Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, February 23, 2013

BOJ COMPANY LTD YA MJINI MOSHI YADHAMINI FILAMU YA GHOST OF MY MOM

Kundi la CHOPER ART’S GROUP la mjini moshi ambalo kwa sasa lipo kambini katika kijiji cha Soko ndani ya kata ya Kahe katika wilaya ya Mwanga kwa ajili ya Maandalizi ya mwisho ya kufanya Filamu yao inayokwenda kwa Jina la GHOST OF MY MOM.
Kundi hilo ambalo limepata sapoti kubwa kutoka kwa kampuni ya DRM INVESTMENT chini ya mkurugenzi wake Rosemary Migire sasa Kundi hilo limepata Sapoti nyingine kutoka kwa kampuni ya BOJ COMPANY LTD ya mjini Moshi. 
 Baadhi yaWasanii wa Choper art's Group wakiwa katika pozi kabla ya kuanza safari ya kuelekea kambini.



BOJ COMPANY LTD kampuni ambayo inajihusisha na usambazaji wa vifaa vya maofisini, Mashuleni, Vifaa vya Computer n.k iliyopo katika jengo la Vodacom mjini Moshi  Gorofa ya kwanza Room namba 117, Imejitolea kuhakikisha wanawasaidia vijana hao mpaka kukamilisha filamu hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kuchukuliwa picha ya video Tarehe nne mwezi wa Tatu chini ya Kampuni ya Uwezo video Production ya jijini Dar es Salaam chini ya Mtaalamu wa video Farid Uwezo, Huku ikiwa chini ya Muongozaji anayekuja kwa kasi katika kuongoza video Bora Lea Mwendamseke au maarufu kama Lamata.

CHADEMA WASEMA "KAWAMBWA AMEBAKIZA SIKU KUMI TU"

                                                    
 Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika
KAULI ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kwamba hawezi kujiuzulu, imeamsha hasira ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho kimesisitiza kwamba maandamano ya kumng’oa yako pale pale na sasa amebakiza siku kumi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika wakati alipotakiwa kueleza msimamo wa chama chao, hasa baada ya kauli ya Waziri Kawambwa jana kwamba hawezi kujiuzulu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mnyika ambaye ni Mbunge wa Ubungo, alisema kauli aliyoitoa Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe kwamba anampa siku 14 Waziri Kawambwa ajiuzulu, vinginevyo atang’olewa kwa maandamano bado ipo pale pale.

Alisema majibu ya Waziri Kawambwa yameonesha dharau kwa Watanzania, hasa walalahoi ambao ndio watoto wao wengi wamepata ziro katika mitihani yao ya kidato cha nne.

“CHADEMA tunaendelea kusisitiza kwamba Waziri Kawambwa ang’oke, awajibike, ameshindwa kazi na hili tunamaanisha,” alisisitiza Mnyika.

Alisema CHADEMA inaangalia namna ya kuitisha maandamano hayo kwa kuwashirikisha vijana waliofeli kwani wanaamini wamehujumiwa.

Mnyika aliwataka Watanzania na wengine wenye uchungu na udhaifu wa elimu ya Tanzania, hasa wazazi wajitokeze kwani fedha walizowekeza kwa watoto wao kwa ajili ya elimu, zimeteketea.

Wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Furahisha, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ikiwa ni ufunguzi wa Baraza la Viongozi wa CHADEMA, Kanda ya Ziwa Magharibi, Mbowe alitoa siku 14 kwa Dk. Kawambwa na Naibu wake, Philipo Mulugo, kuhakikisha wamejiuzulu nyadhifa zao.

Mbowe ambaye aliongoza maandamano makubwa ya magari na pikipiki kuelekea uwanjani hapo, alisema Kawambwa, naibu wake, Mulugo, pamoja na katibu mkuu wa wizara hiyo, wameshindwa kuiongoza sekta hiyo muhimu, ndiyo maana kwa sasa wanafunzi wanaishia kuandika matusi na kupata sifuri katika mitihani.

Alisema waziri huyo lazima ajiuzulu nafasi hiyo, kwani taifa ameliingiza pabaya na kuanza kuzalisha maelfu ya watoto wa maskini kumaliza elimu zao za msingi na sekondari wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Alisema hili ni janga la kitaifa, hivyo lazima Kawambwa aondoke ndani ya wiki mbili, vinginevyo CHADEMA itaitisha maandamano makubwa nchi nzima kushinikiza kiongozi huyo ang’oke madarakani.

