSTAFA HASSANALI AWAZAWADIA WASHINDI MISS DAR INTERCOLLEGE 2012...!
Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Mustafa akimkabidhi zawadi ya gauni lenye
thamani ya shilingi 300,000 Mshindi wa pili wa Miss Dar Intercollege
2012 Jamila Hassanofisini kwake leo,
anayeshuhudia ni mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail.
Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Mustafa katika picha ya pamoja na
wawakilishi wa kitongoji cha Miss Dar Intercollege katika shindano la
Miss Higher Learning 2012, Hilda Edward na mshindi wa pili Jamila Hassan
pamoja na mratibu Dina Ismail ofisini kwake leo,
It’s Over: Tom Cruise na Katie Holmes wapeana talaka...!

- Tom Cruise na Katie Holmes

- Tom Cruise na Katie Holmes

- Tom Cruise na Katie Holmes

- tom-cruise-katie-holmes-premiere-of-valkyrie-jan-09
Hatimaye ndoa ya waigizaji wakubwa kabisa wa Hollywood Tom Cruise na Katie Holmes imefikia tamati.
Holmes alitangaza jana kupitia mwanasheria wake kuwa amewasilisha nyaraka za talaka dhidi ya mume wake Tom Cruise waliyedumu naye kwa miaka mitano.
Habari hizo zimeushangaza ulimwengu wa filamu unaomchukulia Cruise kama kati ya waigizaji wanaofahamika zaidi.
Cruise aligundua kuwa Holmes ameanzisha mchakato wa talaka jijini New York wakati yeye akiwa anaigiza filamu huko Iceland.
“Tom amehuzunishwa sana na anawaangalia zaidi watoto wake watatu. Tafadhali wapeni muda wao kuyakabili hayo,” alisema msemaji wake.
Mwakilishi wake wa siku nyingi Bert Fields amesema Tom bado hajamwajiri wakili wa masuala ya talaka.
Holmes, 33, ameajiri makampuni mawili maarufu yaliyojikita kushughulikia talaka zinazohusisha utajiri mkubwa.
Cruise ameshawahi kuwa na wake wawili wengine wa Hollywood, Mimi Rogers na Nicole Kidman.
Kipato chake kwa mwaka kwa mujibu wa Forbes ni dola milioni 75.
Ray Azindua Filamu kwa Kutoa Msaada Kwa Yatima...!

Ray akikabidhi misaada.
Msaada huo ni sehemu ya mpango wa matukio ya uzinduzi wa filamu yake ‘Sobing Sound’ na pia kurudisha fadhila kwa jamii ambayo ndio wateja wakubwa wa filamu za kitanzania.
Filamu hiyo imezinduliwaa kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua ukumbini kama ilivyozoeleka na wasanii wengi, msanii huyo ameamua kuzindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5.
Akizungumza na www.bongo5.com mara baada ya kuzindua filamu hiyo, akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray, ambaye pia aliongozana na afisa masoko wa kampuni ya steps,bwana Ignatusu Kambarage ,alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutaabika, kitendo ambacho amesema, si kizuri.

Ray akiwa na watoto yatima
“Hii ni filamu ya kwanza kutoa, tangu kifo cha mwigizaji mwenzangu Steven Kanumba alipofariki dunia, Aprili mwaka huu, na najisikia furaha kuja hapa na kutoa msaada kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu” alisema Ray.
Flora Mvungi amkingia kifua H.Baba dhidi ya madai ya Irene Uwoya...!

Flora Mvungi
Baada ya mrembo na muigizaji wa filamu nchini Tanzania,Irene Uwoya kuliambia gazeti la Baabkubwa kuwa katika wanaume ambao hawezi kurudiana nao, H.Baba ni wa kwanza kwasababu ni ‘mchovu’ kitandani, mpenzi wake mpya Flora Mvungi ameibuka kujibu shutuma hizo.
Kupitia Clouds Fm jana, Flora amesema anamshangaa Irene kwa madai hayo, na kusema kuwa H.Baba humpagawisha kwa an ‘earth shaking and mind-blowing sex’ na huenda yeye (Irene) alikuwa anadate na H.Baba mwingine.
