Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, December 27, 2012

PROMOTA ALIYEWALETA P SQUARE UGANDA ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUIBIWA PESA YOTE YA SHOW...!


 
 Muandaaji wa concert iliyopewa jina la chop my money, nakuwaleta P Square, amelazwa hospitali mara baada ya wajanja kutokomea na mkwanja wa ticket zilizouzwa kabla ya show na police wanasema inawezekana wezi hao wamekimbilia congo. 

Pesa iliyopotea ni zaidi ya milioni 450 za Uganda. Mkurugenzi wa silverback Yvonne naye amelazwa baada ya kugundua hata mkwanja wa getini umepotea. hiyo ndo chop my money.
 

KESHO NDIO ROMA MKATOLIKI ATAACHIA NGOMA YAKE MPYA IITWAYO "2030" ...!


Baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya mwaka bila kutoa ngoma mpya, hatimaye rapper Roma anatarajia kutoa ngoma yake mpya kesho Ijumaa.

Ngoma hiyo inaitwa 2030 na kama kawaida yake amezungumza masuala mengi pamoja na kutaja majina ya watu wengi maarufu kwa kuoanisha na matukio.

Hit ya mwisho aliyoitoa Roma ni Mathematics.

Tuesday, December 25, 2012

MJINI ZANZIBAR PADRE APIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA...!


Padre anayefahamika kwa jina la Ambrose Mkenda amepigwa Risasi na Watu wasiofahamika kwenye geti la nyumbani kwake wakati akifunguliwa geti aingie nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar, ambako ndiko makazi yake yalipo akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha peke yake.

Hali yake sio nzuri kwani Risasi aliyopigwa imemdhuru maeneo ya mdomoni.

Waliompiga Risasi Padre huyo inasemekana ni watu waliokuwa kwenye pikipiki, ambao walimvamia akisubiria afunguliwe geti kuingia nyumbani kwake.

Chanzo: Jamiiforum

MSIKILIZE LORD EYES FEAT BEN POL I - NO MORE DRAMA (BABA LA BABA)


HII NDIO TAARIFA ILIYOTOLEWA NA JWTZ DHIDI YA MWANAJESHI ALIYEJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA NA KUPIGA PICHA NA MH. GODBLESS LEMA...!

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kuona taarifa ya mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa JWTZ wa Kambi ya Monduli, Arusha, iliyochapishwa katikagazeti la Mwanandhi la Desemba 24, 2012 akiwa amevaa sare za JWTZ.

Baada ya kuona habari hii JWTZ linafanya uchunguzi wa kina ili kutambua kama mtu huyo ni askariwa kweli au la. Kimsingi, JWTZ linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari wake kwa sababu zifuatazo; kwanza Jina la mtu huyo halijaandikwa, pili kikosi halisi cha mtu huyo hakijaandikwa kwani eneo la Monduli lina vikosi vingi na hakuna kikosi kiitwacho Monduli. Lakini pia inatia shaka kuwa mavazi yale siyo yale yanayotumika kwa wanajeshi wa JWTZ hivi sasa, kuna tofauti kati ya jampa(jacket) na suruali kama ilivyooneshwa katika picha hiyo. Aidha, jampa la sare hiyo pia lina tofauti katika sehemu za mikono, jambo ambalo linatia shaka kamani sare halisi ya JWTZ.

Ilikuwa rahisikumtambua mtu huyo kwa kuangalia uso, lakini mtu huyo anayedaiwa kuwa ni askari alifunika paji la uso ili asitambulike. Pamoja na hali hiyo ilivyojitokeza, JWTZ linashughulika kumtambua mtu huyo kwa kutumia mbinu mbalimbali. JWTZ litakapobaini ukweli huo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kutokana na Kanuni za Majeshi ya Ulinzi kwani, Sheria nambari nne (4) ya mabadiliko ya nane (8) katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992 ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwikujihusisha katika masuala ya kisiasa.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa kuchapishwa kwa picha hiyo kwani hakuna tija wala faida kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuwatia hofu kuwa Vyombo vya Ulinzi navyo vinashabikia mambo ya siasa, wakati Katiba ya nchi imekataza jambo hilo. JWTZ linawaomba wananchi waliangalie jambo hili kwa makini, kwa usalama wa nchi yetu.

Imetolewana Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

MakaoMakuu ya Jeshi, Upanga

TAZAMA VIDEO YA PNC - "IMEBUMA"...!

Monday, December 24, 2012

XMASS NDO HIYO HILI NI ANGALIZO KWA KINA DADA WAPENDA VYA BURE !!!!

Juzi Ijumaa ndiyo siku masham sham ya Sikukuu ya Xmass yalianza huku Moshi, Magari ya kifahari ya Wachaga yalianza kuingia ndani ya mji wa MOshi asubuhi, Mpaka kufika jioni mji ulikua umejaa sana.