“Kwa vile Kawambwa ameshindwa kuisimamia vema sekta hii ya elimu, na kwa vile watoto wetu wengi wanafeli na kuishia kuandika matusi kwenye mitihani yao, CHADEMA tunampa wiki mbili awe amejiuzulu.

“Kila mwaka wanafunzi 1,200,000 hadi 1,300,000 nchi nzima wanafanya mitihani yao. Lakini wanaoshinda ni kati ya 35,000 hadi 400,000 pekee, hivyo watoto wengine wanashindwa kuendelea na masomo yao. Kwa hiyo tunataka huyu waziri na naibu wake wajiuzulu ndani ya wiki mbili,” alisema Mbowe.

Alisema kwa sasa Tanzania inazalisha vijana wapatao 800,000 kwa mwaka ambao wanakosa fursa ya kuendelea na masomo yao, na alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha kucheka na kubembeleza viongozi wabovu wanaodidimiza maendeleo ya nchi na raia wake, na kwamba Tanzania inakabiliwa na majanga makubwa mawili ya elimu duni na udini.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alimtaka Waziri Kawambwa na Naibu wake, Mulugo, kuwajibika na kupisha katika wizara hiyo.

Pia alimtaka Rais Kikwete aichukue wizara hiyo na kuwa chini ya ofisi yake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Zitto alisema kuwa ni muhimu viongozi wanaosimamia wizara hiyo wakawajibika.

Alisema uwajibikaji huo unapaswa kufanyika kuanzia kwa katibu mkuu wa wizara hiyo pamoja na kamishna.

Zitto alisema kuwa rais anapaswa aelezwe kuwa iwapo matokeo yatabaki hivi mwakani, na yeye atatakiwa kuondoka katika nafasi hiyo.

Chanzo:
Tanzania Daima

Friday, February 15, 2013

BARUA YA MASIKITIKO ALIYOIANDIKA PAPII KOCHA KWA MH. RAISI JK...!

 
MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha) Gereza Kuu Ukonga S.L.P 9091 Dar es Salaam Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU. Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya kiMUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais. Nakuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais, kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maishagerezani,niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo, na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo. Si mimi, baba yangu Nguza wala ndugu yangu yeyote aliyefanya kitendo kile. Lakini wenye mamlakawakatuona tuna hatia na kuamua kuteketeza kizazi chetu gerezani. Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi. Lakini pia sisi ni binadamu wenye nafsi na miili kama wengine. Waliotumia mamlaka yao kutuweka gerezani nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi. Ipo siku nafsi zetu zitapaswa kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu tunayoitumia kunyanyasa wanyonge itakuwa imeoza mavumbini. Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu. Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu. Mungu akubariki. Wako mtiifu Mfungwa NO:836'04 JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA).

UPIMZIKE KWA AMANI Goldie Harvey

Nigerian Singer (© Facebook)

Following her sudden death on Valentine’s Day, we remember Nigerian singer and star Goldie Harvey.
Harvey passed away at the Reddington Hospital in Victoria Island, Lagos after a short illness. The former Big Brother housemate died shortly after returning from the Grammy Awards in the US.
The singer first shot to fame in 2006 when she released her debut album Spin Me. Harvey was a contestant on Big Brother Africa in 2012. While on the show she met and started a relationship with Kenyan star Prezzo.
"Goldie, 31, died on Thursday after she complained of a severe headache shortly after her arrival from the United States where she went to witness the Grammy Awards. She was rushed from her Park View, Ikoyi, Lagos residence to her official hospital, Reddington, Victoria Island, Lagos, where doctors pronounced her dead on arrival at exactly 7:30pm in the evening," the statement posted on Facebook said.
"We consider this period a gloomy moment for us and the entire Nigerian music industry in view of the circumstance in which she passed away; the abundance of talent she exhibited in her short but eventful music career and the various opportunities her trip to the United States of America would have availed her.
"She is survived by her father, step- mother, brothers and sisters. We deeply sympathise with her family and fans all over the world and very grateful to all and sundry, especially, the vibrant Nigerian media for their concern and prompt reportage. We shall keep everybody informed as events unfold as we are devastated by the sudden loss.”
According to reports, Harvey’s sudden passing has been attributed to pneumonia. Fans are gathering outside the Lagos hospital where she passed to mourn the star.