Flora amesema katika uhusiano wote na msanii huyo wa Bongo Flava amekuwa akiridhishwa na wala haoni hayo anayoyasema Irene.
Ameongeza kuwa anachojua yeye ni kuwa mapenzi ni kusikilizana na kuzungumza,kuheshiamiana,kujaliana na mwisho kabisa suala la kitandani ndio hufuata ambalo hata hivyo mzee wa ‘Mpenzi Bubu’ analimudu vyema.
Muigizaji huyo pia amesema anashangaa kwanini Irene ameendelea kuongea sana kuhusu mpenzi wake wa zamani H.Baba wakati kila mmoja ana maisha mapya na mpenzi mpya.
Amesema hafurahishwi na tabia hiyo ya Irene ya kumsema na kumzushia scandal H.Baba ambaye huwa hapendi kuzungumza mambo hayo hadharani, tena kwenye vyombo vya habari.
"Kipigo Kililenga Kumnyamazisha Ulimboka"- CWT...!
Na Pamela Chilongola,Issa Lazaro (SJMC)
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimesema tukio la kutekwa nyara na baadaye kujeruhiwa kwa Dk Steven Ulimboka, linalenga katika kuwanyamazisha wanyonge wanaodai haki zao.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumatano.
Katika tukio hilo watu wasiojulikana, walimteka nyara kiongozi huyo wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, akiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni na baadaye kupelekwa katika Msitu wa Pande ambako alipigwa na kujeruhiwa vibaya.
Tukio hilo limekuja wakati madaktari katika hospitali mbalimbali za Serikali, wakiwa katika mgomo usiokuwa na kikomo, wakishinikiza kulipwa maslahi bora.
Akizungumzia tukio hilo, Mukoba, alisema kitendo cha kutekwa nyara na kujeruhiwa kwa daktari huyo, si tu kwamba ni cha kuwanyamazisha wadai haki, lakini pia kimeidhalilisha Tanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiheshimu katika kuheshimu haki za binadamu.
“CWT inalaani sana kitendo cha kumwagiza bure kwa damu ya Dk Ulimboka, Msitu wa Pande unatumika kutesa na kuulia watu wasiokuwa na hatia, msitu huo unapaswa kuwa kielelezo na alama ya Watanzania wanaoamka kupambana na dhuluma inayotekelezwa na idadi ndogo ya watu dhidi ya umma wa Watanzania,”alisema Mukoba
Mukoba alisema CWT inahamasisha misingi ya kutetea haki za jamii na wafanyakazi ambazo zimekuwa zikimomonyoka.
Wakati huo huo, baadhi ya wananchi katika Jiji la Dar es Salaam, wamesema tukio hilo lililenga katika kumyamazisha Dk Ulimboka, katika jitihada zake za kudai haki wa madaktari.
.
Wakizungumza kwa nyakati na mahali tofauti jana, wananchi hao walisema lengo la watu waliofanya unyama huyo ni kudhoofisha nguvu za Dk Ulimboka, ili asiendelee kudai haki.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Furaha Alex, alisema kitendo hicho kimedhihirisha kuwa madaktari hapa nchini hawathaminiwi hapa wanapodai haki zao za msingi.
“Kitendo cha kupigwa kwa Dk Ulimboka, kimewadhalilisha sana madaktari hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa anawawakilisha wenzake. Hili ni jambo la kusikitisha saba,” alisema Alex.
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimesema tukio la kutekwa nyara na baadaye kujeruhiwa kwa Dk Steven Ulimboka, linalenga katika kuwanyamazisha wanyonge wanaodai haki zao.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumatano.
Katika tukio hilo watu wasiojulikana, walimteka nyara kiongozi huyo wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, akiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni na baadaye kupelekwa katika Msitu wa Pande ambako alipigwa na kujeruhiwa vibaya.
Tukio hilo limekuja wakati madaktari katika hospitali mbalimbali za Serikali, wakiwa katika mgomo usiokuwa na kikomo, wakishinikiza kulipwa maslahi bora.
