HII NDIO MSG YA MATUSI DOGO JANJA ANADAI MADEE ALIJIANDIKIA AKIJIFANYA DOGO JANJA.
Posted: 17th June 2012 by MillardAyo
1
Hii ni moja ya msg anazodai
Dogo Janja kwamba Madee ndio alikua anajitumia baada ya kumnyanga’nya
simu ili kuja uwaonyesha watu kwamba Dogo Janja ndio aliziandika.
Dogo Janja anasema Madee hajui kutumia simu ya Blackberry vizuri hivyo hayo maneno ya mwanzoni alikua bado hajaijulia vizuri.
Kuna meseji nyingine kadhaa ambazo haziwezi kuwekwa hapa kwa sababu zina matusi sana.
Dogo Janja ambae sasa yuko kwao Arusha aliondoka alhamisi kurudi kwao baada ya kukataa kuendelea kuwa chini ya usimamizi wa Madee akidai kwamba hayakua maisha mazuri, alidhulumiwa kuteswa na hata kutokupata matunzo aliyotakiwa kuyapata.
Ijumaa akiongea Exclusive kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Janja alisema kwamba “sitaki kabisa kusoma Dar es salaam nitakwenda kusoma Arusha au mkoa mwingine wowote, alijitumia msg nyingi sana alizoandika kupitia simu yangu ili mimi nionekane mbaya, kuna nyingine aliandika producer Maneke ni snich tu, nyingine mimi nitamloga yani sikuweza kufikiria kwamba mtu mzima wa miaka 32 anaweza kumfanyia kitu kama hicho mtoto wa miaka 16″

Dogo Janja mwenye shali la kaki akiwa anaondoka Dar kwenda kwao Arusha Alhamisi June 13, hapo ni katika stand ya Ubungo.
“Naapa kwa mwenyenzi Mungu kama nimekula hata shilingi kumi yake nife hata sasa hivi yani, mpaka ilifikia kipindi nikienda kufanya show Mwanza nakwenda kwa Mamu nanunua kopi zangu 20, album niliuza bure mimi nikawa nanunua kwa shilingi elfu mbili pale dukani Umoja, nikifika mikoani ndio nauza CD moja labda shilingi elfu 5 napiga sign watu wanakuja wananunua, kihalali ile Album sikunufaika nayo chochote, wamenufaika nayo watu” – Dogo Janja.
Nitafanya tena interview na Madee soon ili kujibu alichosema Dogo Janja.
No comments:
Post a Comment