Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 31, 2012

Mh. JOSHUA NASSARI ATISHIA KUYASHTAKI MAGAZETI....!

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (pichani), ametoa siku 14 kwa magazeti mawili yatolewalo kila siku nchini kumsafisha kwa uzito waliotolea habari ya kumhusisha kufyatua risasi kwenye kata ya Daraja Mbili wakati wa uchaguzi mdogo, vinginevyo atayashitaki Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Akizungumza na vyombo vya habari jijini hapa jana, alisema ameshangazwa kuona propaganda chafu dhidi yake zikiendeshwa kwa wazi na chuki kubwa. “Mimi nilipita eneo la kupigia kura saa mbili kamili asubuhi nikaend kata ya ya Bang’ata wilayani Arumeru nikiwa kama wakala mkuu, kusimamia uchaguzi na tukio hili la kufyatua risasi limetokea mchana saa saba, nashangaa naandikwa mimi,” alisema.

Alisema kuwa kikubwa anachokiona ni kumpaka matope kupitia magazeti hayo. Nassari alisema kuwa anachofahami fika magazeti hayo kupitia waandishi hao wanatumiw ana watu kumchafua kwa sababu wanazojua wao, kufuatia kushinda uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
“Kwa kweli sasa sitakubaliana kamwe na tabia hii, maana nachafuliwa kwa makusudi na kusababisha wapiga kura wangu wajenge chuki dhidi yangu, alisema.

Kamanada wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabasi, alipoulizwa alisema: “Mimi silijui suala hili, nimesikia katika vyombo vya habari, ninachojua mimi risasi zilifyatuliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu, Wilaya ya Arusha (NEC), Godfrey Mwalusamba wakati akimwokoa Mussa Hamisi, aliyekatwa panga, wakati akimwokoa mama mmoja aliyedaiwa kugawa pesa za kuhonga, wapiga kura wa Daraja Mbili ili kuipigia CCM,”alisema.


Alisema Mwalusamba alilazimika kufyatua risasi baada ya kumwona Mussa Hamisi, akikatwa panga na kundi la watu hao walitawanyika na kuwa watu wanane walitiwa mbaroni.


Chanzo: Nipashe

KIONGOZI WA UPINZANI RWANDA AHUKUMIWA JELA...!






Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire (pichani) amehukumiwa miaka minane gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kosa la uhaini

Viongozi wa mashtaka walitaka afungwe maisha jela kwa kutishia usalama wa nchi.Mahakama imempata na hatia ya kupuuza mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994.Ingabire hakuwa mahakamani wakati hukumu ilipotolewa dhidi yake kwani amekuwa akisusia kuhudhuria vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo akisema imeshinikizwa ksiasa,.Alikamatwa mwezi Aprili mwaka 2010 na kuzuiwa kushiriki uchaguzi uliofanyika mwaka huo.

Chanzo - BBC Swahili

Tuesday, October 30, 2012

BAADHI YA PICHA ZNAZOONYESHA UHARIBIFU ULIOSABABISHWA NA KIMBUNGA CHA SANDY HUKO MAREKANI...!

Kimbunga Sandy ni kimbunga ambacho Marekani haijawahi kukishuhudia kwa miaka tisa iliyopita ambapo kwa mujibu wa Sky News ni watu 16 wamepoteza maisha mpaka sasa na nyumba zaidi ya 50 zimewaka moto huku mamilioni ya wananchi wakikaa bila umeme majumbani mwao. Kutokana na hiki kimbunga pia safari za ndege zaidi ya eflu zimeahirishwa ambapo kwa upande mwingine nyumba laki sita na elfu sabini kwenye jiji la New York zimeachwa bila umeme.
 





 
Chanzo: www.thisisdiamond.com

DIWANI AWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA KUJISHUHULISHA...!

 Zainab Maeda, Iringa.

       WATENDAJI wa serikali za mitaa wamewatakiwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii ili kuleta maendeleo. Sambamba na hayo Diwani wa kata ya Mtwivila aliwataka kutokuwa na kauli za uwongo wakati wakipigiwa simu na viongozi wa juu au wananchi.

       Aliyabainisha hayo, Diwani wa kata ya Mtwivila manispaa ya Iringa,
Vitus Sabas Mushi wakati wa mkutano wake pamoja na watendaji hao kilichofanyika kwenye  ofisi ya mtendaji katika kata hiyo.

         Mushi alisema kata hiyo inamazingira machafu hali ambayo yanaeza
kusababisha mlipuko wa magonjwa, pia kata hiyo inakabiliwa na uhaba wa maji .

