Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, March 2, 2014

PANONE AND CO. LTD. WAWADHAMINI NA KUWAKABIDHI VIFAA VYA KUSHIRIKI KILIMANJARO MARATHON KWA WATOTO WA SALAMA CETRE.

Muwakilishi wa  Panone and co. ltd, Kassim Mwinyi akipeleka tisheti za watoto katika kituo cha SALAM CENTRE.


Afisa masoko wa Panone ndugu Frank Mwaikatale akikabidhi tisheti za watoto wa kituo cha SALAMA CETRE kwa mlezi wa watoto hao Bi. Upendo.

 Afisa masoko wa Panone ndugu Frank Mwaikatale akiwakabidhi baadhi ya watoto wa kituo cha SALAMA CETRE namba za kushiriki katika mbio za Kilimanjaro marathon.

Panone and co. ltd ni kampuni ya Usambazaji na uuzaji wa mafuta ya magari jumla na rejareja. Ikiwa imejikita katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja na kwa masaa ishirini na nne yaani usiku na mchana. Katika kuhakikisha jamii inapatahuduma Muhimu katika kila kituo kuna supermarket na huduma ya kibenki na kifedha kupitia simu ya mkononi M-Pesa inayopatikana muda wote. Panone and co. ltd ina bakery ya kisasa ambayo kwa sasa inazalisha mikate inayokwenda kwa jina la Panone Bread, Queen Cake, Pan Cake, Maandazi na pia inafanya Parking ya Mchele, Korosho, Karanga vyote vikiwa katika nembo ya Panone. 

Akizungumza na Mwanahabari wetu Afisa masoko wa Panone ndugu Frank Mwaikatale alisema Panone katika kuhakikisha inashiriki vyema na Jamii na kuthamini michezo imeweza kudhamini timu ya riadha ya Mkoa kilimanjaro ilikuhakikisha inashirikivyema katika mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon. Mbali na timu hiyo pia imeweza kutoa Udhamini kwa watoto waishio katika mazingira Magumu wanaolelewa katika kituo cha SALAMA CENTRE kilichopo Majengo Moshi. Udhamini huo ni katika kuhakikisha kituo hicho kinafikia Lengo la watoto 50 kushiriki katika mbio fupi za kilometa tano zinazofahamika kama "FUN RUN" zinazodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano Tanzania Vodacom. 

Mbali na hilo pia Panone and co. ltd imeweza kuwatengenezea watoto hao wa SALAMA CENTRE tisheti zenye ujumbe maalumu wa kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa watoto katika mbio hizo ujumbe ambao unasomeka. "Let's KidsRun for fun" Pamoja na kuwapatia vifaa mbalimbali. Katika kuhakikisha jamii inatambua bidhaa zinazozalishwa na Panone katika uwanja wa Ushirika kutakua na banda maalumu kwa ajili ya kuonesha bidhaa zinazozalishwa na Panone.


No comments:

Post a Comment