Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, May 31, 2013

BOFYA HAPA KUANGALIA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA SITA


KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA BOFYA HAPA 

BONYEZA HAPA KUPATA MATOKEO: MATOKEO KIDATO CHA SITA

Machafuko bungeni

Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa  jana ilisababisha mtafaruku mkubwa bungeni na siku nzima Bunge likakwama kufanya shughuli zake. Awali  Naibu Spika, Job Ndugai, aliahirisha Bunge asubuhi hadi jioni, lakini hata liliporejea jioni, aliliahirisha tena ili kutuliza hali ya hewa. Vile vile, Msemaji wa Kambi hiyo, Ezekiah Wenje alinusuruka kupigwa ka wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), baada ya kuokolewa na askari wa Bunge na kupelekwa kusikojulikana kutokana na hotuba aliyokuwa ameitoa bungeni.. 
Vurugu zilianza wakati Wenje alipokuwa akisoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusu Wizara hiyo na kukihusisha Chama cha Wananchi (CUF), na vyama vinavyoshabikia vitendo vya ushoga na usagaji duniani.


Wenje alikuwa anawasilisha hotuba ya kambi ya upinzani baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kusoma hotuba yake ya bajeti kwa mwaka 2013/14.
 Hali ya hewa bungeni ilibadilika alipofika ukurasa wa saba wa hotuba yake aliposema itikadi za CUF ni za mrengo wa kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake ni pamoja na kupigania haki za ndoa za jinsia moja, usagaji na ushoga na kwamba hilo ndilo tangazo la chama hicho kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali duniani.
Mbunge wa Mtambile (CUF),  Masoud Abdalah Salum, alisimama na kuomba mwongozo kuhusu kauli hiyo ya Wenje kukihusisha chama chao na ushoga na usagaji, lakini hata kabla ya Spika hajatoa mwongozo wabunge wote wa CUF walisimama huku wakimporomoshea matusi Wenje.
Naibu Spika alisimama na kuwaomba wabunge hao wa CUF wampe nafasi Wenje afafanue kauli yake na aliposimama alikataa kufuta kauli yake akijitetea kwamba wanaomshutumu hawajaelewa alichokuwa akikisema.
“Mheshiniwa hapa tunazungumzia uhusiano wa vyama vya hapa nchini na vile vya nje kuhusu itikadi wanazofuata, CCM wanafuata mlengo wa kushoto, Chadema sisi tuko kati na CUF wanafuata mlengo wa waliberali, tunachosema hapa ni mrengo wa itikadi,” alisema Wenje na kusababisha wabunge kulipuka kwa kelele wakisema hotuba hiyo haitasomwa huku wakiwa wamesimama.
Utetezi huo wa Wenje ulionekana kama umeongeza mafuta kwenye moto huku wabunge wote wa CUF wakisimama na kutoa matusi mazito kwa Wenje wakiungwa mkono na baadhi ya wabunge wa CCM, ambao walisikika kwenye vipaza sauti wakisema apigwe apigweeee hana adabu.
Kauli ya Wenje ilizua zogo kubwa kiasi cha kutoweka kwa usikivu hali iliyomlazimu Naibu Spika kusimama na kuahirisha shughuli za Bunge hadi jioni huku akiiagiza Kamati ya Maadili ya Bunge ikutane kujadili hali hiyo.
Baada ya kuahirishwa kwa shughuli za Bunge, wabunge wa CUF walionekana wakitoka nje kwa kasi huku wengine wakichana chana hotuba hiyo ya kambi ya upinzani wakiwahi nje kwa ajili ya kumzonga Wenje.
Walipofika nje hawakufanikiwa kumwona Wenje ambaye aliondolewa maeneo hayo na askari wa Bunge kwa sababu za kiusalama na ndipo hasira zao zikamwangukia Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vincent Nyerere, waliyemkuta nje ya ukumbi ingawa wakati wa mzozo wote hakuwapo bungeni.
Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bundala ‘Bwege’, aliwaongoza wenzake kumporomoshea matusi Nyerere ambaye alionekana kuduwaa kwani hakuwa anajua yaliyotokea bungeni.
“Sisi tutawapiga kweli chezeeni CCM, sisi msituchezee tutawatandika msidhani CUF ni CCM mnaowachezea kila siku, acheni mambo ya kijinga tutawakomesha muache kutuchezea,” alisikika Bungala huku wabunge wengine wa chama hicho wakiwa wamemzingira Vincent.
Mbunge huyo wa CUF alipokaribia kumtwanga ngumi Vincent Nyerere, Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde, alifanya kazi kubwa kumlinda Nyerere kujinasua katikati ya kundi la wabunge wa CUF walioonekana wakizungumza kwa jazba huku wakimnyooshea kidole.
Wabunge wengi walionekana nje ya ukumbi wa Bunge wakiwa katika makundi makundi wakijadili mtafaruku huo uliosababishwa na hotuba ya kambi ya upinzani.
Mbunge wa Mjimkongwe (CUF), Ibrahim Sanya, alionekana akifoka kwa sauti ya juu akidai kuwa wabunge wa Chadema tangu Bunge lianze wamekuwa wakitoa hotuba za kuwadhalilisha wabunge wa chama chake.
