Jamii hapa nchini imetakiwa
kushirikiana na serikali katika kuwafichua majangili wa wanyama
pori katika hifadhi za taifa hapa nchini hali ambayo inalitia hasara
taifa kwa kupunguza idadi ya watalii , pia kupoteza rasilimali ambayo ni urithi
kwa vizazi vilivyopo na vile viajavyo.
Afisa wanyamapori wa malihai club Tanzania Saidi Mshana , ametoa
kauli hiyo alipofanya ziara katika hifadhi ya taifa ya mlima kilimanjari
(KINAPA), akiandamana na wanafunzi ambao ni wanachama wa club hiyo
wapatao 160 , wanaosoma katika shule za sekondari za mikoa minne ya kanda ya kaskazini kwa lengo la kupinga ujangili
wa wanyama pori.
Bw. Mshana amesema vita
vya ujangili wa wanyama pori ni vikubwa hapa nchini hivyo
kila mtanzania anawajibu wa kushirikiana na serikali katika vita hivyo kwa kutoa
taarifa kwenye vyombo husika pindi wanapobaini mtandao wamajangili ili hatua stahiki ziweze
kuchukuliwa dhidi yao.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi Joshua John wa Arusha na Salome
Jumbe wa Kilimanjaro wamesema, umefika wakati sasa kwa serikali
kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kutunga sheria zenye adhabu kali ili
kila atakayebainika kujihusiha na mtandao ujangili ,aweze kuwajibishwa
kwa
mujibu wa sheria.
Aidha baadhi ya wanfunzi walioshiriki katika ziara hiyo Abubakari Molel wa Arusha na Emiliana Msodoka wa Tanga mkoani wameiomba
wizara husika kuhamasiha jamii kushiriki katika utalii wa ndani kwa kutoa matangazo kupitia katika vyombo mbalimbali
vya habari pia kutoa elimu kuanzia shule za msingi na maeneo ya vijijini ili
jamii iweze kunufaika na rasilimali zilizopo katika nchi yao.
No comments:
Post a Comment