Thursday, February 14, 2013

MAJINA YA AJIRA ZA WALIMU HAYA HAPA...!

BUNGE LA TANZANIA LASITISHA VIKAO VYA BUNGE KUONESHWA LIVE KWENYE RUNINGA...!

BUNGE KUSITISHA KURUSHA VIKAO VYAKE.

BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.

Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.

Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile ya Mashirika ya umma POAC zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi juu ya hatua hiyo.
Chanzo:jamiiforum

LOWASSA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUREJESHA AMANI KATI YA WAISLAMU NA WAKRISTO


WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amewataka viongozi wa dini nchini kusaidia kurejesha hali ya amani kati ya Waislamu na Wakristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.

Akizungumza nyumbani kwake Monduli, wakati akipokea ujumbe kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa alisema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buseresere mkoni Geita yanasikitisha sana na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.

``Rais ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba viongozi wa dini na madhehebu yote wasimamie kuzuia mambo haya, nawaomba Watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu isipotee,” alisema.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, aliongeza kuwa Watanzania wameoleana, wamekuwa wakiishi pamoja kwa miaka yote bila kubaguana kwa misingi ya dini, rangi wala kabila, na kuhoji haya mambo yanatoka wapi.

Alisema kuwa Tanzania imekuwa ni mfano wa kuigwa kote dunia kutokana na amani iliyopo, ambayo ni matunda ya uongozi wa waasisi wa taifa hili hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume.

Katika fujo hizo za Buseresere, mchungaji mmoja wa kanisa aliuawa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya Waislamu na Wakristo, chanzo kikiwa ni Wakristo kuamua kuchinja ng’ombe na kuuza kwenye bucha yao, hatua iliyopingwa na Waislamu.

Ujumbe huo uliofika nyumbani kwa Lowassa uliongozwa na msaidizi wa askofu mteule wa KKKT dayosisi hiyo, ulimshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa kuu la Shinyanga Januari mwaka jana ambapo zaidi ya sh milioni 200 zikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi zilipatikana.


Chanzo: kalulunga.blogspot.com

NCHI YA ZIMBABWE KUPIGIA KURA KATIBA MPYA.!


Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai anasema nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wa bunge na urais mwezi Julai baada ya kupiga kura maoni juu ya katiba mpya mwezi Machi.

Alisema hayo Jumatano baada ya waziri wa maswala ya katiba Eric Matunenga kupanga tarehe ya Machi 16 kwa ajili ya kupiga kura ya maoni.

Katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare , Matinenga alieleza wasi wasi wake kuwa muda hautoshi na pengine muda zaidi huenda ukahitajika kwa ajili ya uchaguzi wa Machi.

Baraza la kitaifa la bunge (NCA) ambalo linajumuisha makundi ya harakati za kidemokrasia huko Zimbabwe limesema litapinga tarehe upigaji kura wa maoni hapo Machi 16 mahakamani .

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika mwenyekiti NCA Lovemore Madhuku amesema kundi lake linataka serikali itoe kipindi cha mdahalo cha miezi miwili hivi kabla ya wapiga kura kufanya uamuzi wao juu ya katiba mpya.

Chama cha Bw. Tsvangirai cha MDC na kile cha rais Robert Mugabe cha ZANU PF wote wanaunga mkono mabadiliko hayo mapya.

Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini inataka katiba mpya iidhinishwe kabla ya Zimbabwe kufanya uchaguzi mkuu.

KUNDI LA PAH ONE LASAMBARATIKA ...!



Taarifa zilizogonga vichwa vya habari katika uwanja wa burudani Bongo ni kwamba kundi lililowahi kutamba na ngoma kali la Pah One limevunjika rasmi after First Lady wa kundi hilo mwanadada Aika na mpenzi wake Nahreel, Rapper ambaye pia ni Producer wa kundi hilo kutangaza kujitoa kwenye kundi.
Akichonga nasi Aika amesema sababu ya iliyomfanya ajitoe kundini ni kutokuwa na maelewano mazuri ndani ya kundi hilo na kuongeza kuwa Nahreel ni Solo Artist so wasilaumiwe kwa uamuzi wao na mapenzi yao yasihusishwa na kujitoa kwao katika kundi.

Nahreel na Aika wanatarajia kuachia ngoma yao ya kwanza wakiwa kama Solo Artists Siku ya Valentine mapema mwezi huu.

