Habari
njema kwa watanzania wote wenye matatizo ya macho winaoishi mkoa wa
Kilimanjaro na maeneo ya karibu. Huduma hii ya kuvanyiwa vipimo vya
macho na kupewa dawa au miwani inatolewa na madaktari kutoka Marekani
wanaofahamika kwa jina la “Artists for world peace”.
Huduma hiyo inapatikana bure na kwa mtu yeyote mwenye matatizo ya macho,
anaweza kufika katika
kijiji cha onan kuna katika kituo kipya cha afya kinaitwa “Good Hope”
ila wakazi wa eneo hilo la kibosho wamezoea kupaita kwa “mayatima” kwa
kuwa mmiliki wa kituo hicho ana kituo cha kuwalelea watoto yatima
kinachofahamika kwa jina la “Good Hope”.
Unaweza kupanda haice (daladala) zinazoelekea kibosho ubwe, katika stand
kuu ya mabasi Moshi mjini kisha ukawaambia wakushushie kibosho ubwe au
kwa raphael, ukishuka utaona pikipiki (bodaboda) unauliza kwenye huduma
ya miwani, wakazi wote wa eneo hilo wanapafahamu na watakuelekeza, na
kwa wale wenye usafiri binafsi wanaweza kufika bila tatizo lolote maana
barabara ni nzuri.
Na kwa mtu yeyote mwenye kuhitaji kupata maelekezo ya ziada anaweza
kupiga namba hii +255 (0) 764 505 284 ni namba ya mama ni na anaitwa
Josephine Machuwa.
Na huduma itatolewa tena kuanzia tarehe 8 August 2014 hadi tarehe 10
August 2014 yaani ijumaa, jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu asubui
mapaka saa kumi na mbili jioni.
No comments:
Post a Comment