“Leo (jana) jioni wakirudia ujinga huu tunapiga mtu humo humo ndani ya ukumbi wa Bunge, hatuwezi kukubali dhihaka ya namna hii, Bunge liongeze askari wa kutosha maana hapatakalika mle ndani tukidhalilishwa tena,” alisikika Sanya akifoka.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CUF), Ali Keisy, alisikika akiwafokea wabunge hao wa CUF kwamba wameshindwa kumshughulikia Wenje ndani ya Bunge, hivyo hawana sababu ya kupiga kelele wakiwa nje ya ukumbi.
Alisema matusi yaliyotolewa dhidi ya CUF yangekuwa yameelekezwa upande wa CCM machafuko makubwa yangetokea ndani ya ukumbi huo kwa kuwa wasingekubali Wenje atoke bila kufuta kauli yake.
“Mmeshindwa kumshughulikia bungeni mnakuja nje kupiga kelele tu, mngemtandika akalazwa Muhimbili au Aga Khan ningewaelewa, lakini mmeishia kuangalia tu, angeitukana CCM ningemla nyama mimi, kwa kweli wabunge wa CUF mmenidhalilisha sana kwa uzembe mliouonyesha,” alisema Mbunge huyo wa CCM na kuongeza:
“Naomba msiendelee kutupigia kelele hapa nje, kama mmeshindwa kummaliza mle mle bungeni msitupigie kelele….mnasema mtamshughulikoa jioni huo ni uongo, ni sawa na kumfumania mtu halafu unamlea badala ya kummaliza hapo hapo, ingekuwa chama changu kimetukanwa asingetoka akiwa anacheka,” alisema Keisy kwa sauti kubwa akiwaeleza wabunge wa CUF waliokusanyika nje ya ukumbi wa Bunge.
Akizungumzia tukio hilo, Nyerere alisema amesikitishwa na tukio hilo kwani hakuwa sehemu ya mzozo huo.
Alisema alivamiwa na wabunge wa CUF ambao walianza kumporomoshea matusi na kejeli za kina aina wakiongozwa na ‘Bwege’.
“Mimi nimemheshimu Bungala kwa utu uzima wake, sikuwa najua lolote, nimeshangaa kuona navamiwa na kundi la wabunge kila mmoja akitoa tusi lake dhidi yangu na Chadema, wamenifedhehesha sana,” alisema.
Katika hali ya kushangaza, Naibu Spika, Job Ndugai, aliwalaumu waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge kwamba ndio wanasabasisha vurugu bungeni.
Ndugai alisema waandishi wa habari wamekuwa wakipendelea vyama vya upinzani na kuwakandamiza wale wa CCM.
“Haya ni matokeo ya kazi zenu waandishi wa habari, mnawabeba sana wapinzani, fanyeni kazi zenu kwa usawa maana wapinzani hata wangefanya uovu gani nyinyi huwa hamuoni ila wakifanya wabunge wa CCM mnayakuza,” alisema Ndugai.
WENJE AGOMA KUOMBA RADHI
Wakati huo huo kikao cha Bunge kilichokuwa kiendelee jana joni kilivunjika tena baada yaa kutokea kutoelewana baina ya wabunge wa CUF na Wenje.
Kikao hicho kilipoanza jioni Ndugai, alimwita, Mbunge wa Manyoni Mashariki (CCM), John Chiligati, ambaye aliongoza kikao cha Kamati  ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kusuluhisha mzozo huo atoe taarifa.
Chiligati aliposimama alilitaarifu Bunge kuwa kwenye kikao cha kamati hiyo, waliwashirikisha Mbunge wa Mtambile  Salim na Wenje kwa ajili ya mashauriano na kuwa  walikubaliana Wenje afute maneno yake na aombe radhi.
Alisema katika kikao hicho, Wenje alikubali ushauri wao wa kufuta maneno yake na kuomba radhi bungeni na akwamba hakuwa na nia mbaya.
“Lakini mheshimiwa Spika katika hali ya kushangaza Wenje hajafuta maneno yake isipokuwa ameyaweka kwa lugha ya Kingereza tu, hivyo kamati imekushauri mheshimiwa Naibu Spika umwamuru ayafute,” alisema Chiligati.
Ndugaia, alisimama na kumpa Wenje dakika tano kujieleza kuhusu tuhuma zilizokuwa zimeelekezwa kwake.
Katika maelezo yake, Wenje alisema hataomba radhi kwa kuwa yote aliyosema ni ya kweli na CUF ilisaini makubaliano ya kuwa mwanachama wa vyama vyenye mrengo wa kiliberari.
“Mkutano uliofanyika Oxford 1997 CUF wakiwa wanachama ulitoka na maazimio kwamba ushoga na usagaji ni mambo yanayokubalika kwamba ni halali kwa  vyama vya mfumo wa mrengo huo, sasa mnataka nifute maneno ambayo ni kweli? niombe radhi kwa kosa lipi, mimi siwezi kuomba radhi kwa kosa ambalo halipo,” alisema.
Salim ambaye aliomba mwongozo asubuhi, alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema lazima Wenje afute maneno yake na kuomba radhi la sivyo hotuba ya kambi rasmi ya upinzani haitasomwa bungeni.
Katika hatua ya mwisho, Ndugai alimwomba Wenje kuendelea na hotuba yake kwa kuanza kuomba radhi na ayaondoe maneno katika kifungu cha tatu na badala yake asome kuanzia cha nne.
Wenje aliposimama alianza kusoma hotuba yake kuanzia ukurasa wa nne na kuyaacha maneno yaliyokuwa yamewaudhi CUF asubuhi, lakini wabunge wa chama hicho hawakuridhika na kusimama huku wakizomea.
Wabunge wote wa CUF walisimama na kumtaka Wenje aombe radhi hali iliyomlazimu Ndugai kusimama na kusitisha shughuli za Bunge.
“Waheshimiwa kwa hali ilivyo siwezi kuendesha shughuli za Bunge kwa hiyo nasitisha shughuli za Bunge hadi kesho saa tatu asubuhi,” alisema Ndugai.