       Alifafanua kuwa wanampango wa kuboresha ofisi ya kata hiyo pamoja na
barabara zilizopo kwa kuweka matuta madogo na makubwa ili kuzuia ajali ambazo zinasababishwa na mwendo kasi wa magari.

      Wakati akihojiwa na chanzo chetu  mtendaji wa kata hiyo Angela Mtimwa
alisema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili mambo mbalimbali kama ujenzi wa kituo cha polisi, ukarabati wa ofisi hiyo ya mtendaji ujenzi wa kituo cha afya, mfuko wa elimu pamoja na ukusanyaji wa mapato.

      Aidha alisema changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ni wakati wa ukusanyaji wa
mapato wananchi hawapatikani katika maeneo yao hali ambayo inawalazimu kutumia gharama kubwa kwa kuwatafuta wanaohusika na majengo hayo kwa kuwapigia simu.

Nape amvaa tena Dr.Slaa ..!


*DR. SLAA AMECHANGANYIKIWA: Nape

*Adai amekubuhu kwa utapeli wa kisiasa

*Amtuhumu kuiua Chadema

*Asema si M4C tena bali ni M4D

Tarehe 28/10/2012 kumefanyika uchaguzi mdogo katika kata 29 kwenye mikoa mbalimbali nchini. Kata hizi zilikuwa wazi kwa sababu mbalimbali, hivyo kwa mujibu wa sheria ililazimika kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi wazi.

Ukiacha matukio kadhaa ya vurugu, maeneo mengi uchaguzi umeenda kwa utulivu. Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza wote waliofanya uchaguzi kwa amani na utulivu, huo ndio utamaduni wa watanzania, kushindana bila kupigana.

Muhutasari wa matokeo ya jumla unaonyesha kuwa TLP wameshinda kata moja(1), CUF wameshinda kata moja(1), CHADEMA wameshinda kata 5 na CCM imeshinda kata ishirini na mbili(22).

Kwa matokeo haya ambayo kwakweli yanatafisiri pana sana hasa ikizingatiwa kuwa mgawanyo wa kata ulikuwa nchi nzima basi matokeo haya yanatoa ujumbe wa jinsi CCM inavyokubalika nchini kwasasa.

Na pia ni uthibitisho wa kile kilichoitwa M4C(movement for change) kwa Chadema kuwa ni kiini macho kisichokuwa na matunda chanya bali ni M4D ( movement for dealth). Na hii inatokana na aina ya siasa za hovyo zinazoambatana na operesheni hii. Bila shaka sauti ya Watanzania kwa aina hii ya siasa imesikika bila kumumunya maneno.

Aidha kwa upande mwingine siasa za uongo,uzushi na ulaghai zilizotumiwa na vyama vya upinzani hasa Dr. Slaa kwenye kampeni hizo imekidhalilisha chama hicho na kudhalilisha utu uzima wa Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Mfano mzuri ni pale ambapo Dr. Slaa bila ya soni alipoamua kumzushia Rais na Mwenyekiti wa CCM kuwa kasafiri mpaka China eti kwenda kumuokoa mwanae ambaye kwa madai ya Dk. Slaa alikamatwa na madawa ya kulevya nchini humo.

Bila aibu Dr. Slaa alizusha uongo huo Tabora kwa wapiga kura huku akijua kuwa ni uongo, lakini hata hivyo uongo huo hauna sehemu kwenye kampeni hizo za udiwani. Wananchi walitegemea kusikia namna ya kutatua kero zao badala yake wakashuhudia mtu mzima akizusha ujinga wa ajabu.

Uongo huu na mwingine mwingi unathibitisha kuwa Dr. Slaa anazeeka vibaya kwani kila anavyoongeza siku hamu na tamaa yake ya kusema uongo ili kujiongezea umaarufu na kujenga chuki kati ya watanzania inaongezeka sana. Hakika TAPELI HUYU WA KISIASA, LICHA YA KUZEEKA VIBAYA SASA ANACHANGANYIKIWA.

Naamini mzigo aliotwishwa na wenzake unamlemea sana, hivyo namshauri awaachie vijana wajaribu kukiokoa chama hicho kinachoporomoka kwa kasi, vinginevyo wana Chadema waanze kuandaa matanga kwa chama chao.

Ukitazama mgawanyo wa ushindi huu utagundua kuwa, pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa kwenda na kupiga kambi kanda ya ziwa ameambulia kata sifuri(0). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kutumia gari ya serikali alijikita kusini nako katoka kapa.

