Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 31, 2015

DAVIS MOSHA AWALIZA WANANCHI WA MOSHI...,

 Mh. Davis Mosha akizungumza na wakazi wa Moshi katika Mkutano wa Kuwaaga.


Aliyekua Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mh. Davis Elisa Mosha amewaaga Wananchi na wanachama wa ccm jana jioni katika vbiwanja vya Penfold vilivyopo katika hifadhi ya Raylway Mjini Moshi. Katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Mamia ya Wananchi wa Moshi huku wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa wamevalia Nguo za ccm.
Baada ya viongozi mbalimbali kumaliza kuongea ndipo majira ya saa kumi na Moja Mh. Davis Elisa Mosha alipata fura ya kuzungumza na Wananchi wa Moshi na kuwaaga. Kitendo cha Mosha kupanda jukwaani kulizua kelele na shangwe kwa Wananchi zilizodumu kwa Zaidi ya dakika tano mpaka pale alipowaomba wamsikilize. Mosha alianza kushukuru Wananchi wa Moshi kwa upendo mkubwa waliomuonesha katika kipindi chote cha Miezi mitatu aliyokaa nao Pamoja katika harakati za kuomba ridhaa ya kuongoza jimbo la Moshi na kuleta Maendeleo.

Sehemu ya Umati wa wananchi wa Moshi waliojitokeza kumsikiliza Mh. Davis Mosha.



Pia Mosha aliweza kuwalaumu viongozi wa ccm kwa kushiriki katika harakati za kudhoofisha jitihada zake za kuongoza jimbo hili huku akiwaasa wanachama wa ccm kutumia nafasi iliyopo kuweza kubadili uongozi wa chama kama kweli wana nia ya dhati ccm ije kuongoza jimbo la Moshi Mjini.

“Baadhi ya viongozi wa ccm wamenunuliwa, Ni mamluki na wanakiuza chama. Si wakati wa kulia Wananchi wa Moshi na wanachama ni wakati wa kuanza kwa mchakato wa kusafisha chama ndani ya Moshi na kuwaondoa viongozi ambao si waaminifu” Alisema Mosha.

Wananchi wakiwa hawaamini kama Mh. Davis Mosha ndio anawaaga sasa.


Hata hivyo hali ilibadilika Ghafla baada ya Davis Mosha kutangaza kutorudi na kugombea tena ndani ya Jimbo la Moshi ndipo Wananchi na wanachama walipoangua kilio na wengine kuzimia. Hali hiyo ililipa kazi ngumu jeshi la Polisi kwa kuwa hawakua wamejiandaa na hali iliyojitokeza pamoja na kutokuwepo na watu wa huduma ya Kwanza. Kitendo hicho kilipelekea viongozi mbalimbali wa ccm na Wananchi kumuomba Mosha kusitisha maamuzi yake ili kunusuru Maisha ya Wananchi hao waliokua wakilia kwa uchungu na wengine kutishia kujidhuru. Mosha aliwasihi wasilie na aliwaahidi kuimiza ahadi zake zote alizoahidi ambazo zipo ndani ya uwezo wake.


Wananchi na wanachama wa ccm wakiangua vilio kwa majonzi.







Mwishoni ililazimu jeshi la Polisi kumshinikiza Ndugu Mosha kushuka jukwaani na kuelekea katika Gari lakini Wananchi walimzuia kuingia kwenye gari na kutembea nae Zaidi ya kilometa tano kutoka eneo la Mkutano mpaka Nyumbani kwake Kiboriloni. Baada ya kufika nyumbani Wananchi hawakuridhika walimzuia kuingia ndani mpaka azungumze nao ndipo alipozungumza nao na kuwaahidi hatoondoka mpaka ajue hatima ya Jimbo la Moashi ikiwemo kushughulikia baadhi ya tuhuma za sitofahamu zinazohusu mapungufu ya Uchaguzi.

Jeshi la Polisi likimsindikiza Davis Mosha baada ya kumalizika kwa Mkutano.

No comments:

Post a Comment