Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, July 22, 2014

KILA WILAYA NCHINI TANZANIA ZATAKIWA KUJENGA CHUO CHA UFUNDI

Wilaya zote nchini zimetakiwa kujenga vyuo vya ufundi ili watoto wanaomaliza elimu katika ngazi mbalimbali hapa nchini  waweze kujiunga katika vyuo hivyo  ili waweze kupatiwa elimu itakayowawezesha kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa maofisini  au kwenye makampuni.

Waziri mkuu wa  jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la chuo cha ufundi cha Gonja wilayani Same, mkoani Kilimanjaro kinachojengwa kwa udhamini wa kampuni ya kutengeneza magari ya Suzuki, pamoja na uhifadhiwa faru na mbwa mwitu katika hifadhi ya taifa mkomazi.

Waziri mkuu aliendelea kusema kila wilaya inawajibu wa kujenga chuo cha ufundi na chuo kikuu cha ufundi kwa kila mkoa  ili kuhakikisha vijana wanaomaliza elimu yao watumie fursa hiyo kujiajiri wenyewe ili kuondoa tatizo la ajira hapa nchini.
 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Suzuki, inayofadhili ujenzi wa chuo hicho Bwana Ted Van Dam aliseama pamoja na kampuni yake kujishughulisha na utunzaji wa faru na mbwa mwitu katika hifadhi hiyo, wameona ni vyema kujenga chuo hicho ambacho kitakuwa na manufaa kwa wakazi wa wilaya na Same na taifa kwa ujumla.

Akiongea katika uzinduzi huo Mbunge wa jimbo la Same mashariki Anne Kilango Malicela pamoja na kuwashukuru wafadhili wa mradi huo pia aliiomba serikali kuigawanya wilaya ya same kwa kuwa imekuwa ni kubwa mno kijiografia hali ambayo inayosababisha maendeleo ya wilaya hiyo kusuwasua.

No comments:

Post a Comment