CHANZO: NIPASHE

JINSI YA KUTUMA MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA..!

YAH: MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA

Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya Maziko.

Mpaka sasa ushirikiano tulioupata ni kampuni ya Clouds Media Group ambayo imebeba jukumu la kusafirisha mwili wa marehemu kutoka South Africa mpaka Tanzani, Bongo Records wameshachangia shilling milion 5 na Push Mobile wametoa million 5. Kamati inaomba wizara husika, mashirika, makampuni pamoja na watu binafsi kutoa michango yao katika kukamilisha jukumu la kumhifadhi katika nyumb yake ya milele ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha.

Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:

Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738

Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB

Tukitegemea ushirikiano wenu tunatanganguli shukrani za dhati

Thursday, May 30, 2013

BOFYA HAPA KUANGALIA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE

KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE BOFYA HAPA  http://196.44.162.25/csee2012/Olevel.htm

*************************

Full Interview P-Funk Akizungumzia Kifo Cha Marehemu Albert Mangwair

OPEN LETTER FROM MANGWAIR - MSWAKI FT. UNICE

Huu Wimbo Ameimba Producer wa mziki anayejulikana kwa jina la Mswaki Kutoka Studio ya Black Curtains....Ameimba kama Marehemu Ngwear Akiimba baada ya Kifo chake...Sikiliza Hapa chini: Big up Sana Mswaki

AMPLIFAYA LIVE KUTOKA AFRIKA KUSINI STORY NAMBA 4, 3, 2 & 1 NA MILLARD AYO..!

TAARIFA KUTOKA AFRICA KUSINI MUDA HUU KUHUSU MWILI WA ALBER MANGWEA

#CloudsFM #SA Taarifa tulizopewa jana mchana ktk mochwari ya Hillbrow hapa Johannesburg, mwili wa Ngwea utafanyiwa uchunguzi leo hivyo majibu yatatoka leo au kesho... shea post hii na wengine waone mtu wangu kuepuka habari nyingine zinazovuruga watu.

BREAKING NEWS:BUNGE LASITISHWA KISA HOTUBA YA MH;WENJE.

Katika hali isiyo ya kawaida leo hii mapema Bungeni Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani imesitishwa baada ya hotuba hiyo kuwataja chama cha CUF kwamba
wanamahusiano na chama kinachosapoti Usagaji pamoja na Ushoga hivo nao kuwahusisha katika mambo hayo.
Mbunge wa CUF alisimama na kuomba muongozo juu ya jambo hilo kutokana na kanuni ya 68 ya sheria na miongozo ya Bunge.Suala hilo lilizua kizaazaa na kusbabishwa bunge kuahirishwa.

Vurugu za Mtwara, 12 wadaiwa kufa..!

VURUGU zilizofanyika hivi karibuni mkoani Mtwara zimechukua sura mpya, baada ya mambo mazito yenye sura ya kinyama ndani yake kuibuliwa. Utafiti uliofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), umebaini watu zaidi ya 12 wamepoteza maisha katika vurugu hizo tofauti na takwimu za watu watatu wanaotajwa na Serikali.  Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kwa kushirikiana na Mtandao wa Haki za Binadamu Kusini Mwa Afrika (SAHRINGON).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Harold Sungusia alisema utafiti huo wa muda mfupi umebaini kasoro katika takwimu za Serikali kuhusiana na vifo vya watu.

