Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 25, 2014

MTU ANAYESADIKIKA NI KIBAKA AMEUWAWA KIKATILI NA KUTELEKEZWA BARABARANI

MOSHI kibaka wa uporaji kwa kutumia nguvu vitu  mablimabali katika nyumba za watu ameuwawa kikatili  na watu wasiojulikana  kwa kupigwa mawe kichani  katika mtaa wa kaloleni, kata ya Pasua, manispaa ya Moshi, Mkoani kilimanjaro.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert boaz, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba julai 24 mwaka 2014 majira ya saa 1:00 kamili asubuhi wapita njia walikuta mwili huo metelekezwa ndipo wakatoa taarifa polisi.

Boaz alisema kuwa  kijana huyo ametambulika kwa jina moja  la  Alen (25) maarufu kwa jina la Mmeruu na kwamba alikuwa anatafutwa na jeshi la polisi kwa muda mrefu kutokana kupora watu kwa nguvu vitu mbalimbali.

Alisema mwili huo ulikuwa na majeraha makubwa kichwani, na damu nyingi zikiwa zimevuja, huku pembeni ya mwili huo kukiwa na mawe makubwa ambayo yalitumika kumjeruhi marehemu

“Uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini chanzo cha kifo cha marehemu  ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua waliofanya kitendo hicho cha kinyama”alisema Boaz.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Mawezi kamanda amewataka ndugu na jamaa kwenda kutambua mwili huo.

No comments:

Post a Comment