Katikati ya mji wa moshi na Viunga vyake idadi kubwa ya kinadada ilionekana huku wakipita katika maduka mbalimbali kufanya manunuzi ya xmass. Ilipofika jioni hapo ndipo pilika pilika za kuelekea katika sehemu za starehe zilipoanza. {BAta Time}

Ndani ya Mji wa Moshi katika Uwanja wa Ushirika kulikua na Tamasha kubwa La muziki wa Dansi linalokwenda kwa jina la TUSKER CARNIVAL ambapo Bendi za muziki wa dansi Tanzania ambazo ni Twanga Pepeta International na Diamond Musica Original walikuwa wakitumbuiza.

Watu waliserebuka huku wakipata kinywaji Aina ya Tusker na nyama choma hakika ilikua shangwe sana. Ilipofika mnamo saa tisa na nusu Usiku Presenter aliyekua akiongoza Tamasha hilo Babi D'e Conscious alihitimisha Tamasha hilo hapo ndipo kilipoibuka kizaa zaa baada ya jamaa watatu kuanza kumgombania Binti mmoja anayesemekana ni mwanafunzi wa chuo cha Muccobs na kila mmoja akimtuhumu kanywa bia zake na nyama na anataka kuondoka nae.

                          Hapa ma baunsa wakimuokoa toka katikati ya watu.


Vurugu hizo zilizimwa na Walinzi wa Clouds Media baada ya kumuokoa dada huyo katikati ya kundi la watu akiwa anavuliwa nguo.

Hii ni changamoto kwa kina dada kwa msimu huu wa sikukuu, Kumbuka sikukuu ni kwa siku Moja tu ila Gharama ya maisha yako ni zaidi ya X mass.
                               HApa akisaidiwa kutoka nje ya Uwanja.


Yetu ndo hayo, Na wewe sema yakooooooooo....!

Saturday, December 22, 2012

KONTENA LA KONDOMU ZISIZOFAA KUTOKA INDIA LAZUIWA BANDARINI DAR...!

KONTENA lililosheheni kondomu za kiume kutoka nchini India imekamatwa na kuzuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamelazimika kufanya msako mkali kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye thamani ya Sh222.1 milioni zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na kuzuiliwa bandarini hapo kwa taratibu zaidi za kisheria, “Jambo lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba zipo madukani, tukajaribu kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa huenda zimetolewa kinyemela licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au zirejeshwe nchini India kwa gharama zao wahusika.

Tulipokwenda bandarini tukabaini kwamba bado zipo katika hali ile ile, kumbe zimeingizwa nchini kwa njia ya panya, kwa kweli ni mbovu na ndiyo maana tumelazimika kuwajulisha wanahabari ili muwape taarifa wananchi wawe makini,” alisema Kinabo.

Alifafanua zaidi kwamba kondomu hizo ni mbovu kwani zimebainika kuwa na vitundu, pia zinapasuka haraka, hazina kabisa viwango vya ubora wa bidhaa unaotakiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO). Kinabo alisema kuwa TBS bado wanaendelea kufanya mawasiliano na kampuni iliyotengeneza kondomu hizo, lakini kwenye kasha lake inaonyesha kuwa inaingizwa nchini na kampuni ya Fair Deal Exim ya Dar es Salaam.

---
Chanzo: Mwananchi

ANGALIA PICHA ZA MH. LEMA NA WAFUASI WA CHADEMA WALIVYO TIKISA JIJI LA ARUSHA...!






Mbuge  wa jimbo la Arusha mjini Mh. Godbless Lema  apokelewa kwa shamra shamra za kutisha baada yakushinda kesi yake iliyo kuwa ikimkabili, wakazi wa  jiji la  Arusha na wanachama wa chama cha CHADEMA wafurahia ushindi huo uliokuwa na kipingamizi.

TAIFA STAR YAWALIZA MABINGWA WA AFRIKA 'CHIPOLOPOLO' 1-0...

Hivi ndivyo Usomekavyo Ubao wa Matokeo katika Uwanja huu wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa kipindi cha kwanza cha mchezo katika ta Taifa Stars na Mabingwa wa Afrika,Zambia wana Chipolopolo.kipindi cha kwanza kimemalizika sasa huku Taifa Stars ikiongoza kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mrisho Ngassa mnamo dakika 45 ya mchezo kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda goli 1-0.
Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijaribu kutaka kumtoka beki wa Taifa stars,Salum Aboubakar wakati wa Mchezo wa Kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Taifa stars wanaongoza kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachari,Mrisho Ngassa mnamo dakika ya 45 ya mchezo. 
Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Tanzania wakishangilia Ushindi wa timu yao. 

Chanzo: MICHUZI BLOG

JOCELYNE MARO NDIO ANYAKUA TAJI LA MISS EAST AFRICA...!


 
Jocelyne Maro Miss East Africa Tanzania akipunga mkono kwa mashabiki wake mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo.
Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo toka lilipoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye thamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi wake.

 
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na Miss Uganda Ayisha Nagudi mshindi wa pili katika shindano hilo kushoto  na Miss Burundi Ariela Kwizera ambaye alipata nafasi ya tatu katika shindano hilo.
 