Akizungumzia tukio hilo, Mukoba, alisema kitendo cha kutekwa nyara na kujeruhiwa kwa daktari huyo, si tu kwamba ni cha kuwanyamazisha wadai haki, lakini pia kimeidhalilisha Tanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiheshimu katika kuheshimu haki za binadamu.
“CWT inalaani sana kitendo cha kumwagiza bure kwa damu ya Dk Ulimboka, Msitu wa Pande unatumika kutesa na kuulia watu wasiokuwa na hatia, msitu huo unapaswa kuwa kielelezo na alama ya Watanzania wanaoamka kupambana na dhuluma inayotekelezwa na idadi ndogo ya watu dhidi ya umma wa Watanzania,”alisema Mukoba
Mukoba alisema CWT inahamasisha misingi ya kutetea haki za jamii na wafanyakazi ambazo zimekuwa zikimomonyoka.
Wakati huo huo, baadhi ya wananchi katika Jiji la Dar es Salaam, wamesema tukio hilo lililenga katika kumyamazisha Dk Ulimboka, katika jitihada zake za kudai haki wa madaktari.
.
Wakizungumza kwa nyakati na mahali tofauti jana, wananchi hao walisema lengo la watu waliofanya unyama huyo ni kudhoofisha nguvu za Dk Ulimboka, ili asiendelee kudai haki.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Furaha Alex, alisema kitendo hicho kimedhihirisha kuwa madaktari hapa nchini hawathaminiwi hapa wanapodai haki zao za msingi.
“Kitendo cha kupigwa kwa Dk Ulimboka, kimewadhalilisha sana madaktari hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa anawawakilisha wenzake. Hili ni jambo la kusikitisha saba,” alisema Alex.
BABA WA DR. ULIMBOKA AMWAGA MACHOZI...!
BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda
Baba wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda akilia na kufarijiwa
Usu Mallya akilia baada ya kushuhudia mzee Steven Mwaitenda akibubujikwa na machozi mbele yao
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (kushoto) akiwa na Mkuu wa
Kitengo cha
Habari na Mawasiliano, Lilian Liundi walipomtembelea Dk. Ulimboka
kumfariji jana
Mzazi akimlilia mwanaye Dk. Ulimboka kwa uchungu MOI
Baadhi ya wanaharakati anuai wakiwa na maua walipomtembelea
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka kumfariji jana
Baadhi ya wanaharakati wakiwa na nyoso za hudhuni baada ya kilio cha baba wa Dk. Ulimboka jana
BABA
wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda amejikuta
akiangua kilio kwa uchungu mbele ya wanaharakati ambao walimtembelea
mwanae, Dk. Steven Ulimboka kumpa pole kufuatia tukio la kutekwa na
kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana.
Hali
hiyo ilitokea jana jioni katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili
(MOI), ambapo wanaharakati kutoka taasisi na asasi mbalimbali za utetezi
wa haki za binadamu walifika kwa lengo la kumpa pole Dk. Ulimboka
kufuatia kitendo kilichomfika.
Mzee
Mwaitenda alijikuta akibubujikwa na machozi na kushindwa kuendelea
kuzungumza alipokuwa akitoa shukrani kwa wanaharakati hao, kwa niaba ya
mwanaye ambaye wanaharakati hao walishindwa kumuona wote kutokana na
hali yake ilivyo sasa.
“Niseme
wazi nimefarijika sana kwa ujio wenu kumwona mwanangu dhidi ya mambo ya
kikatili aliyofanyiwa akitetea haki za wengine…,” alisema mzee
Mwaitenda kabla ya kushindwa kuendelea na kuangua kilio mbele ya
wanaharakati.
Baada
ya tukio hilo baadhi ya wanaharakati walimshika wakishirikiana na
wanafamilia ya mzee Mwaitenda na kumbebeleza kisha kumtoa mbele ya
mkusanyiko huo wa wanaharakati na kumrudisha wodini huku wakimfariji.
