Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, July 27, 2014

MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO HENRY LYIMO (KIPESE) AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA PIKIPIKI


MOSHI mtangazaji wa habari za michezo wa Moshi FM radio iliyopo mkoani Kilimanjaro Henry Lyimo maarufu kwa jina la Kipese amefariki dunia jana usiku.

Kifo chake kilisababishwa na ajali mbaya iliyotokea jana jioni maeneo ya Mwika wakati Kipese akitokea Rombo katika majukumu ya kikazi akirudi Moshi mjini. Ajali hiyo ilisababishwa na kugongana kwa pikipiki aliyokuwa akiitumia Kipese na pikipiki nyingine ambayo haijafahamika kwa haraka ilikuwa ya nani.

Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kilema iliyopo wilaya Moshi vijijini ukingojea utaratibu utakaofuata baada ya ndugu wa Henry Lyimo kufanya maamuzi.

uongozi mzima wa mtandao huu wa king jofa unawapa pole sana ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.

No comments:

Post a Comment