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na  warembo wenzake alioingia nao kwenye tano bora ya shindano hilo.
 
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akiwa amepigwa na butwaa mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo jana usiku.
 
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipongezwa na wenzake mara baada ya kushinda katika shindano hilo.
 
Warembo hawa ndiyo walioingia katika tano bora ya shindano la Miss East Africa.
 
Warembo hawa ndiyo walioingia katika kumi bora ya shindano la Miss East Africa.
 
MC wa shindano la Miss East Afrca Guetano Kagwa akitangaza warembo walioingia katika kumi bora kwenye shindano hilo.
Mkurugenzi wa Rena Event Rena Calist akizungumza katika shindano hilo huku MC Guetano Kagwa akimuangalia.
 
Warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni.
 
Warembo wakipita na vazi la Ubunifu.
Mkurugenzi wa Rena Event Bw. Rena Calist wa pili kutoka kulia akifuatilia kwa karibu jinsi shindano lilivyokuwa likiendeshwa kulia ni mmoja wa maofisa wa Miss East Afrca John Momadi
 
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.
Mwanamuziki Mad Ice akifunika kwa wimbo wake katika shindano hilo kama anavyoonekana akishangiliwa na mashabiki wake
 
The Voice Wonder nao wakifunika mbaya.
 
Mzungu Kichaa akaleta kichaa chake jukwaani na kuwaburudisha vya kutosha watu mbalimbali waliohudhuria katika shindano hilo.

DIAMOND: HAYA HAPA MASHAIRI YA WIMBO WA NATAKA KULEWA...!

We niache niende niende niende ni ende x2

{Verse 1}

Usiniulize kwanini sababu utanizingua
ukitakajiunge na mimi kama ni pesa we kunywa ntanunua..
Mi mwanzo sikuamini nikajuaga vyakuzua
Kumbe mjinga ni mimi ninayetunza wenzangu wanachukuwa..
(Oooh! Mapenzi) Mapenzi yalinifanya ka_mtoto nilie vibaya,
mie siwezi kwa yalonikuta we niache niseme jina
(Ooooh! Mapenzi) yalinifanya ka_mtoto nilie vibaya
na nnamengi yamenikaa moyoni

{Chorous}
Leo nataka kulewa {Lewaaaaa}
Mi nataka kulewa {Lewaaaaa}
Nataka kulewa {Lewaaaaa}
Zikipanda nimwage radhi....x2
We niache niende niende niende ni ende...x2

(Vearse II)

Mi kwa mapenzi maskini Nikamvisha na pete nikamuoa
kukata vilimilimi vya wazushi wanafki wanaomponda...
kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua
si tuko kama ishirini mabuzi ving`asti wengine anawaonga..
(Oooh! Mapenzi) yalinifanya ka_mtoto nilie vibaya,
mie siwezi, kwa yalonikuta we niache niseme jina
(Ooooh!) Mapenzi yalinifanya ka_mtoto nilie vibaya
na nnamengi yamenikaa moyoni

{Chorous}
Leo nataka kulewa {Lewaaaaa}
Mi nataka kulewa {Lewaaaaa}
Nataka kulewa {Lewaaaaa}
Zikipanda nimwage radhi....x2
We niache niende niende niende niende..x2

Friday, December 21, 2012

MH. GODBLESS LEMA NDIO MBUNGE HALALI ARUSHA MJINI...!


Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa Tiketi ya CHADEMA (aliekuwa amesimamishwa Ubunge),Mh. Godbress Lema akiwasalimia wanachamana na wafuasi wa Chama hicho waliokuwepo ndani ya Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es Salaam leo.wakati alipofika kusikiliza Rufaa yake dhidi ya kesi ya Kupinga matokeo ya Uchaguzi dhidi yake iliyofunguliwa na Wanachana wa CCM jijini Arusha.Mh. Lema ameshinda Rufaa hiyo na kufanikiwa kurudishiwa nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo la Arusha mjini.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe (katikati) akiwa sambamba na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Godbress Lema (pili kulia) na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari wakiwa ndani ya Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusikiliza Rufaani ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyokuwa ikimkabili Mbunge,Godbress leo ambaye ashinda Rufaa hiyo leo.

Wanachama na Wafuasi wa Chadema wakimshangilia Mbunge wao mara baada ya kushira Rufani ya kesi yake ya kupinga matokeo ya Uchaguzi jimbo la Arusha mjili iliyokuwa ikisikilizwa leo kwenye Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es salaam.

Lema na Mnyika pamoja na wanachamwakiwa katika maandamano.

Wanachadema wakitembea kwa maandamano kuelekea kwenye ofisi za Chama chao zilizopo Kinondoni jijini Dar.

Mwanamama huyu ambaye ni Mama ntilie na hakutaka kuwa nyuma kishangilia ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha,Mh. Godbress Lema. 


Pongezi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama,Mh. Wilbrod Slaa.

Katibu Mkuu wa CHADEMA,Mh. Wilbrod Slaa akizungumza na vyombo vya Habari baada ya Ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mh. Godbress Lema.