HU NDIO UJUMBE WA VALENTINE'S DAY KWA MARAFIKI WOTE...!

Leo Ni Siku ya Wapendanao (Valentine's Day) Na nivyema kila moja wetu kuendeleza kudumisha au kuimarisha upendo wake kwa mtu au watu ambao anawapenda kwa dhati. Lakini pia ni siku ambayo ni vyema kwa kila moja wetu kuwa makini sana mana watu wengi huitumia siku hi kwa kudanyanya kua anaupendo wa dhati kumbe lengo lake ni kukidhi mahitaji na kukuacha na maumivu. 
 
Picha hi iwe somo kwa marafiki wote na fans wa blog hii.

Mtandao huu wa w.kingjofa.blogspot.com unawatakieni valentine's day njema na yenye furaha tele..


Wednesday, February 13, 2013

ANGALIA PICHA 10 ZA SHAMRASHAMRA ZA MAPOKEZI YA MABINGWA WA AFRICA HUKO NIGERIA...!

Timu ya Taifa ya Nigeria ikiwasili Abuja Nigeria.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MOTO UMEWAKA TFF WAZIRI AINGILIA KATI, ATUMA UJUMBE MZITO KWA TENGA ...!

Siku moja baada ya kamati ya rufaa ya shirikisho la soka nchini kumuengua mgombea uraisi wa TFF, Ndugu Jamaly Malinzi kutoka kwenye kugombea uraisi katika uchaguzi ujao wa TFF, leo hii wadau tofauti wa michezo wametoa maoni yao kuhusiana na sakata. Mmoja wa wadau aliyepaza sauti kuzungumzia suala hilo ni naibu wa waziri wa michezo, Bwana Amos Makalla.

Akizungumza na Ibrahimu Masoud kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM leo usiku, Makalla alisema ameshangazwa sana na kitendo cha kamati ya rufaa kumuengua Malinzi kwa sababu ambazo ameziita hazina mashiko na zimekuosa ushawishi.


"Mimi kama mdau wa soka na michezo kwa ujumla napenda kusema kuhusu hili bila kupepesa macho kwamba kamati hii imepotoka kwenye suala hili. Hii kamati kwenye hili inataka kujishushua heshima, unajua wakati mwingine unaweza kujishushia heshima kwa gharama nyepesi. 


"Sababu walizotoa kumuengua Malinzi zimekosa ushawishi. Hoja walizotoa mimi kama mwanamichezo naona hazina mashiko. Malinzi anakosa vipi uzoefu sasa hivi, huku akiwa kiongozi wa chama cha soka cha mkoa? Alishawahi kuwa katibu wa klabu kubwa kama Yanga kwa miaka kadhaa, pia hi huyu huyu Malinzi ambaye aligombea uraisi wa TFF dhidi ya Tenga wakati huo, sasa iweje kipindi hicho aweze kugombea na sasa hivi ashindwe eti kisa kakosa uzoefu. Uzoefu gani wanauzungumzia ambao alikuwa nao kipindi hicho na asiwe nao sasa," aliongeza Naibu waziri huyo.


"Maamuzi ya namna hii yanadhoofisha kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya Jakaya Kikwete katika kurudisha uzalendo kwenye michezo. Raisi amefanya mengi katika kuhamasisha watu kupenda michezo, sasa hivi watanzania tumeanza kupenda michezo. Tenga ameongoza vizuri na sasa tunahitaji TFF makini itakayokuwa ikiongozwa na viongozi makini watakaoiongoza soka yetu na hatimaye tuweze kwenda AFCON na World Cup.


"Mimi kama waziri wa Michezo ninamuomba Raisi Tenga aliyewateua watu wa kamati hiyo aingilie suala na kuweka sawa, hali isije kuwa mbaya na watu wakaanza kupoteza upenzi na soka kwa mambo ya ajabu kama haya. Viongozi wa kamati kama walitaka tujue na madaraka na uwezo wa kufanya hili walilofanya wamefanikiwa kwa hilo, lakini sasa nawaomba watumie busara. Wasiwafanye watanzania waache kupenda mpira, wasiturudishe nyuma na jitihada za serikali katika kukuza michezo. Nawaomba wamrudishe Malinzi kura zipigwe kwa haki tupate uongozi bora." - alimaliza naibu waziri huyo wa michezo na utamaduni.