Sungusia alisema utafiti uliofanywa na shirika lake umebaini kuwapo kwa vitendo vya ubakaji wa wanafunzi wa vyuo, huku wazee wa kimila wakidaiwa kuchinja mbuzi za tambiko kupinga ujenzi wa bomba kwa ajili ya kusafirisha gesi.



Vifo

Sungusia alidai kuwa wamebaini vifo vilitokea katika vurugu hizo ni zaidi ya 12 na kwamba shirika lake linaendelea kuhakiki majina ya watu waliofariki dunia na taarifa zao nyingine.

Sungusia alitoa shutuma nzito kwa askari polisi kwamba ndio waliohusika na ongezeko la vifo hivyo.

“Hivi vifo ni kutokana na askari polisi kuvamia nyumba za wananchi, kuvamia maduka na kuingia ndani na kupiga mabomu ya machozi, huku wakiiba mali za raia zikiwamo televisheni, redio na fedha,” alisema.

Alisema timu ya watafiti hao inaendelea kuzungumza na wazazi na familia zilizopoteza ndugu zao ili kuwa na uhakika wa majina yao, umri na maeneo walipozikwa.

Sungusia alisema katika hali isiyo ya kawaida, taasisi za Serikali zikiwamo hospitali na polisi zimeshindwa kutoa ushirikiano wa karibu pale walipotakiwa kutoa taarifa halisi kuhusu madhara ya vurugu hizo.

“Tumezungumza na baadhi ya wakazi wa Mtwara juu ya mambo mbalimbali kuhusu gesi na athari zilizotokea katika vurugu za hivi karibuni.

“Walieleza ndugu zao waliokufa na baadhi tumepata majina yao, tutayaweka baada ya kukamilisha taarifa zote,” alisema.
Matambiko ya kimila 
Alisema kuwa katika vurugu hizo zilizotokea, wamebaini kuwa tayari baadhi ya wazee maarufu wa kimila wamekwishafanya matambiko yao na kuwapa vijana imani ya kuapishwa juu ya kutetea na kulinda rasilimali za Mtwara zisitoke bila wao kuridhia.

“Tumezungumza na wazee wa kimila na wakakiri kwamba walikwishafanya matambiko yao na kutoa mbuzi wawili kama kafara, mbuzi mmoja alichinjwa wakanywa damu na wa pili alipelekwa eneo lenye gesi na kufanya matambiko yao.

“Katika matambiko yao walikubaliana kama mbuzi huyo akipiga magoti, basi gesi hiyo haitatoka Mtwara na kama angesimama ingeashiria inatoka. Wanasema mbuzi wao alipiga magoti.

“Pia tumeelezwa kwamba, vurugu hizo zilichochewa na taarifa zilizotolewa na wavuvi wanaovua kina kirefu cha bahari kwamba, kuna meli imetia nanga baharini na inavuna gesi na inaipeleka ng’ambo kupitia Nyambizi yaani Sub-marine.

“Kutokana na hali hiyo, wananchi wa Mtwara walianza kuhamasishana mjini hadi vijijini na kuwa na msimamo wao wa lugha ya kimakonde kama ‘AIYUKI’ yaani haitoki,” alisema.



Ubakaji 

Sungusia alisema wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Chuo cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Chuo cha Mtakatifu Augostine ni miongoni mwa watu walioathiriwa.

Alisema wanafunzi hao walivamiwa na polisi wakiwa njiani wakienda mjini kujifunza kwa vitendo ‘field’ na kufanyiwa vitendo hivyo vibaya.

Alisema licha ya wananchi wa Mtwara kushukuru askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kurejesha amani, lakini wameendelea kuwa na hofu kubwa.



CUF kukutana na Wanamtwara

Wakati huo huo Chama cha Wananchi (CUF), kimeandaa kongamano kubwa kwa ajili ya wananchi wanaotoka Mtwara na Lindi waishio jijini Dar es Salaam, ili kujadili kwa uwazi tukio la Mtwara.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa Habari Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema kongamano hilo litafanyika Juni 2, mwaka huu.

Alisema CUF imeamua kufanya kongamano hilo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamikia hatua ya Serikali kutosikiliza kilio chao.

“Baada ya majadiliano ya kina mawazo ya wananchi yatakusanywa kisha kupelekwa kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na Spika wa Bunge, Anne Makinda ili waweze kuyachambua nao kwa nafasi zao na kuyachukulia maamuzi,” alisema Mtatiro.

Alisema kuwa chama chake kinafanya hivyo kutokana na vyama vya siasa kuzuiwa kufanya mikutano katika mikoa ya kusini katika kipindi hiki.

“Sisi vyama vya siasa hatuna mtutu wa bunduki, ila tunatoa elimu kwa wananchi ni wapi tumeyumba kiuchumi na nini kifanyike katika kuiondoa CCM madarakani,” alisema.



Chanzo - Mtanzania

‘Tuandamane kupinga muswada wa mabadiliko ya uchaguzi 2015’ ..!

Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema amewataka wakazi wa Arusha, kujiandaa kwa maandamano hadi bungeni Dodoma, kupinga kuwasilishwa muswada wa mabadiliko ya kufanyika Uchaguzi Mkuu, badala ya 2015 ufanyike 2017. Akizungumza katika mkutano wa kampeni jana katika Kata ya Kaloleni, Lema alisema kuna taarifa kuwa kuna mpango wa kupelekwa bungeni muswada wa mabadiliko ya uchaguzi ujao, jambo ambalo linapaswa kupingwa kwa nguvu zote. 
“Tunajua wabunge wa CCM wataukubali muswada kwani wanajua ukifanyika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 wengi hawatashinda, lakini wajue nguvu ya umma itashinda,” alisema Lema.
Lema ambaye kesi yake ya kufanya vurugu Chuo cha Uhasibu Ausha, imepangwa kuanza kusikilizwa Julai 2 baada ya upelelezi kukamilika, alisema kuna hoja kuwa Uchaguzi Mkuu lazima ufanyike baada ya kukamilika kwa mchakato wa Katiba Mpya au kuwapo na fedha za kutosha jambo ambalo Chadema hawatalikubali.
“Tunajua mwaka 2015 Chadema tunachukua nchi hivyo, hatutaki kuwaongezea muda CCM na tukichukua nchi tu kama nikichaguliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika kipindi cha miezi sita kitaeleweka,” alisema Lema.
Alisema ndani ya miezi sita Serikali ya Chadema,itahakikisha fedha zote zilizofichwa Uswisi na nchi nyingine zinarudi na watuhumiwa kufikishwa mahakamani.
Akizungumzia uchaguzi mdogo wa Kata ya Kaloleni,Themi, Kimandolu na Elerai,Lema alisema chama hicho kina uhakika wa ushindi kwani wagombea wake wanakubalika na wana uwezo.
Hata hivyo, aliwataka wakazi wa Kaloleni na kata nyingine, kujitokeza kwa wingi kupiga kura June 16, ili mchana tayari wawe wanashangilia ushindi.
Lema alisema wanataarifa za kugawanywa fedha mitaani, akawataka wafuasi wa Chadema kuzichukua fedha hizo kwani ni kodi zao, lakini kura wapige kwa Chadema.
Awali mgombea wa udiwani wa Chadema wa kata hiyo, Emanuel Kessy alitoa ahadi kuwa akichaguliwa,atahakikisha wazee wote wanatibiwa bure, hakuna watoto wa shule watakaorudishwa nyumbani kwa kukosa ada pia ataimarisha usafi wa kati hiyo.
Mgombea wa udiwani wa Kata hiyo kupitia CUF, Abbas Mkindi maarufu kama Darwesh akizungumza katika kampeni juzi hiyo , aliwataka wakazi wa kata hiyo, kutofanya makosa kuchagua watu wasio na uchungu na kata hiyo.
“Mimi mnanifahamu hapa, nimezaliwa hapa, tumekuwa wote hapa,na hivyo najua shida zetu naomba mnichaguwe,” alisema Mkindi.

Chanzo - Mwananchi

Mishahara Kima cha chini sekta binafsi juu..!

Serikali imetangaza nyongeza mpya ya mishahara ya kima cha chini kwa sekta binafsi nchini, ambayo itaanza kutumika Julai mwaka huu. Vile vile, serikali imetangaza kutengeneza ajira mpya 600, 000 kwa vijana nchini kupitia programu ya ajira kwa vijana katika mwaka ujao wa fedha. Hayo yalitangazwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudence Kabaka, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Waziri Kabaka alisema nyongeza hiyo mpya pia itakuwa katika sekta binafsi nne mpya zilizoainishwa hivi karibuni ambazo ni Ujenzi, Shule Binafsi, Nishati na Mawasiliano. 