Wakizungumza
mara baada ya tukio hilo wanaharakati wameelezea kusikitishwa na
vitendo vinavyoendelea MOI eneo ambalo amelazwa kiongozi huyo wa
madaktari ambavyo vimeendelea kutishia usalama wa Dk. Ulimboka.
Akifafanua
zaidi mwakilishi wa wanaharakati hao, Markos Albania alisema taarifa
walizozipata usiku wa juzi kuna wagonjwa ‘feki’ ambao walijitokeza MOI
huku wakitaka kulazwa wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) alipolazwa Dk.
Ulimboka lakini baadaye waligoma kuingizwa wodini.
“Wapo
wagonjwa ambao waliletwa na kutaka kupelekwa ICU moja kwa moja…kuna
watu wanakuja usiku wa manane wakitaka kumtembelea Dk. Ulimboka…matendo
yanayoendelea kutokea ukilinganisha na kauli za Serikali zilizotolewa
bungeni yanatishia usalama na uhai wa mgonjwa,” alisema Albania.
Aidha
amesema kitendo cha vyombo vya usalama kuendelea kumuhoji Dk. Ulimboka
akiwa hoi hospitalini si vya kiungwana kwani tayari muhusika amewataja
hadi kwa majina watu ambao anawashuku lakini hadi sasa hakuna
aliyechukuliwa hatua yoyote.
Pamoja
na hayo wanaharakati hao wameitaka Serikali kuunda tume huru
mchanganyiko na raia ambayo itachunguza kiundani suala hilo, kwani
hawana imani na Jeshi la Polisi ambalo limedai kuunda timu ambayo
inachunguza kwa kina suala hilo.
Dk.
Ulimboka ambaye ni kiongozi wa madaktari ambao wanaendelea na mgomo wan
chi nzima kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao alitekwa juzi na
watu wasiojulikana na kupigwa na kuteswa kikatili kabla ya kutelekezwa
katika msitu wa Mabwepande.
Friday, June 29, 2012
WAZIRI WA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO,MH.DKT. FENELLA MUKANGARA AMEPATA AJALI MBAYA....!
Mh.Dkt. Fenella Mukangara
Mh. Mukangara anasema chanzo chake ni kuchomekewa na basi moja la abiria (ambalo hakulitaja jina lake).
Hapa namnukuu "Ni kweli tumepata ajali hapa maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati tukiwa njiani kuelekea jijini Mwanza ambako leo kunafanyika ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Darts, tunashukuru Mungu wote tumetoka salama japo tumepata majeraka katika sehemu mbali mbali za mwili."mwisho wa kunukuu.Tunaendelea kuwasiliana na Mh. Mukangara na tutaendelea kupeana taarifa zaidi.
MPANGO MZIMA SERENGTI FIESTA 2012...!
Kwenye picha ni Mratibu wa Fiesta "Sebastian Maganga" na aliyevaa
tisheti ya serengeti ni brand meneja wa bia ya Serengeti Alan Chonjo.
wakiwa na wadu wengine wa Serengeti.
dizaini inakua hivi
tuna story kuhusu Serengeti Fiesta 2012 Muonekano Mpya burudani ile ile bhaaasss
Shangwe zinaanzia Arusha kesho Jumamosi ya Kesho Kiwanja cha Mawingu club Hapo tunakutanisha vipaji
eh bana bhaaasss ni kucheza ku dance kuruka ngoma kiduku kibega mtindo mmoja hapo ni kattika mchakato wa kutafuta wakali watakao dance katika screen stage ya fiesta na jumapili ndo balaaa hapo ni washika mic hapo tunatafuta star wapya kwa mwaka huu wa 2012 ambapo watagonga ngoma kwenye jukwaa la kioo la Fiesta
xo wanyamwezi wa Arusha, R chuga, R yeyo, A masive, A town
Tukutane Mawingu Club buruani ile ile Bhaaassss
RAY, MAINDA WABAMBWA LAIVU...!
Na Shakoor Jongo
MASTAA
wawili katika tasnia ya filamu Bongo ambao wanatajwatajwa kuwa ni
wapenzi wa siku nyingi, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Ruth Suka ‘Mainda’
juzikati walinaswa ‘live’ katika mapozi yaliyoacha vingi viulizo.
