Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, July 21, 2014

RATIBA YA WAZIRI MKUU KWENYE ZIARA YAKE MKOANI KILIMANJARO

MOSHI waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Mizengo Pinda, anatarajiakufanya ziara ya kikazi ya siku moja wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, kwa lengo la kuweka jiwe la msingi la Chuo cha Maendeleo ya jamii Maore wilayani Same.

Ziara hiyo anatarajia kuifanya leo, ambapo atakwenda katika wilaya ya Same, kuweka jiwe la msingi katika chuo hicho, kilichopo kijiji cha Muheza kata ya Maore, na mara baada ya hapo atatenmbelea hifadhi ya taifa ya Mkomazi na kisha kuzindua nyumba ya Mwalimu katika kata hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, ambayo imetolewa na Kaimu mkuu wa mkoa huo, Dkt. Ibrahim Msengi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuja kumlaki kiongozi huyo.

Pia Dkt. Msengi amesema mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika chuo hicho atapata fursa ya kuongea na wananchi wa eneo hilo.

Waziri huyo aliwasili mkoani Kilimanjaro jana majira ya saa kumi jioni, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa KIA, na baadae alikwenda katika Ikulu ndogo ya mjini Moshi na kupokea taarifa ya mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment