Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, March 30, 2013

UHURU KENYATA AUTHIBITISHIA ULIMWENGU KUWA YEYE NDIE RAISI HALALI WA KENYA KWA KURA NA MAHAKAMANI PIA...



MAHAKAMA KUU YAAMUA UHURU NDIYE MSHINDI HALALI

MAHAKAMA ya Juu imekataa ombi la Waziri Mkuu Raila Odinga wa CORD la kutaka ibatilishe uchaguzi wa Uhuru Kenyatta wa muungano wa Jubilee kuwa rais. Hii ina maana kuwa Bw Kenyatta sasa ataapishwa kuwa rais Aprili 9.

“Mahakama ya Juu imefikia uamuzi kwa kauli moja kuhusu masuala manne yaliyoibuliwa kwenye kesi za uchaguzi. Uchaguzi ulifanyika kwa njia huru na ya haki na kwa kufuata Katiba na Sheria,” alisema Jaji Mutunga kabla ya kutangaza kuwa Uhuru Kenyatta na William Ruto walichaguliwa kwa njia huru na ya haki kuwa Rais na Naibu Rais mtawalia.

“Kesi za Raila na AFRiCOG zimetupwa. Kila mtu ajilipeie gharama. Uamuzi wa kina utatolewa katika muda wa wiki mbili.”

Kuhusu kesi ya wanaharakati Dennis Itumbi na Moses Kuria kuhusu kura zilizokataliwa, Jaji Mutunga alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa uamuzi.

Alihitimisha kwa kutoa wito kwa Wakenya wadumishe amani.

“Mahakama imetekeleza jukumu lake. Jukumu sasa ni kwa raia, viongozi wao, mashirika ya kijamii na wanahabari kuhakikisha umoja wa Kenya unadumu,” alisema Jaji Mutunga.

RAILA AKUBALI KUSHINDWA, AMTAKIA UHURU KILA LA HERI

WAZIRI MKuu Raila Odinga amekubali kushindwa baada ya Mahakama ya Juu kutupilia mbali kesi yake kupinga kupinga kuchaguliwa kwa Uhuru Kenyatta. Bw Odinga amemtakia Rais Mteule kila la heri.

“Hatua yangu ya kwenda mahakamani ilikuwa ishara ya imani yangu katika Mahakama. Haikuwa ni ya kisasi. Tulijaribu kadiri ya uwezo wetu. Mawakili wetu wakiongozwa na Oraro walikusanya na kuwasilisha ushahidi mwingi.”

“Tunasikitika kwamba Mahakama ilikataa ushahidi kwa msingi kuwa uliwasilishwa kuchelewa au mahakama haikuwa na muda. Mwishowe, Wakenya walipoteza nafasi ya kujua nini kilitendeka.”

“Mimi na Kalonzo hatuna majuto kwa kuwasilisha kesi kortini. Ni matumaini yangu kwamba serikali ijayo itaheshimu Katiba na kuitekeleza. Namtakia Rais Mteule Uhuru Kenyatta na kundi lake kila la kheri. Pia, maseneta wabunge, wawakilishi wa wanawake na magavana ufanisi. Tusigawanywe na mtukio haya. Natoa wito kwa Wakenya na wafuasi wangu wakumbuke maneno ya Wimbo wa Taifa – “Haki iwe ngao na mlinzi.’”




Monday, March 25, 2013

WEMA SEPETU AMTENGANISHA KAJALA NA UKUTA WA GEREZA

Leo ilikua ni siku ya Huzuni sana kwa msanii wa Filamu Kajala MAsanja, na Pia ni siku ya Furaha na ya kihistoria katika maisha yake. Akiwa mbele ya Mahakama akisikiliza kwa Makini hakimu akisoma hukumu ya kesi inayomkabili, Hakimu akisoma vipengele vya sheria na mwisho alipomaliza kesi hiyo kwa kumuhukumu Kajala Masanja kwenda Jela miaka Nanea au kulipa faini ya Shilingi milioni kumi na tatu.

