Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 24, 2014

MIZANI MPYA YA NJIAPANDA YA HIMO YAWAPUNGUZIA WASAFIRISHAJI KERO YA MUDA MREFU

KILIMANJARO  kufuatia kero ya miaka mingi ya wadau wa usafirishaji wa abiria na mizigo mkoani kilimanjaro katika mizani ya Njiapanda ya Himo wilayani Moshi imeondolewa baada ya wakala wa barabara mkoani Kilimanjaro (TANROAD) kukamilisha ujenzi wa mizani mpya katika barabara kuu inayotokea Moshi kuelekea Dar es salaam.
 
Wakizungumza na muandishi wa mtandao huuj ana  baadhi ya wadau wa usafirishaji walisema kuwa kabla ya kujengwa kwa mizani hiyo walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kupoteza muda mrefu katika foleni ya kupima uzito katika mizani ya mwanzo.

Hata hivyo wadau hao Francis Ali, Salum Awadhi, na Wilton Meena walisema  kujengwa kwa mizani hiyo kutaondoa kero mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili ikiwa ni pamoja kukaa kwa muda mrefu katika mizani hiyo bila kupatiwa huduma ya kupimimwa uzito kwa magari yao.

 Aidha walisema kuwa  kuna haja ya kuiongezea uwezo barabara hiyo ambayo hupitisha magari mengi  ya ndani na nje ya Tanzania  kwa kuwa mizani mpya ni ndogo na haiwezi kukithi mahitaji


Mizani hiyo imeanza  kutumika mwanzo mwa mwenzi Julai Mwaka 2014 ambapo magari yote yanayo toka Dar es salaam na Tanga yanapima uzito katika mizani mpya na yale yanayotoka Arusha, Moshi na nchi jirani kupitia Namanga na Mombasa yanapima uzito wake  katika mizani ya zamani.

Kwa upande wake Meneja wa TANROAD mkoani Kilimanjaro Marwa Rubrya alisema, mizani hiyo mpya imegharimu fedha nyingi sana, baada ya kilio cha muda mrefu cha usafirishaji na abiria wakiwemo wafanyabiashara.

 Nae afisa wakala wa vipimo mkoani Kilimanjaro Efremu Asenga, alithibitisha ubora wa mizani hiyo mpya baada ya kuifanyia tathmini ya vipimo kitaalamu ili kuondoa malalamiko ya kuzidishiwa uzito yaliyokuwa yakitolewa na wamiliki na madereva wa magari hayo.

 Afisa wa zamu wa mizani ya zamani Abubakari Makoi alisema kuwa, idadi ya magari yaliyopimwa katika mizani hiyo kwa kipindi cha wiki tatu za mwezi julai yalipungua kutoka 7509 wakati kabla ya mizani hiyo mwezi juni katika kipindi hicho magari 15,242.

No comments:

Post a Comment