Alisema wizara imekamilisha utafiti wa majadiliano ya kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi 12 na kwamba katika sekta zote 12 kima cha chini kimeongezeka.
Alitaja sekta hizo kuwa ni  Ujenzi, Shule Binafsi, Nishati, Viwanda na Biashara, Hoteli na Huduma Majumbani.
Nyingine ni, Ulinzi Binafsi, Afya, Madini, Uvuvi na Huduma za Majini, Usafirishaji na Mawasiliano na Kilimo.
Waziri Kabaka alisema kima cha chini katika sekta zote 12 kimeongezeka kwa kiwango tofauti tofauti, huku Viwanda na Biashara kikiongezeka kwa asilimia 43.8, Hoteli na Huduma za Majumbani (asilimia 55.2), Ulinzi Binafsi (asilimia 46.4), Madini (asilimia 25), Afya (asilimia 65), Uvuni na Huduma za Majini (asilimia 21.2), Usafirishaji (asilimia 49) na Kilimo (asilimia 42.9).
 Kuhusu ajira 600, 000, Waziri huyo alisema utekelezaji wa programu hiyo utafanyika katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013/2014-2015/16.
Aidha, alisema serikali katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 inatarajia kuwezesha kupatikana kwa fursa za ajira zaidi ya 300,000 na kwamba ajira hizo ni mbali ya ajira 61, 915 za watumishi wa umma watakao ajiriwa na serikali.
Alisema serikali imewabaini waajiiri ambao hawalipi wafanyakazi wao mishahara ya kima cha chini cha serikali, kutowapa mikataba ya kazi na kuwafanyisha kazi kwa saa nyingi bila malipo ya ziada.
Alisema baadhi ya waajiri hawatoi likizo ya uzazi, lakini serikali imeshawachukulia hatua za kisheria ikiwamo wizara kutoa amri elekezi kwa waajiri 118 na kuwafikisha mahakamani waajiri 33.
Alisema wizara imehakiki mikataba ya ajira ipatayo 56,000, kati ya hiyo mikataba 19,247 ni madereva wa malori yanayosafirisha bidhaa nje ya nchi.
Waziri Kabaka alisema mpango huo utaanza kutekelezwa baada ya kukamilika kwa taratibu na maandalizi ya utekelezaji wake kwa lengo la kuufanya kuwa bora na endelevu.
Alisema wizara yake kwa kushirikiana na taasisi za hifadhi ya jamii nchini zimefanya utafiti na tathmini ya tatizo la malipo ya fao la kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi watakaopoteza ajira kabla ya umri wa kustaafu.
Alisema mapendekezo ya namna ya kushughulikia suala hilo yameandaliwa na yatajadiliwa na wadau kabla ya kuwasilishwa bungeni katika mwaka ujao wa fedha.
AJIRA MPYA ZA SERIKALI, SEKTA BINAFSI
Waziri Kabaka alisema katika mwaka 2012/13 jumla ya ajira 274,030 zilipatikana na kati ya hizo, ajira 56,746 zilitolewa na serikali, ajira 8,603 zilitangazwa na sekta binafsi kupitia vyombo vya habari na ajira 208,681 zilitokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
VIBALI VYA AJIRA KWA WAGENI.
Kabaka alisema katika kipindi hiki wizara ilipokea na kushughulikia jumla ya maombi 6,424 ya vibali vya ajira za wageni vya daraja B na imefanya ukaguzi katika kampuni 148 kwa lengo la kuhakiki vibali vya ajira.
Alisema rasimu ya muswada wa vibali vya ajira kwa wageni utawasilishwa bungeni katika mwaka ujao wa fedha na kwamba lengo lake ni kuwa na sheria moja ya kusimamia masuala ya vibali vya ajira za wageni, hivyo kuondoa utata na migogoro katika utaratibu unaotumika sasa.

CHANZO: NIPASHE

Wednesday, May 29, 2013

HAYA NDIO MAADHIMISHO YA SIKU YA KULINDA AMANI DUNIANI..

DW (Kiswahili) Leo ni siku ya Umoja wa mataifa ya kulinda amani
duniani. Miongoni mwa nchi ambako umoja huo
unasimamia zoezi hilo barani Afrika ni Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo ikiwa na jumla ya wanajeshi
17,000. Ni miaka 10 tangu Umoja huo ulipotuma
wanajeshi nchini Kongo, ambapo wanajeshi 149 wa umoja huo wameuawa . Ngome kuu ya ujumbe
wake wa amani ni katika jimbo la Kivu Kaskazini
mashariki mwa nchi hiyo

P Funk Majani amekataa nyimbo za marehem Albet Magwea alizo rekod Bongo Record kupigwa Clouds Fm


Source : Djchokablog

UPDATE KUHUSU MSIBA WA ALBERT MANGWAIR ..!

Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach. Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.

Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu. Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.



Source: EA Radio

SIKILIZA MAELEZO YA ALIYEKUWA MWENYEJI WA NGWAIR AFRICA YA KUSINI AKISIMULIA MKASA MZIMA

MAMA NGWAIR: MWANANGU ALINIAHIDI KURUDI IJUMAA ILIYOPITA..!

Marehemu Albert Mangwair enzi za uhai wake.

Akiongea kupitia kipindi cha Amplifire cha Clouds FM, kutoka mkoani Morogoro, mama mzazi wa msanii Albert Mangwair aliyefariki dunia leo akiwa nchini Afrika Kusini, amesema kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na marehemu ilikuwa wiki mbili zilizopita ambapo Mangwair alimwambia kuwa mzima na anaendelea vizuri na kwamba angerejea nchini Ijumaa iliyopita. Aliongeza kuwa taarifa za kifo cha mwanaye amezipata jioni hii kwa masikitiko. Wakati Mangwair anaelekea Afrika Kusini hakumuaga mama yake japo akiwa huko alikuwa anawasiliana naye. Kuhusu taarifa za mazishi mama Mangwair amesema bado anasubiri shemeji zake wafike ili wapange. Mungu ampumzishe Mangwair mahali pema peponi. Amen!