Hukumu hiyo ilikua ni mzigo kwa kajala iliyopelekea kutokwa na machozi akiwa kizimbani mbele ya wasanii wenzake wa bongo Muvi. Bila kuongea Chochote Icon wa Bongo Muvi Wema Isaack Sepetu alitoka eneo la Mahakama hiyo kimya kimya na kurudi baada ya muda akiwa na Fedha Taslim shilingi milioni Kumi na Tatu na kumtoa Kajala katika kifungo hicho. Bila kuamini kajala Hakuishiwa kutokwa na machozi huku akiwa haamini kama kweli Wema kamuokoa Kutoka katika kifungo.



Kwa niaba ya KingJofa naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Wema Isaack Sepetu kwa Moyo aliouonyesha na pia kumpa Pole kajala kwa Mitihani ya maisha aliyopitia na sasa ni wakati wa kujipanga katika harakati za kulijenga taifa.

Monday, March 18, 2013

BREAKING NEWS: Askari wa usalama barabarani agongwa na gari!


Askari wa usalama barabarani katika mataa ya kuongezea magari yaliyoko eneo la Bamaga Dar es Salaam amegongwa na gari na inadhaniwa amekufa papo hapo.

 Wasamaria Wema wakifuniaka mwili wa Askari wa Usalama barabarani baada ya kugongwa na gari.

Friday, March 15, 2013

SOMA ALICHOSEMA DIAMOND KUHUSU KUOA NA KUMNUNULIA MKE WAKE MTARAJIWA GARI YENYE THAMANI YA MILIONI 15...!


Kupitia segment ya U Heard ya XXL Clouds FM na Soudy Brown, mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa bongo alieandikwa sana kwenye internet mwaka 2012 amethibitisha kumnunulia mkoko mama watoto wake mtarajiwa.

Soudy Brown alimuuliza kuhusu fununu za kutumia Milioni 15 kununua gari la mke wake mtarajiwa mtangazaji Penny ambae kwa sasa ni mjamzito.

Diamond amekiri kwamba ni kweli kamnunulia Penny gari kwa sababu anaelekea kuwa mama watoto ambapo namkariri akisema “nilimuuliza gari gani anapenda, nimemuagizia iko njiani inakuja siwezi kusema ni bei gan ila kwa sasa anatumia la muda wakati akisubiria gari lake”

Alipoulizwa kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond amejibu “siwezi kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza ikawa harusi ila kuna time inafika inabidi utulie, siwezi kusema chochote kwa sababu inawezekana mtoto akazaliwa ndani ya ndoa pia “

Mh. BERNARD MEMBE AKANUSHA KUHUSIKA NA SAKATA LA ABSALOM KIBANDA KAMA ILIVYOANDIKWA NA GAZETI LA MTANZANIA...!


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe. 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika gazeti la Mtanzania toleo namba 7255 la tarehe 13 Machi, 2013 ilitolewa taarifa yenye kichwa cha habari “SAKATA LA KUTESWA KWA KIBANDA: Membe atajwa” na kwamba eti mimi ninahusika na vitendo vya kikatili na unyama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari, Bw. Absalom Kibanda.Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na habari hizo na ningependa kuwahakikishia Watanzania wenzangu kwamba sijahusika, sihusiki na sina sababu ya kuhusika kwa namna yoyote ile. Sina nia, genge wala fedha za kufanya shughuli kama hiyo. Katika maisha yangu yote, sijawahi kugombana naye na hajawahi kunifanyia ubaya wowote. Kwa kifupi, sina uhasama na Bw. Absalom KIbanda.Taarifa iliyotolewa na Mtanzania ni taarifa ya uongo, ni habari za kuunga-unga maneno na habari za kughshi. kwa vyovyote vile, mwandishi wa habari hii na wenzake wana malengo ya kisiasa anayoyajua yeye na wenzake wanaomtumia. Huu ni mwendelezo wa mkakati wa kisiasa wa kunichafua ambao umekuwa ukiendelezwa na wale wasionitakia mwema. Wanajaribu kuwaondoa Watanzania katika kiu yao ya kutaka kufahamu ukweli wa jambo hili.

Nawashukuru sana wananchi wenzangu, jamaa na marafiki walioniletea salamu za kunitia moyo. Naungana nao katika kujiuliza, hivi kiburi hiki, dhihaha hii na ujasiri huu wa kusema uongo hadharani wanautoa wapi!? Jeuri na kiburi cha namna hii hakiwezi kutokana na sheria za nchi, haki ya kikatiba wala hofu ya Mwenyezi Mungu. Naomba Watanzania wenzangu mnisaidie kutegua kitendawili hiki. Naamini kwa dhati kwamba ukweli kuhusu suala hili utajulikana na yeyote mwenye ushahidi wa kweli aonyeshe uzalendo wake kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.

Mwisho, wakati nashauriana na wanasheria wangu kuona hatua ya kuchukua dhidi ya kuchafuliwa huku, nawaomba Watanzania wenzangu tuvute subira na tuache vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi zake ili Watanzania hatimaye wajue ukweli wa kilichotokea.
Bernard Kamillius Membe (Mb).
WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Monday, March 11, 2013

HUYU NDIO MTOTO WA MIAKA 8 ALIYEMUOA MWANAMKE WA MIAKA 61...!

Hii imetokea Tshwane South Africa.

Huyu mtoto anasema wazee wa zamani ndio walimuamrisha aoe lakini pamoja na hilo, hawajasaini cheti cha ndoa na wala hawaishi pamoja ambapo wazazi wa huyu bwana harusi walichangia harusi kwa kutoa euro 1500 ambazo walisisitiza ni kama matambiko na sio kisheria.

Mtoto huyu aitwae Sanele amekaririwa akisema “nilimwambia mama yangu, nahitaji kweli kuoa na nimefurahi nimemuoa Helen lakini nikikua nitaoa mwanamke wa umri wangu”

Mama mzazi wa Sanale anasema “babu yake ndio alimchangulia Sanale amuoe Helen kwa sababu yeye(Babu) anampenda, na wamefanya hivyo ili kutimiza maagizo ya wazee wa koo ambao wameshafariki, yani ni kama matambiko”

.


Wednesday, March 6, 2013

HII NDIYO KAULI YA OBAMA BAADA YA KIFO CHA RAIS WA VENEZUELA HUGO CHAVEZ

Baada ya taarifa za uhakika kutoka kuhusu kifo cha Rais wa Venezuela Hugo Chavez amefariki dunia, kupitia taarifa ambayo imetolewa na kituo cha Al Jazeera Rais Barack Obama wa Marekani amesema nchi yake imehamasika kuanza mazungumzo ya uhusiano mpya wa nchi hizo mbili.


Rais Hugo Chavez amefariki akiwa na umri wa miaka 58 akisumbuliwa na kansa na taarifa yake kutangazwa usiku wa kuamkia march 6 2013 ambapo kifo chake kilitangazwa na makamu wa Rais Nicolas Maduro ambae sekunde 40 baada ya kuanza kutangaza kifo hicho alishindwa kuzuia hisia zake na kulazimika kusimama kuongea kwa muda kutokana na machungu.

Friday, March 1, 2013

MOSHI KWACHAFUKAAAAAAAAAAAAA!!!



Ikiwa ni siku moja tu imebakia kufika siku ya jumapili, Siku ya Mbio za Kilimanjaro Marathon zinazofanyika kila mwaka nchini Tanzania Mkoani Kilimanjaro. Moshi kumefurika watu.

Wakati unaingia ndani ya Mji wa Moshi utakutana na mabango makubwa pembezoni mwa barabara yanayokuashiria kuwa kuna tukio kubwa limewadia mjini Moshi, Si lingine ni Kilimanjaro Marathon 2013.

                               Hili ndilo Bango linalokukaribisha ndani ya Mji wa Moshi

Hali ya kiburudani imeanza toka wiki iliyopita mji wa Moshi a na umechangamshwa na leo katikati ya viunga vya mji wa Moshi katika barabarA ya Voda Club linadondoka bonge la Event litakalohusisha wapenzi wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager na wakimbiaji wa mbio za Kilimanjaro marathon maarufu kama Kili Marathon iliyodhaminiwa na Kampuni ya bia Tanzania. {TBL} ku kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.


 Anaitwa Abraham ni Sound Engineer wa Bills akihakikisha  sound inakaa vizuri leo

Leo anzia saa moja jioni kutakua na burudani kibao kutoka kwa Twanga Pepeta, Joh makini, Warior band from the east na wengine kibao huku nyama choma na bia vikiwa vimesambaa kila kona.
Kama huna pesa bora ulale……! Mimi nitakuwepo.


                                      Stage ikiwa imesimama vyema nje ya voda Shop