DIAMOND PLATINUM ASEMA "MAMA YANGU NDIO MGANGA WANGU"...!



Diamond akipata baraka za mama yake

Huenda ile story ya kwamba Diamond amepata na anaendelea kupata mafanikio kutokana na kutumia waganga wa kienyeji si kweli!! You never know! Staa huyu ambaye gazeti la Daily Nation limemtaja kuwa miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava matajiri zaidi, yupo karibu mno na mama yake mzazi na pengine ndio maana anafanikiwa, nani kama Mama? Vipi kama mafanikio yake ni thawabu halisi kutoka kwa Mwenyezi Mungu?

Akipiga stori na thesuperstarstz diamond amesema kuwa yeye ana mtegemea mungu na katika dunia nguzo yake pekee ni mama yake mzazi hivyo kama kuna swala la mganga basi mama yangu ndio mganga wangu kwani haniruhusu kutoka hadi tumefanya dua kumshukuru mungu,msanii huyo aliendelea kuchonga na thesuper starstz kuwa hawezi kufanya jambo bila mama yake na hata akitaka kutoka ni lazima apate dua na baraka za mama yake mzazi na ndio maana anafanikiwa sana msanii huyo ambaye anatajwa sana katika vyombo vya habari amesema anamuamini mungu na ndio maana hawezi kupoteza hata dakika moja bila kumuomba mungu.

The super stars tz ilifunga safari hadi nyumbani kwa diamond maeneo ya sinza mori na kuongea na bi mkubwa huyo ambaye alianza kwa kusema,,,Namshukuru mungu kwa kunipa afya pia na mshukuru kwakuzidi kumuangazia mwanangu Nasibu katika kazi zake alisema mama huyo,na alipoulizwa kuhusu kashfa zinazomkabili mwanae mama huyo amesema kuwa si za kweli na ana muamini sana mwanae na hajamlea katika mazingira hayo alimaliza mama huyo.

Hizi ni picha ambazo Diamond ameziweka kwenye website yake na kuandika kwenye moja ya picha hizo: Siku zote kabla ya kwenda popote lazima tupitie kwa mama yetu mpendwa atupe Barka zake na nyingine hiyo juu akiandika: Nikipokea baraka za Mama ….Nijaliwe Mema….na Niende kwa Amani…!!

 
Wasafi wakipata baraka za mama


Diamond akisalimiana na mashabiki wake

The super stars tz inazidi kumpongeza kijana Diamond kwa kazi nzuri na kumuombea mungu aendelee kumjalia katika kazi zake pia inawaomba wadau haswa watanzania tuthamini vya kwetu tusiwe watu wakuongea na kutafuta mabaya ndio tuyaseme kijana anajitaidi basi tumuunge mkono ili afike kama akina jiga ,50 na wengine tunao waona na kuwasikia huko kwa wenzetu.

Tuesday, February 12, 2013

SERENGETI, NGORONGORO NA MLIMA KILIMANJARO YAFANIKIWA KUINGIA KATIKA MAAJABU 7 YA VIVUTIO BARANI AFRIKA ...!

?????????????????????? 
TANZANIA kupitia shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) limefanikiwa kuingia katika maajabu saba katika bara la Afrika kupitia vivutio vyake vitatu bora vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro na Hifradhi ya Serengeti ambavyo viliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi zingine hali ambayo itafanya Sekta ya utalii hapa nchini iweze kukua na kuimarika

 Akitangaza matokeo hayo jana mjini hapa, rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani,alisema kuwa katika kinyanganyiro hicho Tanzania imepata ushindi kwa kuwa vivutio vya aina yake.

Alitaja vivutio hivyo kuwa ni Pamoja na Mlima Kilimanjaro,hifadhi ya Serengeti pamoja na bonde la Ngorongoro ambapo vivutio hivyo viliweza kupigiwa kura nyingi sana na hivyo kuvipa ushindi wa hali ya juu huku  ndani ya vivutio hivyo kuna maajabu ya aina mbalimbali ambavyo havipatikani popote barani Afrika na duniani kwa ujumla

“leo nina furahi kutangaza kuwa Tanzania imeingia ndani ya maajabu saba na hivyo basi hii ni kama changamoto ya kuhakikisha kuwa bado mnaendelea kufanya viendelee kukua na kuinarika zaidi ili hata wakati mwingine muwe na vivutio vingi zaidi’aliongeza Dkt Imler.

Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema kuwa nchi za Afrika zina vivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya kukuza pato kupitia utalii huo.

Alisema anaamini kutokana na sifa ambayo Tanzania imeipata kupitia vivutio vyake vitatu itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato la taifa.

Aliongeza kuwa ndani ya Nchi  ya Tanzania kwa sasa wamejiwekea juhudi za makusudi kuanzia ngazi ya kitaifa ambapo kupitia ngazi mbalimbali wataweza kuharakisha maendeleo ya utalii hususani utalii ili maajabu mbalimbali ya Tanzania yaweze kufahamika duniani.

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema ushindi huo ni historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la Watanzania wote kujivunia.

kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa hapa nchini(TANAPA)Alan Kijazi alisema kuwa wanatarajia mapato kuongezeka hasa katika mlima Kilimanjaro,bonde  la Ngorongoro, na hifadhi za Serengeti kwa kuwa vivutio hivyo vimetangazwa rasmi kama vivutio venye maajabu ya kutosha

Alisema Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya kushinda na Watanzania waendelee kuutunza, Ngorongoro alisema kuwa imeshinda kwa kuwa na wanyama wa kila aina kama Big Seven: simba, tembo, viboko, nyati, vifaru, sokwe na mamba.

Kijazi aliongeza kuwa pamoja na kutangazwa kwa vivutio hivyo lakini bado TANAPA limejiwekea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wanaendeleza shuguli za utalii hapa nchini ingawaje bado kuna changamoto kubwa sana kwenye masuala ya utalii wa ndani

??????????????????????
Rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa Marekani akitangaza matokeo hayo
??????????????????????
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo akihutubia mara baada ya kutangazwa kwa vivutio hivyo
??????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
????????????????????????????????????????????

??????????????????????

??????????????????????
??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????
??????????????????????
??????????????????????

JACKLINE WOLPA AELEZEA SIRI NYINGINE ZA MAISHA YAKE KAMA ASINGEKUA STAR WA BONGO MOVIE...!

MSANII wa filamu Tanzania Jackline Wolpa anaamini mafanikio hutokana na juhudi, kujituma pamoja na kutimiza malengo yako uliyojiwekea kwa kipindi ulichokusudia

Msanii huyo wa filamu alielezea maisha yake yako nje ya Tasnia ya filamu alipokutana na mwandishi wa safu hii

Wolpa mbali na kuigiza pia yeye ni mcheza netiboli katika timu ya bongo movi akiwa anachukua nafasi ya mfungaji 'GS' huku akiwa tishio kwa timu pinzania kwa uwezo alionao na jinsi anavyoweza kutumia urefu aliokuwa nao kwa kufunga magoli mengi

Alianza kucheza netiboli akiwa shuleni na huko ndipo alipopata ujuzi wa mchezo huo ambapo mpaka sasa ameweza kuwa tishio kwa kuumudu mchezo huo na kuweza kuisababishia ushindi kwa timu anayoichezea

Alisema kuwa anapata muda wa kutosha kufanya mazoezi kila siku jioni na asubuhi hivyo mazoezi yanamsaidia kujenga mwili wake pia na kumpa pumzi zinazomsaidia kucheza kipindi chote bila ya kupumzika mpaka mwisho wa mchezo

Aliendelea kusema kuwa kwa upande wake anathamini sana mazoezi kwani yanamfanya kuzidi kuwa imara na pia hutumia mazoezi kwake ni kama dawa ya kuondoa uchovu katika mwili wake

Wolpa aliweka wazi kuwa kama ingekuwa si muigizaji basi angekuwa mchezaji mzuri wa netiboli na angeongeza nguvu katika hilo na kuweza kuchezea timu kubwa na anaamini kuwa angefanya vizuri kwenye upande huo

Anaeleza kuwa hatoweza kusahau siku alipoumia vidole vya mikono kwenye mechi iliyokuwa inachezwa katika viwanja vya Leaders Club na aliweza kuendelea kucheza mchezo huo na hatimaye waliibuka washindi katika mechi ya kujipima

Mbali na kucheza netiboli pia msanii huyo ni bingwa wa kuogelea, huku akidai kuwa muda wake mwingi wa mapumziko anautumia kuogelea ili kuweka mwili wake imara

