Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, May 15, 2013

HIP HOP NI ZAIDI YA MAUZO NA HIKI NDO KIASI ALICHOINGIZA MWANA FA KWA KUUZA RBT.

 IMG_1042
Somebody please tell Madee kuwa Hip Hop inauza sana. Kwa mujibu wa Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA ambaye ni mmoja kati ya wasanii wakongwe wa Hip Pop nchini Tanzania leo ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la "Kama Zamani" kwa mujibu wa maelezo yake amekiri kwa kusema hivi karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza miito ya simu aka RBT yanayofikia shilingi za kitanzania milioni kumi na nane (18,000,000).

Akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.
Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.

No comments:

Post a Comment