Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, January 31, 2013

BREAKING NEWS: TAARIFA KUHUSU JAHAZI LILILOZAMA NUNGWI LEO JANUARY 31 2013 LIKIWA NA WATU 32...!

Hili ndio Jahazi liitwalo Sunrise lililozama kwenye eneo la Nungwi.

TAARIFA zilizoteka vyombo vya habari kwa sasa ni kuhusu kuzama kwa Jahazi liitwalo Sunrise likitokea Tanga kulekea visiwani Zanzibar likiwa na abiria 32 ambapo limezama kwenye lile eneo la Nungwi ambalo ni hatari siku zote.


Namkariri Kamanda wa Polisi Zanzibar akisema “tayari tumeshapokea watu 21 waliookolewa wakiwa wazima na hakuna maiti iliyopatikana mpaka sasa hivi, waliokuwemo kwenye chombo ni watu 32 hivyo watu bado watu 11 hawajulikani walipo”

Endelea kuisikiliza Clouds Fm pamoja na kupita hapa millardayo.com kwa taarifa zaidi zitakazotufikia wakati wowote

HIVI NDIVYO VIWANGO VYA PUNGUZO LA KUPIGA SIMU KWA MITANDAO YA TZ, MARCH 2013, JAN 2014, 2015 NA 2016

 

 

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imeyataka makampuni ya simu za mkononi Tanzania kuhakikisha yanaanza rasmi mpango wa punguzo la bei ya kupiga simu katika mitandao mingine kutoka bei inayotumika sasa hivi ya shilingi 113 kwa dakika mpaka shilingi 34 na senti 92 ikiwa ni bei mpya inayotakiwa kuanza kutumika kuanzia siku ya kwanza ya mwezi March 2013.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA Profesa John Nkoma amesema uamuzi wa kufanya hivyo ni kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ambapo makampuni hayo yanatakiwa kuanza utekelezaji wa agizo hilo na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa kampuni yeyote ambayo itafanya kinyume na hayo maagizo.

Namkariri akisema “bei itaendelea kushuka kadri miaka inavyokwenda, tarehe 1 january 2014 bei itatakiwa kuwa sh 32 na senti 40, tarehe 1 january 2015 sh 30 na senti 58, tarehe 1 january 2016 itatakiwa kuwa sh 28 na senti 57, hizi bei ni za juu kabisa na Kampuni za simu ni ruksa kwao kuzungumza na wakatumia bei ya chini kabisa”

Wednesday, January 30, 2013

LULU AREJEA URAIANI HUKU AKIBUBUJIKWA NA MACHOZI...!


HATIMAYE msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia amerejea uraiani jana baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Lulu anakabiliwa na shtaka la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu. Aliachiwa kwa dhamana jana saa 9:56 alasiri, baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa ametimiza masharti. Hadi anaachiwa kwa dhamana jana saa 9:55 alasiri, msanii huyo alikuwa ameshakaa mahabusu kwa miezi tisa, tangu alipokamatwa kwa tuhuma hizo, Aprili 7, 2012.

Aliachiwa baada ya Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Francis Kabwe kukagua na kuridhishwa na nyaraka muhimu zilizohitajika kama sehemu ya masharti ya dhamana na kutoa amri kwa msanii huyo kuachiwa huru kwa dhamana.

Dhamana hiyo ilitolewa juzi lakini msanii huyo hakuweza kutoka gerezani kutokana na Msajili wa Mahakama aliyepaswa kuthibitisha vielelezo vya dhamana hiyo kutokuwepo mahakamani.

Akizungumza huku akitokwa machozi muda mfupi baada ya kuachiwa, Lulu alimshukuru Mungu, mawakili wake na watu wote waliokuwa wakimwombea katika mapito yake hayo.

“Nawashukuru watu wote. Watu waendelee kuniombea, hii ni dhamana tu lakini kesi bado ni safari ndefu. Nawashukuru watu wote waliokuwa pamoja nami, namshukuru Mungu kwani yeye ndiye kila kitu,” alisema Lulu.

Mmoja wa mawakili wake, Peter Kibatala aliishukuru Mahakama kwa ushirikiano katika kufanikisha dhamana hiyo... “Sisi mawakili pamoja na Lulu mwenyewe tunaishukuru sana Mahakama kwa kufanikisha haki hii ya msingi. Msajili ametusubiri hadi sasa na hatimaye mchakato huu umetimia.”


Hali ilivyokuwa mahakamani

Lulu aliwasili mahakamani hapo saa 7:58 mchana akiwa kwenye gari la Jeshi la Magereza aina ya Landrover chini ya ulinzi.

Alipofikishwa, alipelekwa katika mahabusu na baada ya takriban saa moja, aliingizwa katika Ofisi ya Naibu Msajili, Kabwe huku akiambatana na wakili wake, Wakili wa Serikali, Joseph Maugo, wadhamini wake wawili na askari Magereza.

Kabwe alipitia masharti yote ya dhamana ikiwamo wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh20 milioni kila mmoja. Bondi hiyo iliwekwa na Florian James Mutafungwa wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Dk Verusi Mboneko Kataruga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Saa 9:26 alasiri alitoka katika ofisi hiyo na kurudishwa mahabusu ya mahakama hiyo kwa ajili ya kukamilisha taratibu nyingine za kimahakama na za Jeshi la Magereza na baadaye aliingizwa masjala ya makosa ya jinai kwa ajili ya kusaini hati ya dhamana.


Baada ya hapo, alitoka nje ya masjala hiyo na kutoa shukrani kwa waandishi wa habari, ndugu na jamaa waliojitokeza mahakamani kisha kuondoka mahakamani hapo kwa gari aina ya Toyota Landcruiser.

Lulu anadaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia, Aprili 7, 2012, nyumbani kwake (Kanumba), Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.



Picha zaidi angalia hapa chini



Dr. Cheni ( Big Brother wa LULU) amekuwa mstari wa mbele toka mwanzo hadi leo



Hapa LULU akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwa huru, Dr Cheni na mama LULU walikuwa karibu nae



OMG..... Familia ni kitu kingine , Mama na LULU akikumbatiana na Mwanawe huku wakilia kwa furaha



Wakili wake akiongea na wanahabari



LULU aliondoka na gari hii kuelekea nyumbani

Habari na James Magai na Vicky Kimaro Chanzo - Mwananchi
Picha - kishymba blog

Monday, January 28, 2013

HATIMAYE LULU ATAKIWA KUTIMIZA MASHARTI YA DHAMANA ILI AREJEE URAIANI...!


MAHAKAMA kuu kanda ya Dar es salaam leo imetangaza dhamana ya mwigizaji muigizaji Elizabeth maarufu kama Lulu endapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni  kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni ishirini za kitanzania.

Upande wa familia ya Lulu wamesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.

Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.