Source: http://g5click.com

UPDATES ZA KIFO CHA ALBERT MANGWAIR

 PICHA ZA HOSPITALI AMBAYO MWILI WA NGWAIR UMEHIFADHIWA KWA SASA NA HOSPITAL ALIYOLAZWA M2THE P

ANAYEONEKANA KWENYE KIVULI CHEUPE NDIYE ALIYEPELEKA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWAIR HOSPITALI.…


 Chanzo chetu cha habari kinatupasha kua marehemu Albert Mangwea alikua na msanii mwenzake wa bongo flavor ajulikanae kama M2-THE-P miongoni mwa wasanii waliokuwa marafiki wa kundi la CHAMBER SQUAD, habari zinasema kua M2-THE-P nae hali yake sio nzuri na yuko mahututi katika chumba maalumu (I.C.U) ambapo madaktari wamethibitisha kua matumaini ni hafifu ya uhai wa M2-THEP pia.."hali yake sio nzuri, tumemuwekea mashine ya kupumua na yuko kwa uangalizi wa kina kwa muda wa masaa sita nbaada ya hapo tutaweza kusema nini hatima yake kwa sasa ni hayo tu" - Daktari amenukuliwa..…

KIFO CHA ALBERT MANGWAIR - SOMA TWEET YAKE YA MWISHO..!

 EVERY SECOND OF EVERY MINUTE OF EVERY HOUR OF DAY I NEED GOD

HII NDIO SABABU INAYODAIWA KUSABABISHA KIFO CHA NGWAIR. SIKILIZA APA KUPITIA E-NEWZ YA EATV

Tuesday, May 28, 2013

BREAKING NEWZZZ..! MSANII WA MUZIKI WA BONGO ALBERT MANGWEA AFARIKI DUNIA....!


HABARI ambazo hazijadhibitishwa zimetufikia  hivi punde ni  kwamba  msanii wa muziki wa bongo flavor  Albert Mangwea  amefariki dunia  akiwa  Afrika  kusini, na inasemakana Albert Mangwea alikua amelazwa katika hospital ya St. Hellen.
 
Endelea kutembelea hapa hapa kwa habari kamili kuhusiana na ukweli wa habari hii

MTANZANIA FEZA AZIDI KUNGA'ARA BIG BROTHER AFRICA....AUKWAA UKUU WA KAYA ..!

Tunaenda vizuri, bahati inaonekana kutuangukia watanzania kwani mshiriki Feza jana ameukwaa ukuu wa kaya ama kwa lugha ya ki-big brother ‘Head of House’.

Ilikuwaje?

Baba mwenye nyumba, biggie, alitoa task ambayo washiriki walitakiwa kuelekea bustanini na kuchagua box, ambaye angechukua box la ushindi ndo huyo angekuwa mkuu wa kaya. Kama zali, bahati hiyo ilimuangika mrembo Feza. Washiriki wenzie akiwemo mtanzania Nando, walimkumbatia kwa furaha kama ishara ya kumpongeza.

Iko hivi, ukichaguliwa kuwa mkuu wa kaya, unauwezo wa kumuokoa mtu ambaye anakuwa amependekezwa atoke katika wiki hiyo. Usipofanya hivyo basi wewe mwenyewe unawekwa kikaangoni.

Feza alitumia nafasi hiyo kumuokoa Elikem ambaye ni mshiriki kutoka Ghana na kumuweka kikaangoni Betty kutoka Ethiopia. Hiyo ni siri ambayo Feza inabidi aitunze hadi siku ya Jumapili wakati wa Eviction.

Hii issue ya kumuokoa Elikem wa Ghana, je ni dalili ya shemeji shemeji mbona wazima taa? Endelea kufuatilia..
BBA PAGE

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AENDESHA ZOEZI LA UVALISHAJI NISHANI KANDA YA KASKAZINI LEO ..!

Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja akikagua Guard ya Heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake kabla ya kuanza zoezi la Uvalisha Nishani kwa Maafisa na Askari wa Magereza toka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini leo Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.

 Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kulia) akimvalisha Nishani ya Utumishi Uliotukuka Kazini, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamis Nkubasi. Jumla ya Maafisa na Askari 30 kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini wamevalishwa Nishani mbalimbali leo, Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
 Guard Maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja (hayupo pichani) ikitoa heshima kabla ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini lililofanyika leo Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa Nishani mara baada ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini leo Mei 28, 2013 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro. 
Picha na Felix Mwagara.

Monday, May 27, 2013

Lema: Polisi wanatumiwa na Mulongo..!

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amelishutumu Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwamba limekwa kipeperushi cha Mkuu wa Mkoa wa huo, Magesa Mulongo, kutokana na kutumika katika kumsafisha katika sakata la kutumiwa ujumbe wa vitisho katika simu yake ya mkononi. Lema ametoa kauli hiyo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kufafanua taarifa ya jeshi hilo kwamba ujumbe mfupi wa vitisho aliotumiwa haukutumwa kutoka katika simu ya Mulongo.