Wawili hao walibambwa ndani ya Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempinski, Posta jijini Dar, usiku wa Juni 23, mwaka huu kulikokuwa na uzinduzi wa Filamu ya Super Star ya Wema Sepetu.
Wakiwa ukumbini hapo, Ray alionekana akimshika mkono Mainda kama mtu aliyemtaka waondoke lakini pia akaonekana akimnong’oneza jambo demu huyo.
Haikuweza kufahamika mara moja walichokuwa wakiteta lakini baada ya muda, msanii Steven Mangere ‘Nyerere’ alitokea na kumkumbatia Mainda huku akitaka kuondoka naye.
Wakati Steve akifanya hivyo, Ray alionekana akimuonya kitu Mainda huku akimnyooshea kidole ambapo mdau mmoja aliyekuwa ukumbini hapo alisikika akisema: “Mh! Sijui huyu Ray na Mainda bado ni wapenzi au wameshabwagana, maana mapenzi ya mastaa yamekuwa ni kizungumkuti siku hizi.”
Ijumaa lilizungumza na Mainda kutaka kujua kama bado anatoka na msanii huyo lakini alijibu kwa kifupi: “No Comment.”
Wawili hao walibambwa ndani ya Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempinski, Posta jijini Dar, usiku wa Juni 23, mwaka huu kulikokuwa na uzinduzi wa Filamu ya Super Star ya Wema Sepetu.
Wakiwa ukumbini hapo, Ray alionekana akimshika mkono Mainda kama mtu aliyemtaka waondoke lakini pia akaonekana akimnong’oneza jambo demu huyo.
Haikuweza kufahamika mara moja walichokuwa wakiteta lakini baada ya muda, msanii Steven Mangere ‘Nyerere’ alitokea na kumkumbatia Mainda huku akitaka kuondoka naye.
Wakati Steve akifanya hivyo, Ray alionekana akimuonya kitu Mainda huku akimnyooshea kidole ambapo mdau mmoja aliyekuwa ukumbini hapo alisikika akisema: “Mh! Sijui huyu Ray na Mainda bado ni wapenzi au wameshabwagana, maana mapenzi ya mastaa yamekuwa ni kizungumkuti siku hizi.”
Ijumaa lilizungumza na Mainda kutaka kujua kama bado anatoka na msanii huyo lakini alijibu kwa kifupi: “No Comment.”
RECHO AZABWA VIBAO NA MPENZI WAKE...!
Rachel Mrisho ‘Recho’.
KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu Bongo, Rachel Mrisho ‘Recho’ hivi karibuni alijikuta akizabwa vibao na mpenzi wake aitwaye Saguda baada ya kutokea hali ya kuzinguana.
Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu kwenye Hoteli ya Hayyat Regency (zamani Kilamanjaro Kempinski Hotel) mishale ya saa 7 usiku, chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
Awali, Saguda na Recho walionekana wakizozana wakati wakitoka kwenye hoteli hiyo kulikokuwa na uzinduzi wa filamu ya Wema ya Super Star.
Mara Saguda akamnasa vibao Recho, kitendo kilichomfanya demu huyo aangue kilio na kuondoka eneo hilo akiwa amenywea.
Jitihada za paparazi wetu kuongea na mmoja kati ya wawili hao hazikuzaa matunda ila rafiki wa Recho aliyeomba hifadhi ya jina lake alilitonya Ijumaa kuwa, chanzo cha Saguda kutoa kipigo hicho ni baada ya kuhisi anasalitiwa.
JACK WA CHUZ ADAIWA KUTAMBA NA MAGARI YA KUKODI...!
Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’.
MKALI wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ amechafuka baada ya kudaiwa kukodi magari ya watu na kudai ni yake.
Habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa msanii huyo zilisema kuwa, ili aonekane naye ni matawi ya juu, Jack hukodi magari kila siku baada ya kuona marafiki zake kadhaa wanatanua na mikoko ya kifahari.
