Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 6, 2014

KUZAGAA KWA TAKANGUMU KWASHUSHA HADHI YA MKOA WA KILIMANJARO

MOSHI wakazi wa mtaa wa relini kata ya bomambuzi iliyopo katika halmashauri ya manispaa ya Moshi mkoani kilimanjaro wameulalamikia uongozi wa halmashauri hiyo kwa kushindwa kusimamia sheria za usafi wa mazingira hivyo kusababisha takangumu kuzagaa katika maeneo mbalimbali, hali ambayo inakuhatarisha afya za wakazi wa maeneo hayo. 


Wakazi hao wakiongea kwa nyakati tofauti, walisema tatizo la kuzagaa kwa takangumu katika mtaa huo ni la muda mrefu, na uongozi wa halmashauri hiyo ikifumbia macho hali hiyo ya uchafu. Waliendelea kusema kuwa hali hiyo inahatarisha afya zao hususani kwa watoto wadogo, ambao hucheza kwenye taka hizo na kuokota vitu mbalimbali. 

Waliendelea kulalamikia uongozi uliopo madarakani kwa kusema taka hizo zimekuwa zikisababisha, harufu mbaya na inzi kuzagaa hadi kwenye makazi ya watu na kibaya zaidi ni pale wanapochangishwa shilingi elfu moja (1,000) kwa kaya kwa kila mwezi, huku takataka zikiachwa bila kuzolewa. 

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mboga na matunda wa soko la mbuyuni, lililoko kata ya Bondeni Bw. Lameck Mziray alisema hali ya uchafu katika manispaa hiyo kwa sasa ni mbaya hususani maeneo ya pembezoni mwa mji, hali ambayo inatokana na uwezo mdogo wa kiutendaji katika halmashauri hiyo. 

Kwa upande wake, kaimu mkurugenzi wa halmashari ya manispaa ya Moshi Bi. Martha Kimambo, amekiri kuwepo kwa changamoto ya uzoaji wa takangumu katika halmashauri hiyo, na kufafafanua kuwa, imetokana na baraza la madiwani kuwaondoa mawakala wa kusimamia sheria za usafi, na badala yake kuwatumia watumishi wa halmashauri hiyo, Halmashauri ya manispaa ya Moshi, imekuwa ikiongoza kwa usafi hapa nchi nzima kwa miaka nane mfululizo, lakini kwa mwaka huu imeshuka na kushika nafasi ya pili, hali ambayo imesababishwa na kulegalega kwa usimamizi wa sheria za usafi wa mazingira katika manispaa hiyo.

No comments:

Post a Comment