“Nimesikitishwa sana na taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Mei 5, mwaka huu kuhusu ujumbe niliotumiwa sasa inathibitisha bila mashaka kuwa Jeshi la Polisi Arusha, hasa Mkuu wake anatumika,” alisema Lema.
Alisema kuwa ujumbe huo alioupokea ulikuwa unasomeka “Umeruka  kihunzi cha kwanza nitakuonyesha  kuwa mimi ni Serikali , ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi”.
Lema alisema amekuwa akijiuliza maswali mengi yanayokosa majibu, kuhusu taarifa ya Jeshi la Polisi na mtandao wa simu  kampuni moja (jina tunalihifadhi), amabyo ni pamoja na kwa nini jeshi hilo lilikataa kuchukua maelezo yake, juu ya tuhuma hizo nzito dhidi ya Mkuu wa Mkoa ambaye amemtumia meseji kupitia simu yake ya mkononi kama alivyolalamika.
Alisema ni takribani mwezi mmoja umepita tangu atoe malalamiko yake Polisi, lakini Jeshi hilo limeona ni busara kwenda kampuni hiyo ili kutafuta mawasiliano yake Mulongo.
Wiki iliyopita, Sabas alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa simu iliyotumika kumtumia Lema ujumbe wa vuitisho ni ya kampuni ya nje ya nchi na siyo namba ya Mulongo.
“Nilipokuwa rumande msaidizi wa Mkuu wa Makosa ya Upelelezi  Arusha alinifuata  na kuniomba nimpe simu yangu, nilimwambia sina nimemwachia mke wangu, na walimtafuta mke wangu na kumuomba hiyo simu na kumhakikishia kuwa akiwapa simu wataniachia na kunifutia kesi.
Mke wangu aliwajibu kuwa simu aliidondosha kwenye gari ya  Polisi ile ambayo walinichukua nayo usiku wa siku waliyonikamata,” alisema Lema na kuongeza.

SOURCE: NIPASHE

HII NI NEEMA KWA WALIOFELI KIDATO CHA NNE....UFAULU WAONGEZEKA, MATOKEO NI MUDA WOWOTE..!



Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.

Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.

Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.

Matokeo ya awali

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.



Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.

Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.

Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.

“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.

Matokeo ya awali ndiyo chimbuko la kupitiwa upya baada ya wadau kuyalalamikia na kumlazimisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume ya kuyachunguza Februari 23, mwaka huu.

Kabla ya tume hiyo kuhitimisha shughuli zake, ilitoa taarifa ya awali ambayo ilipendekeza kufutwa kwa matokeo hayo kwa maelezo kwamba Necta ilitumia kanuni mpya ya kukokotoa matokeo bila kushauriana na wadau.

Serikali ilitoa taarifa bungeni kwamba imeamua kufuta matokeo ya 2012 na kuamuru yapangwe upya kwa kufuata madaraja yaliyotumika mwaka 2011.


WARSHA YA UTENGENEZAJI FILAMU- MAOMBI YAFUNGULIWA...,



 Zikiwa zimesalia Takribani siku 34  ili kuweza kufikia katika Tamasha la kumi na sita la nchi za majahazi lijulikanalo kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) kwa mwaka wa 2013 ambapo linategemewa kuanza mnamo Tarehe 29 ya mwezi wa sita mpaka Tarehe Saba ya Mwezi wa saba mwaka wa 2013.
 Katika kuhakikisha ZIFF inanufaisha watengenezaji wa Film wa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
ZIFF sasa inapokea maombi kutoka kwa watengenezaji filamu Afrika Mashariki wanaotaka kushiriki katika warsha ya utengenezaji filamu wakati wa ZIFF mwaka huu..
Wanafunzi 5 (mmoja toka kila nchi ya Afrika Mashariki) watalipiwa safari, malazi na chakula ili kushiriki kwenye warsha hiyo. Wanafunzi 5 wengine watajilipia wenyewe.
Mfumo wa warsha utakuwa ni kufuatilia kikundi cha watengeneza filamu walio tayari mafundi watakaokuwa wanatengeneza filamu fupi wakati wa ZIFF. Utengenezaji huu unaitwa Guerilla Filmmaking (yaani filamu chapchap) na katika siku 6 filamu itapigwa, itahaririwa na kuonyeshwa ZIFF siku ya mwisho.
Wanaotaka kushiriki kwenye warsha watume maombi yao hivi:
CV fupi.
Maelezo kwa nini wachaguliwe (maneno 1000)
Maombi yatumwe kwa: workshop@ziff.or.tz
Warsha imedhaminiwa na Goethe Institute na GIZ (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani) na Jumuia ya Africa Mashariki (EAC)
Maelezo pia yako www.ziff.or.tz