Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, February 28, 2014

HAWA NDIO WASANII WATAKAOTUMBUIZA KWENYE USIKU WA KILIMANJARO MARATHON

WASANII mbalimbali wanatarajia kutoa burudani leo usiku katika Ukumbi wa Voda House mjini Moshi ikiwa ni mkesha kabla ya kufanyika kwa mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon Jumapili zitakazoanzia katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa burudani hiyo ni moja ya hamasa kabla ya kufanyika kwa mbio hizo.
Aliwataja wasani watakaotoa burudani katika siku ya mkesha huo wa Kilimanjaro Marathon kuwa ni Jambo Squad,
Jambo squad
 

 
The warrios

Extra Bongo
Joh Makini
 “Kwa mwaka huu tumeona tufanye tofauti kwa kuweka burudani katika siku ya mkesha kabla ya kufanyika Kilimanjaro Marathon,” alisema.

Alisema pia siku ya mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon kutakuwepo na burudani kutoka kwa Joh Makini, Jambo Squad, Wakali Dancers na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma.

Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.


Credit: Dixonbusagaga Blog

No comments:

Post a Comment