“Namshangaa rafiki yangu Jack, amekuwa na kawaida ya kukodi magari na kuzunguka nayo katika ‘mishemishe’ zake na huwaambia watu kuwa ni yake,” alisema swahiba huyo wa Jack aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimpigia simu staa huyo na kumsomea tuhuma zake ambapo alisema:
“Jamani, kwani mimi sina uwezo wa kununua gari mpaka nitumie magari ya kukodi. Sijui watu wananionaje mimi, nakuambia mwandishi huwa sina kawaida ya kubadili magari bali natumia la kwangu.”
WEMA, OMOTOLA WASHINDANISHA MAKALIO...!
Wema Sepetu (kushoto) wakati
akimpokea mgeni wake ambaye ni mwigizaji na mwanamuziki kutoka nchini
Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
STAA asiyeishiwa vituko, Wema Sepetu na mgeni wake kutoka Nigeria ambaye ni msanii, Omotola Jelade juzikati walitoa kali baada ya kushindanisha ukubwa wa makalio yao.
Tukio hilo lililowavutia wengi lilichukua nafasi kwenye Hoteli ya Giraffe iliyopo Mbezi jijini Dar kulikokuwa na uzinduzi wa filamu ya Wema iitwayo Super Star.
Wakati wakishuka ngazi zilizopo kwenye hoteli hiyo, Omotola alionesha kuvutiwa na umbile la Wema ambapo alisema anahisi mwenzake huyo ana ‘inye’ kubwa kuliko yake.
Baada ya Omotola kusema hivyo, Wema alionekana kutaka kupinga lakini kabla ya kufanya hivyo, Omotola alisimama sambamba na mwenyeji wake huyo kwa lengo la kuangalia nani zaidi na mjadala uliishi kwa Wema kuonekana alimfunika super star huyo wa filamu kutoka Nigeria.
RIPOTI KAMILI KUHUSU DR. ULIMBOKA...!


Dk Ulimboka akiendelea kupata
matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI)
kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
NYUMA ya kipigo alichopewa kiongozi wa madaktari ambao wako kwenye mgomo nchi nzima, Dk. Steven Ulimboka kuna siri nzito, Ijumaa lina ripoti kamili.
Gazeti hili lilinyetishiwa mkanda mzima na mtu aliyekuwa na Dk. Ulimboka (jina tunalo ambaye naye ni daktari) usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
MUVI LA MATESO LAANZA
Jamaa huyo alidai kuwa, wakiwa viwanjani hapo wakipooza koo, walifika watu watano waliojitambulisha kuwa ni askari wakiwa na silaha ambapo walidai kuwa walimfuata Dk. Ulimboka na kumwambia anatakiwa Kituo cha Polisi Kati (Central).
Ilidaiwa kuwa Dk. Ulimboka alishurutishwa kupanda kwenye gari leusi ambalo halikuwa na namba za usajili na kuondoka eneo hilo huku akiacha gumzo kuwa Central anapelekwa kwa ishu gani.
Ikadaiwa kuwa baada ya Dk. Ulimboka kuchukuliwa, marafiki zake walitoka spidi kuelekea Central kujua kulikoni na pia kumwekea dhamana.
Jamaa huyo alidai kuwa marafiki zake walipofika Central hawakumkuta na wala hakukuwa na dalili za Dk. Ulimboka kufikishwa mahali hapo.
Aliendelea kudai kuwa walianza kufanya mawasiliano usiku huo ili kujua rafiki yao alipelekwa wapi lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda.
SIMU HAIPATIKANI
Alidai wakiwa Central, askari mmoja aliwataka kutulia hadi asubuhi wangepata taarifa kamili kwani kwa wakati huo hata simu yake ilikuwa haipatikani.
Jamaa huyo alidai kuwa saa 12:00 asubuhi alipokea simu kutoka kwa msamaria mwema aliyekuwa maeneo ya Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar akamwambia kuna mtu amemkuta akiwa taabani ambaye alimtajia namba kwa shida ili aipige na kutoa taarifa ya hali yake.
