Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, March 30, 2015

Matembezi ya hamasa kupinga mauaji ya Albino - IMETOSHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr, Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu, Mwakilishi wa Chama cha Albino  Tanzania (TAS), Abdillah Omar sambamaba na wadau wengine wakishiriki kuimba wimbo 'Tanzania Tanzania' kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.

Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na  Mwanamuziki wa Reggae,Jhiko Manyika "Jhikoman" wakati wa shughuli nzima ya hamasa ya  kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar  es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.



Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud "Kipanya" akimkaribisha Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni jijini Dar es salaam leo.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Mbunge wa Viti Maalum,
Al Shaymar Kweigyr wakiongoza matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment