Banner

Banner

wegazi.com

wegazi.com

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 22, 2014

Tazama na Dowload wimbo wa Smaina - Wayaga (Official Music Video)


Video mpya kutoka kwa Smaina wimbo unafahamika kwa jina la  WAYAGA
Video :Directed by Msafiri (Kwetu Studios)
Audio : Produced By Mesen Selekta (De Fatality Music)

Afya za wafanyabiashara wa soko la Uchira hatarini kwa kujisaidia katika mifuko ya rambo

KILIMANJARO wafanyabiashara  wa soko la  Uchira, katika  wilaya ya Moshi vijijini, mkoani Kilimanjaro,  wapo hatarini  kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa huduma ya vyoo na maji, hivyo kulazimika kujisaidia kwenye mifuko ya rambo na kutupa kinyesi hicho hovyo.

Hali hiyo imejitokeza kutokana na wafanyabiashara  hao kukaa kwa muda mrefu katika soko hilo bila ya kuwa na huduma ya vyoo na maji katika sehemu hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwanaharakati wa mtandao huu wa "Kilimanjaro Official Blog", baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, walisema hali hiyo ya ukosefu wa vyoo inasikitisha kutokana na wafanyabiashara hao kwenda kujisaaidia kwenye vibanda vinavyo zunguka soko hilo na kutupa hovyo uchafu huo.

Walisema kwa takribani miaka 10 soko hilo halijawahi kuwa na vyoo wala maji, licha ya wakala ambaye amepewa tenda ya kukusanya ushuru akiendelea kuwatoza fedha hizo huku huduma za kijamii zikikosekana sokoni hapo.

Jenipha Marandu, alisema soko hilo linakabiliwa na harufu mbayo kutokana na watu kujisaidia kwenye mifuko ya  rambo na pindi wanapokwenda hospitali wamekuwa wakigundulika na ugonjwa wa maambukizi katika mfumo wa kutolea mkojo (U.T.I)

Jeremiah Joseph, mkazi wa Uchira alisema kutokana na ukosefu wa vyoo katika eneo hilo wafanyabiashara hao wamekuwa wakijisaidia kwenye  vibanda vilivyopo karibu na soko hilo na kuweka kinyesi hicho kwenye mifuko ya rambo na kuitupa katika shimo ambalo lilichimbwa na kuachwa wazi bila kukamilishwa.

Njarita Japutia, mkazi wa kijiji cha Uchira alisema tangu soko hilo liwepo halijawahi kuwa na choo, pia hakuna dalili ya kupata vyoo wala maji katika soko hilo, wala hawajawahi  kusomewa  taarifa ya mapato na matumizi ya michango yao kwa kipindi cha miaka mitano.

Alifafanua kuwa soko hilo linamzabuni ambaye amekuwa akiwatoza ushuru wafanyabiashara hao licha ya kuwa huduma za kijamii zinazotakiwa kuwepo katika soko hilo hazipo, licha ya wafanyabiashara hao kuendelea kuchangishwa  fedha na uongozi  huo wa kijiji.      

Akizungumzia Changamoto hizo mtendaji wa kata ya Kirua vunjo Kusini, Jovita Mosha alisema kero za ukosefu wa choo katika soko hilo zipo, licha ya kukataa kuwa hakuna wafanyabiashara ambao wanajisaidia na kutupa kinyesi hicho katika eneo hilo.

Jumla ya watoto laki tano mkoani Kilimanjaro wanatarajia kupatiwa chanjo ya Surua na Rubella

KILIMANJARO jumla ya watoto laki tano, wenye umri wa miezi tisa hadi miaka 15, mkoani Kilimanjaro, wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua na Rubella, katika wiki ya chanjo hiyo iliyoanza Oktoba 18 na inatarajiwa kumalizikia oktoba 24 mwaka huu.