Nguvu iliyotumika kutoka kwa vyama vya upinzani hasa Chadema hailingani na ushindi walioupata. Wakati CCM ikiwa busy na chaguzi za ndani ya Chama wao wamezungusha viongozi wa kitaifa nchi nzima na matokeo ndio hayo.

Tunawashukuru sana Watanzania kokote nchini walioendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuwaongoza na kutekeleza ilani yetu. Tunawaahidi utumishi uliotukuka.
Chanzo ::http://daresalaam-yetu.blogspot.com

Nape Nnauye:“Tunajivunia ushindi katika Kata 22,tumepoteza Kata Nne Naweza kusema ni sawa na asilimia 75. TLP, ilipata kata moja na CUF kilipata kata moja na Chadema ilipata kata tano...!




 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungmza na waaandishi wa Habari
--
LICHA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kunyakua viti 22 kati ya 29 vya
udiwani katika uchaguzi uliofanyika juzi, chama hicho tawala kimepoteza
kata nne kilichokuwa kinazishikilia kabla ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ulifanyika kuziba nafasi zilizoachwa wazi na madiwani walioondoka kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo vifo.

Matokeo
ya uchaguzi huo yanaonyesha kwamba katika Kata 29, Chadema wameshinda
katika kata tano na kukifanya kuongeza madiwani watatu. TLP na CUF kila
kimoja kimepata kata moja.

Kabla ya uchaguzi huo, Chadema kilikuwa na
Kata mbili za Rombo na Mvomero ambazo kimefanikiwa kuzitetea na
kuongeza nyingine tatu, ambazo ni Mlangila (Ludewa), Ipole (Tabora) na
Daraja Mbili (Arusha) ambazo awali, zilikuwa zikishikiliwa na CCM.

TLP
kilitetea kiti chake katika Kata ya Vunjo (Kilimanjaro) wakati CUF
kilitwaa Kata ya Newala ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na CCM.

CCM
kimetetea viti vyake vingine vilivyobaki ambavyo ni Msalato (Dodoma),
Bang’ata (Arumeru Magharibi), Mletele (Songea), Mwawaza (Mjini
Shinyanga), Lwezera (Geita), Bugarama (Kahama) na Bagamoyo mkoani 
Pwani.

Viti vingine ni Mnero na Miembeni (Nachingwea), Myovizi
(Mbozi), Mpapa (Momba), Mahenge (Ulanga), Vugiri (Korogwe), Tamota
(Lushoto), Makata (Liwale), Mpepai (Mbinga), Kiloleli (Sikonge), Miyenze
(Tabora), Karitu (Nzega), Lubili (Misungwi), Kilema Kusini (Moshi),
Nanjara/Neha (Rombo), Lokokona (Nanyumbu) na Kitangiri (Newala).

Katika
Kata ya Rwezera, Misango Jeremiah alishinda baada ya kupata kura 1,309
dhidi ya wapinzani wake, Ibuga Mussa (Chadema) aliyepata kura 933 na
Mussa Mtagala (CUC) aliyepata kura 317.  Uchaguzi huo ulifanyika kujaza
nafasi hiyo iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo,
Anatory Mkufu kufariki dunia kwa ajali ya gari Februari 23, mwaka huu.


Chanzo ::http://daresalaam-yetu.blogspot.com/ 

Sunday, October 28, 2012

POLISI WAKAMATA UJUMBE MFUPI WA SIMU KWA AJILI YA KUTEKELEAZA MAUAJI YA KAMANDA BARLOW...!

Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa ya awali ya uchunguzi wa mauaji ya kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa ajili ya kutekeleza mauaji hayo imenaswa.

Kamanda Barlow aliuawa usiku wa manane alipokuwa akitoka kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake. Alifikwa na mauti hayo baada ya kupigwa risasi akimsindikiza Mwalimu Doroth Moses.


Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya makachero jijini Mwanza zinaeleza kuwa, ukweli wa mauaji hayo umebainika na kwamba watuhumiwa waliokamatwa wanahusika moja kwa moja na mpango kamili wa mauaji hayo.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa kuwa Kamanda aliuawa baada ya mmoja wa wahalifu aliyekuwa akikabiliwa na kesi nzito (jina tunalihifadhi) kutoa kiasi cha fedha kupitia kwa mtu wake wa karibu ili kutekeleza mpango wa mauaji ya kulipiza kisasi.