“Alisema alimtajia namba tu na hakumsemesha tena,” alisema rafiki huyo wa Dk. Ulimboka.
Alidai kuwa baada ya kujulishwa habari hiyo alitaka aende mwenyewe lakini alipoomba ushauri watu walimsihi asiende peke yake.
Jamaa huyo alisema alitafuta watu akaenda nao na walipofika huko walimkuta Dk. Ulimboka aliyechukuliwa akiwa mzima hajitambui na hakuwa na uwezo wa kuzungumza.
Alisema kuwa baada ya kumuona mwenzao alivyochakazwa, wakamchukua na kumpeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Bunju ambapo yule msamaria mwema alitoa maelezo jinsi alivyomkuta.
Rafiki huyo wa Dk. Ulimboka alidai kuwa, katika maelezo ya yule msamaria mwema alisema kuwa alishtuka alipomkuta akiwa porini na hali mbaya huku akiwa amefungwa kitambaa cheusi usoni na kutapakaa madonda mabichi mwili mzima.
Baada ya kuchukuliwa maelezo walipatiwa PF-3 ambapo walifanya jitihada za kumkimbiza katika Hospitali ya Muhimbili kwa kutumia ambulance ya AAR, alipofikishwa tu madaktari wenzake walianza kumpa matibabu ya hali ya juu ili kunusuru uhai wake huku mgomo wao ukiendelea.
MTU ALA KIPIGO
Wakati anafikishwa Muhimbili tayari wanaharakati mbalimbali walishajitokeza ili kumpokea lakini mara baada ya kufikisha mtu mmoja aliyesadikiwa kuwa ‘njagu’ aliingia chooni na akasikika akizungumza na simu.
Ilidaiwa kuwa katika mazungumzo yake alisikika akisema kumbe jamaa hajafa, jambo lililoibua hisia kwamba alijua kilichoendelea.
Ilisemekana kuwa watu waliomsikia wakamchomoa na kumpa kipigo cha mbwa mwizi hadi Radio Call inayotumiwa na polisi ikamchomoka kwenye suruali kabla ya askari waliokuwa doria kumwokoa na kuondoka naye.
KOVA ATHIBITISHA
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo linalodaiwa kuwa la utekaji na kuongeza kuwa uchunguzi unafanyika na sheria itachukua mkondo wake dhidi ya wahusika.
Wananchi waishauri serikali
Wakiongea na Ijumaa mara baada ya tukio hilo kutokea, baadhi ya wananchi wameitaka serikali kuhakikisha uchunguzi wa kina na wa haraka unafanyika na ripoti yake kuwekwa hadharani ili kuondoa utata uliotawala.
Imeandaliwa na Haruni Sanchawa, Issa Mnally na Makongoro Oging.
NAKAAYA ALIA KUPORWA BWANA...!
Nakaaya akiwa na Peter.
Nakaaya Sumari.
Na Musa MatejaMWANAMUZIKI Nakaaya Sumari, juzikati alimwaga machozi huku akidai kuibiwa bwana’ke na mwanamke mwenzake aliyemtaja kwa jina la Beatrice, Ijumaa linakupa mchapo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Nakaaya amekuwa hana raha baada ya kuzidiwa ujanja na Beatrice ambaye inadaiwa ni mzazi mwenza wa mwanaume huyo anayetajwa kwa jina la Peter.
“Yaani Nakaaya hana raha kabisa baada ya kuchukuliwa bwana wake. Lakini sisi uhusiano wake na Peter hatukuwa tunaujua na inaonekana walikuwa wakitoka kwa siri sana,” alisema sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake .
Ijumaa lilipozinasa habari hizi lilimwendea hewani msanii huyo ambaye alipopatikana alitoa ushirikiano kwa paparazi wetu akisema:
“Ni kweli kumetokea msuguano kati yangu na Peter ambaye nilikuwa nampenda sana na tukadumu kwa miaka miwili, lakini niligundua amempa mimba mwanamke mwingine,” alisema Nakaaya na kuongeza:
“Mimi sitaki shari naye kwa kuwa tabia yake haijanifurahisha, nina mambo mengi ya kufanya kama Peter bado anamzimia basi waendelee ila Beatrice asiwe ananisumbua maana nimechoka na mapenzi ya kushea bwana, bora nizame kwenye game la muziki kama mwanzo,” alisema Nakaaya.
