Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi wa
Kimarekani na waalimu wao pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe John Haule, Balozi wa Marekani nchini,
Mhe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar.
Wanafunzi hao wanachukua masomo ya lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu
cha Zanzibar ( SUZA). Walikuwa wameongozana na Watendaji Wakuu wa
Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Rais Kikwete Ikulu
jijini Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa
ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour iliyoandaliwa na
ubalozi wa Tanzania Marekani
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa
Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini Dar es
salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua
tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na ubalozi wa
Tanzania Marekani. Hii ni mara ya pili kufanyika ziara kama hii, ambapo
pamoja na kuwakaribisha tena Rais Kikwete alisema amefurahishwa sana kwa
wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za wanyama za kusini mwa nchi
(Selous na Ruaha) vyenye wanyama wengi na vivutio ambavyo havipatikani
kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu ambayo kwa muda mrefu
sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.
PICHA NA IKULU |
No comments:
Post a Comment