Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, May 15, 2013

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AWAPA SOMO WAANDISHI WA HABARI...!

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi zao.
Gama alisema hayo akiwataka kuepuka kufanya kazi zitakazowaingiza kwenye mikwaruzo huku akiziagiza taasisi za umma kushirikiana na waandishi wa habari ili kuipa jamii haki yake ya msingi.
Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa habari, taasisi mbalimbali zilizoko mkoani Kilimanjaro, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na taasisi za dini, vyuo vinavyofundisha uandishi wa habari vilivyopo mkoani humo na waandishi wa habari katika kongamano la wanahabari.
Kongamano hilo lililenga kujadili changamoto zinazowakabili wanahabari na maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema mwandishi wa habari anayo nafasi ya kusimamisha nchi na kuibomoa endepo hatazingatia maadili yao huku akisisitizia suala la taasisi mbalimbali kutoa ushirikiano na wanahabari mkoani humo.
“Nafahamu wazi kwamba mnazo changamoto nyingi, ninaloweza kusema ni taasisi za umma kuhakikisha zinawapa ushirikiano na kutosha.
“Hata Rais wa nchi ametoa agizo kwa taasisi zote kutoa habari kwa wanahabari; zingatieni maadili ya kazi zenu na msife moyo katika utendaji wenu,” alisema Gama.
Naye mwenyekiti wa klabu hiyo mkoani Kilimanjaro Rodrick Makundi alitaja changamoto wanazokumbana nazo wanahabari kuwa ni mazingira magumu ya kazi na kukosa ushirikiano kutoka kwa wadau.
Katika risala hiyo Makundi alisema sh milioni 71.9 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa kitega uchumi cha waandishi ikiwemo kuanzisha Saccos yao.
Akiwasilisha mada yake, juu ya changamoto zinazowakabili waandishi wa habari meneja wa Redio Kibo, Abdalah Hussein, alisema waandishi wengi hawana uhakika wa ajira na kwamba wanaishi kwa hofu kutokana na vitendo wanavyofanyiwa vya unyanyasaji na mauaji.

No comments:

Post a Comment