Kwa upande wa Peter, alipoulizwa kuhusu madai hayo, alikiri na kusema kuwa ameamua kuendeleza uhusiano wake na Beatrice ambaye yuko naye kwa zaidi ya miaka mitano baada ya kuona Nakaaya haelekei.
“Nilikuwa nampenda sana Nakaaya lakini nimeshindwa baada ya kusikia ana bwana mwingine wa Kizungu, nisingeweza kuendelea naye bora niendelee kudili na kazi zangu na maisha mengine, mapenzi ya ki-supastaa yamenishinda,” alisema Peter.
BREAKING NEWS MADAKTARI 72 WATIMULIWA KAZI -MBEYA...!
![]() |
| Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao |
![]() |
Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya
|
BODI
ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari
72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume
cha makubaliano ya mkataba.
Imeelezwa
kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba
wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale
walioajiriwa na Wizara ya afya.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku
tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu
namba F.16-F17 na F. 27.
"Hivyo
kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa
mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa
hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe
23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na
Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern
doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.
Alisema,
kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54
na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo
tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili
hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.
Sigara,
aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari
ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili
namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.
Alisema,
baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili
waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu
kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za
kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi
"Iwapo
madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo
tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari
hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,"alisema.
Aidha,
alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani
ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi
imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.
Hata
hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa
kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano
wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.
TAKE OVER FRIDAYS THE FLYERS COLLEGE NIGHT IN THE CITY...!
TEXT 0655364409 FOR FREE PASSES AND BOTTLE SERVICE ..
Date/Time : This Friday June 29TH 9pm to 5am
Displayed Title: Take over Fridays the flyest college night in the city
Music By: Dj benny, D dj 91 , dj pachee
Music Style: Naiga music, Bongo fleva,RNb, hiphop, house, reggae, classics, freestyle and reggaeton
Cost: all the college students 5000 Tshs free transpotation (Free guestlist )
Age: 18 t0 21
Displayed Title: Take over Fridays the flyest college night in the city
Music By: Dj benny, D dj 91 , dj pachee
Music Style: Naiga music, Bongo fleva,RNb, hiphop, house, reggae, classics, freestyle and reggaeton
Cost: all the college students 5000 Tshs free transpotation (Free guestlist )
Age: 18 t0 21
ON CLUB AQ for the largest friday night party in Arusha Town.Well
over 400 beatiful young men and woman from in and around arusha.same
even travel from moshi and dar just to experience the thrills that
occur every friday night.the best entertaiment including stage dances
whose visually erotic and exciting gyrations get you in the mood to
dance.The friendlyness of the club staff helps to break the ice for
everyone so finding a partner is very easy at club aq
over 400 beatiful young men and woman from in and around arusha.same
even travel from moshi and dar just to experience the thrills that
occur every friday night.the best entertaiment including stage dances
whose visually erotic and exciting gyrations get you in the mood to
dance.The friendlyness of the club staff helps to break the ice for
everyone so finding a partner is very easy at club aq
JOIN CLUB AQ for the largest friday night party in Arusha Town.Well
over 400 beatiful young men and woman from in and around arusha.same
even travel from moshi and dar just to experience the thrills that
occur every friday night.the best entertaiment including stage dances
whose visually erotic and exciting gyrations get you in the mood to
dance.The friendlyness of the club staff helps to break the ice for
everyone so finding a partner is very easy at club aq..
over 400 beatiful young men and woman from in and around arusha.same
even travel from moshi and dar just to experience the thrills that
occur every friday night.the best entertaiment including stage dances
whose visually erotic and exciting gyrations get you in the mood to
dance.The friendlyness of the club staff helps to break the ice for
everyone so finding a partner is very easy at club aq..
Subscribe to:
Posts (Atom)
























