Huu ndio ukumbi uliharibiwa na washabiki mjini stuttgart,Ujerumani
UJERUMANI Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30 Augasti 2014, majira ya saa 10 alfajiri Mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor Nasib Abdul almaarufu Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show, mashabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 (ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi elfu hamsini na tano za kitanzania) kwa kiingilio, waliaidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anaejulikana kwa jina la Britts Event.
Hapo ndipo mashabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake, Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa. Mmoja wa Djs hao alipoteza kompyuta pakato “Laptop” yake, mwanadada DJ Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal.
Polisi nchini Ujerumani wamesema tukio hili la aibu alijawahi kutokea,n kwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao. Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashtaka promoter huyo raia wa Nigeria, ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Chanzo: Magazeti ya Stuttgart

No comments:
Post a Comment