Kupatikana kwa wauaji hao, kumetokana na simu ya Mwalimu Dorothy Moses kupitia ujumbe wa simu aliokuwa akiwasiliana na wahusika.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lilian Matola alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema taarifa siyo za kweli na kusisitiza kwamba taarifa aliyoitoa DCI Robert Manumba ndiyo sahihi.


"Haya mambo yanatoka wapi, kwanza siyo kweli hata kidogo, hawa ni watu walikuwa kwenye safari zao za uhalifu ndipo wakakutana na Kamanda Barlow," alisema.


Habari hizo zinaeleza kuwa, kubainika kwa mpango huo ni baada ya kunasa ujumbe mfupi wa maandishi uliokuwa ukionyesha matukio yote tangu walipokuwa hotelini na kwamba wakati wote wauaji walikuwa wakipewa taarifa za kila nyendo za Kamanda Barlow.


Ujumbe mmojawapo ulionaswa katika moja ya simu unasema, “Nipo kijiweni kwangu…. nitawajulisha zaidi”.


Alisema kutokana na kubainika kwa ujumbe huo wa maandishi wa simu, jeshi hilo limelazimika kufuatilia matukio kadhaa yaliyomo katika historia ya mtuhumiwa.


Kuhusu kauli ya Manumba alisema kuwa, kama DCI Manumba alitoa taarifa yake kwa lengo la kiintelejensia kwa ajili ya kusaidia upelelezi anakubaliana na hilo.”


“Unajua kuna mbinu nyingi za upelelezi, inawezekana wameeleza hayo ili kuwazubaisha watuhumiwa kisha uchunguzi wa kina ukaendelea, hapo ni sawa, lakini kama ndiyo mwelekeo wa uchunguzi wao, basi wanapaswa kujua kuwa wameacha vitu vingi sana vya msingi,” alieleza askari mwingine.

DCI Manumba katika taarifa yake, alisema kwamba Jeshi la Polisi limewatia mbaroni watu watano jijini Dar es Salaam wakiwa na bunduki aina ya shortgun inayodaiwa kutumika katika mauaji hayo. Hata hivyo walishindwa kubainisha sababu za mauaji hayo licha ya kueleza kuwa watuhumiwa waliokamatwa walikiri kuhusika.


Akielezea chanzo cha mauaji hayo kutobainika, Inspekta Generali wa Polisi, IGP, Said Mwema alisema jeshi lake pamoja na kuwakamata watu watano jijini Dar es Salaam wanaosadikiwa kuwa majambazi, bado wanafanya uchuguzi wa chanzo cha mauaji hayo ili kujua kama majambazi hao walikutana na kamanda kwa bahati mbaya katika kazi zao au la.

Alisema, mbali na kuwakamata watuhumiwa hao watano na kukiri pamoja na kuonyesha bunduki aina ya shortgun waliyotumia kwa mauaji, watuhumiwa wengine wawili bado wanasakwa pamoja na redio ya mawimbi ya kamanda huyo ambayo iliibiwa eneo la tukio yalikotokea mauaji. 


Chanzo : Mwananachi

JCB AKAMATWA KUISAIDIA POLISI KUFUATIA KIFO CHA LEXA ..!


Lexa Julius enzi za uhai wake


JCB

Juzi ijumaa ya tarehe 26 october 2012 mmoja wa member wa WATENGWA anaeitwa Lexa Julius ambapo inasemekana siku ya ijumaa
akiwa maeneo ya viv via alitoka nje ambapo alivamiwa na watu ambao wanamfahamu na kumpiga na kumuibia vitu vyake baada ya hapo alirudi ndani via via na baadae alienda nyumbani kwake kwenda kulala na ndipo kifo kilipomkuta. Hali hiyo ambayo mpaka sasa bado kuna ukungu mzito kwa ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa Lexa ambao wamebaki na masikitiko makubwa sana.

Nilifanikiwa kuongea na producer wa WATENGWA "Daudi Bakari" maarufu kama Daz "Kweli Lexa alivamiwa na watu ambao wanamfahamu na kumpiga na kumuibia vitu vyake baada ya hapo alienda nyumbani kwake kulala na ndipo kifo kilipomkuta na kutokana na tukio hilo polisi walimkamata JCB kwa mahojiano maana JCB ndio mtu aliyekua na Lexa muda mfupi kabla ya kukutwa na mkasa huo. Lakini tayari polisi wamesha mhoji JCB na kumuachia huru na kwa sasa JCB yupo mtaani anaendelea na harakati zake. Mazishi ya Lexa yatafanyika kesho jumatatu tarehe 29 October nyumbani kwao maeneo ya ilboru mjini Arusha" alisema Daudi