KILIMANJARO baadhi ya wafanyakazi wa
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi iliyoko mjini Moshi,
walikusanyika katika ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Kilimanjaro, wakidai
kurudishiwa fedha zao za bima ya afya walizokatwa katika mishahara yao.
Wakiongea kwa sharti la kutokutajwa kwenye
vyombo vya habari baadhi ya wafanyakazi hao walisema walikatwa fedha zao kwenye
malipo ya mishahara ya miezi mitatu.
Walisema wafanyakazi wa halmashauri zingine
walishalipwa fedha zao na kwamba wao bado hawajapata haki zao na wanapofuatilia
swala hilo baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wamekuwa
wakiwapa majibu yasiyo ya kuridhisha ikiwemo kuwakejeli.
Akiongea na wanahabari kuhusiana na swala
hilo, meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kilimanjaro,
Fidelis Shauritanga, alikiri kuwepo kwa makosa hayo na kusema kuwa tayari ofisi
hiyo ilisharudisha fedha hizo ofisi ya katibu tawala mkoani wa mkoa wa
Kilimanjaro.
Alisema katika ofisi ya katibu tawala wa Mkoa
wa Kilimanjaro, wanachama 178, walibainika kukatwa kimakosa na Shilingi Milioni
7,539,612 zililipwa katika ofisi ya Ras toka mwanzoni mwa mwezi julai mwaka huu
2014.
Alisema ya kuwa kwa hali hiyo ofisi ya bima
ya afya ilishatimiza wajibu wake na kwamba haipaswi kunyooshewa kidole cha
lawama kutoka na mtu mwingine kushindwa kuwajibika.
Meneja huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka
waajiri ambao hawajawasilisha fedha hizo kwa watumishi waliokatwa, kuwasilisha
mara moja, ili kuwaondolea watumishi hao, usumbufu ambao wamekuwa wakiupata.
Akiongelea swala hilo katibu tawala wa Mkoa
wa Kilimanjaro, Dkt. Faisal Issa, alikiri kuwepo kwa kasoro hiyo na kwamba
tayari limeshaanza kushughulikiwa.
No comments:
Post a Comment