Akizungumzsa na waandishi wa habari mkoni Kilimanjaro, Meneja Mpango wa chanjo Taifa, Dkt Dafrossa Lyimo, amewataka wazazi, walezi pamoja na wataalamu wa afya kuhakikisha malengo ya serikali ya kuwapatia chanjo watoto hayo yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Dkt Lyimo amewataka wazazi hao kuacha tabia ya kuwazuiwa  watoto wao, wasipatiwe chanjo hiyo,  kwa dhana ya kuwa watoto hao wataua kizazi chao.

Alisema kuwa ugonjwa Surua na Rubella ni ugonjwa hatari, kwani huambukizwa kwa njia ya hewa, na kwamba hauna tiba kamili hivyo tiba yake ni kuwahi kupatiwa chanjo hiyo mapema.

Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Peter Kihamia alisema takwimu zinaonesha kuwa jumla ya watu watatu wamebainiki kuwa na ugonjwa wa Rubella kwa mwaka huu, kati ya vipimo 48 vilivyofanyiwa uchunguzi mkoani Kilimanjaro.

Alisema kwa kipindi cha mwaka jana watu wapatao 28 wilayani Rombo waligundulika kuwa na dalili za ugonjwa wa Rubella, na baada ya kugundua dalili hizo walizitibu.

Monday, October 20, 2014

Tamko kutoka kwa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kuhusu raia kuvaa sare za jeshi


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo : N G O M E                Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM  20 Octoba, 2014
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz


Taarifa kwa Vyombo vya Habari
            Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.

          Aidha, kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ. Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na MahusianoMakao
Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963.

Mwalimu auwawa kikatili na mwili wake kutupwa kwenye mtaro wa maji machafu

KILIMANJARO mtu mmoja alietambulika kwa jina la Eliuteri Leon Kiwia (45) mkazi wa uru Kimanganuni  na mwalimu wa shule ya ufundi na compuiter Santa Cacilia iliyopo Uru Njari amekutwa amekufa maeneo ya Uru Kimanganuni kata  ya Uru Kusini tarafa ya Hai Mashariki  wilaya ya Moshi Vijijini  mnamo  tarehe  19 octoba mwaka 2014 majira ya 06:15 hrs.

Akiongea na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kilimanjaro Koka Moita, alisema mtu huyo alikutwa amekufa baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mwili wake kutumbukizwa katika mfereji wa maji  pembeni mwa barabara ya lami na watu wasiojulikana.

Alisema baada ya mwili wa marehemu kukaguliwa kwenye eneo la tukio ulikutwa na jeraha kubwa kichwani na  kukutwa na fedha 300,300 pamoja na simu ndogo  ya mkononi aina ya Samsung.

Aidha alisema kuwa chanzo cha mauwaji hakijafahamika na hakuna aliye kamatwa kuhusiana na tukio hilo na msako mkali unaendelea kufanyika ili kuwabaini wahusika watukio hilo. >>> "Hadi sasa hajafahamika kama kuna mali yoyote iliyoibiwa na uchunguzi wakina unaendela  juu ya mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kutambua na hatimae kuwakamata wauwaji" alisema Kamanda Moita.

Pia ametoa wito kwa wananchi wote wanaofahamu jambo lolote linaloweza kusaidia kukamatwa kwa watuhumiwa wa tukio hili wasisite  kutoa taarifa  polisi na zitafatiliwa kwa kina ili kuwatia mbaroni wahusika alisema Kamanda Koka.

Chaba ft Jordan - Murder (Official Music Video)


Tazana na ku dowload wimbo wa Chaba aliomshirikisha Jordan unaokwenda kwa jina la Murder. >>>

Official Music Video kutoka kwa Chindo Man (Watengwa) ft Wise Man - Haikupangwa

 

Unaweza kuutazama na ku dowload wimbo wa Chindo Man kutoka Watengwa aliomshirikisha Wise Man, wimbo unafahamika kwa jina la Haikupangwa >>>