Aliongezea kuwa mara nyingi huwa anaratiba ya nini afanye muda gani na kipi kifanyike wakati gani hiyo ndiyo moja ya kitu anachoamini kuwa kinampa mafanikio makubwa katika maisha yake

Wolpa alisema huwa hapendi kuwa na makundi ya watu hivyo hawezi kuamua kwenda kukaa bar kama hana kazi ya kufanya kwa sababu ratiba yake inakuwa imejaa muda wote ule

Wolpa ambaye pia alikuwa anafanya biashara ingawa sasa anajipanga kuianzisha tena biashara yake ili maisha yake yaendelee kuwa yenye mafanikio kwa juhudu anazozifanya

Aliongezea kuwa anapenda kusoma vitabu muda wa mapumziko zaidi kuliko kwenda kukaa bar na marafiki ambao kwake anahisi laba hawana mafanikio ingawa si kila rafiki ni mwema au ni mbaya hivyo kwa upeo wa kiubinadamu huwezi kutambua hilo kwa haraka

Anasema kuwa kusoma vitabu kunamsaidia kumjenga kiuwezo na fikira pia inamuongezea kuwa mbunifu hususani katika kazi zake za sanaa

Wolpa ni msanii wa filamu ambapo alianza kuigiza mwaka 2009 na filamu iliyomtambulisha ni Amazangu amazao kwa sasa anatamba na filamu nyingi ikiwemo ya Ndoa yangu aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba

OMY DIMPOZ APANIA KUFUNIKA USIKU WA VALENTINE'S DAY MOSHI

Katika kusheherekea Siku ya Wapendanao Duniani, Ndani ya Moshi kumekumbwa na homa kali ni Homa ya kushuhudia kundi la Kigoma All Stars ambao wanatarajia kudondosha bonge la show ndani ya Ukumbi wa Aventure Africa ulioko Majengo moshi. 

Akipiga story na King Jofa Msanii anayekuja kwa kasi kutoka katika kundi la Kigoma All Stars Omy Dimpoz amesema usiku huo utakuwa wa kipekee kwani atawapa ladha ambayo hamjaipata kutoka kwa msanii yeyote, Pia amesema atawapa kile alichowapa wakazi wa Dar Es Salaam katika uzinduzi wa video yake mpya aliyofanya na Vanesa Mdee alimaliza kwa kusema. "Wakazi wa Moshi wakae Mkao wa kula."



Katika usiku huo wa wapendanao utaambatana na Burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii kama Baba Levo, Recho, Maunda Zoro, Abdul Kiba, Chege, Omy Dimpoz na Peter Msechu pamoja na zawadi kibao, Kwa wale wapenzi watakaopendeza watapatiwa zawadi ya Silver Set kwa mwanamke zenye thamani ya zaini ya shilingi laki nne na Mwanaume atapatiwa Bracelet ya silva yenye thamani zaidi ya laki mbili kutoka Sonara kubwa Moshi mjini iliyopo mkabala na bank ya Exim Bank iitwayo ASMM PEAK GEMSTONE DEALERS LTT au maarufu kama SONARA SANAAAAAA !!!!




Pia Duka maarufu la uuzaji wa nguo za kike za Mitumba na Washauri wa Mavazi kwa wakina Dada lililopo Moshi mjini Mkabala na Mr Price City linajulikana kama A & A CLASSICS BOUTIQUE watatoa zawadi ya Vocha ya Kufanya Shopping kwa Mwanadada Atakayetoka Ki valentine siku hiyo.

Hii Si ya kukosaaaaaaaaaa

BAADA YA PAPA BENEDICT WA XVI KUTANGAZA KUJIUZURU, HAWA NDIO MAKARDINALI WAAFRIKA AMBAO WANAPEWA NAFASI KUBWA ZAIDI YA KURITHI KITI CHA UPAPA...!

 Kardinali Francis Arinze akiwa katika shughuli mbalimbali za kanisa
 
 
 Kardinali Peter Turkson wa Ghana
 
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP.

Katika taarifa yake, Papa amesema amefikia uamuzi huo ambapo sasa ana umri wa miaka 85.
Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi rasmi tarehe 28 Februari, mwaka huu saa mbili kamili asubuhi.
Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano mikoba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka Afrika.
Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki, linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima.
Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa Nigeria ambaye alichukua nafasi ya Benedict XVIkama Kardinali-Askofu wa Velletri-Segni alipoteuliwa kuwa Papa miaka nane iliyopita.