Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, July 21, 2014

TANESCO MKOANI KILIMANJARO YAANZA ZOEZI LA KUWEKA MITA ZA LUKU KWENYE KILA NYUMBA

Shirika la umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro linatarajia kuanza kuboresha huduma kwa wateja wake ikiwa ni pamoja na kubadilisha mita zote za zamani na kuweka mita za malipo kabla (LUKU) ili kuleta ufanisi zaidi katika kutoa huduma za nishati ya umeme.

Meneja wa Tanesco mkoani Kilimanjaro mhandisi Martin Kasyanju, aliyasema hayo ofisini kwake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema, kwa kutumia mita za malipo kabla (LUKU)  kutaongeza ufanisi zaidi, pia utawaondolea wateja kero ya  kupanga foleni na badala yake wataweza kujinunulia umeme kwa njia ya mtandao wa simu.

Alisema zoezi  hilo litakalofanyika wiki hii likianzia manispaa ya moshi, ambapo  wateja wote  watabadilishiwa mita zao bila kuchajiwa gharama yeyote hivyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi washirika, wakati wakitekeleza zoezi hilo.

Afisa Mahusiano wa Tanesco mkoani Kilimanjaro Bi. Grace Kisyombe alisema, kutokana na kukithiri kwa baadhi ya ya wateja kujiunganishia umeme kiholela mkoani Kilimanjaro na kulisababishia shirika hasara ya zaidi ya shilingi bilioni nane (8,000,000,000) jumla ya watu saba wamefariki dunia huku baadhi ya watu wakifikishwa mahakamani kwa kosa la kuliibia shirika la Tanesco umeme.

No comments:

Post a Comment