Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 31, 2014

MWENYEKITI WA KIJIJI AKUTWA NA SHAMBA LA BANGI.

JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwenyekiti wa kijiji  cha Kisangesangeni Joseph Owoko kwa tumuma za kujihusisha na ulimaji na uuzaji wa bangi.

Akithibisha kukamatwa kwa Mwenyekiti huyo kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema mwenyekiti huyo alikamatwa na makachero wa jeshi hilo julai 28 majira ya saa 10:30 jioni katika kijiji cha kisangesangeni, Kata ya Kahe wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akielezea mazingira ya tukio hilo Boaz alisema askari polisi walipata taarifa juu ya mwenyekiti huyo kujihusisha na ulimaji wa zao la bangi pamoja na uuzaji wa zao hilo na kufika  katika nyumba anayoishi Mwenyekiti huyo na kufanya upekuzi.

Boaz alisema askari baada ya kufanya upekeuzi katika nyumba hiyo kulikutwa kilo 30 za bangi zikiwa ndani ya gunia aina ya kiroba.

Alisema baada ya askari kukuta bangi hiyo walifanya upekuzi katika mashamba yake ambapo mita 20 kuto anapoishi kulikutwa shamba la bangi lenye ukubwa wa robo heka likiwa limestawi  bangi ziliko tayari kwa kuvunwa.

Aidha alisema katika msako mwingi askari hao walibaini shamba lingine la bangi lenye ukuwa wa zaidi ya robo heka likiwa limepandwa bangi ambalo ni mali ya Frances Kidonga.

Alisema mtuhumiwa alikimbia pasipo kujulikana na kwamba askari hao walichukua jukumu la kufyeka mashamba yote ya bangi .

Boaz alise jeshi la polisi linaendelea na msako mkali ili kuweza kumtia nguvuni mtuhumiwa aliye kimbia na kwamba uchunguzi bado unaenelea ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchuliwa dhidi ya Mwenyekiti huyo.

No comments:

Post a Comment