Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 12, 2012

MAAFISA WA HALMASHAURI YA MBEYA VIJIJINI WANUSURIKA KUUAWA...!

Na, Gordon Kalulunga, Mbeya 

MAAFISA wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Jimbo la Mbeya Vijijini, wamenusurika kufa baada ya kupopolewa mawe na wakulima wa kijiji cha Igoma wilayani humo. 
Habari kutoka eneo la tukio zimesema kuwa maafisa hao walifika katika eneo hilo na kuwataka wakulima na wafanyabiashara wa zao la viazi kulipa ushuru wa Sh. 1000 kwa kila gunia hali iliyoleta mtafaruku kati yao na wakulima hao ambao pia ni wafanyabiashara.



Baada ya kulumbanan kwa muda mrefu, ndipo wakajitokeza vijana na kuanzisha vurumai kati yao na maafisa hao kwa madai kuwa Serikali imekuwa ikijotokeza kutoza ushuru huo wakati wa mazao lakini wakati wa kuhudumia mashamba yao inakuwa mafichoni.


Maafisa hao baada ya kuona kuwa wanazidiwa waliamua kuingia katika gari yao yenye namba za usajili STK 864 na kuanza kukimbia huku wakulima hao wakiendelea kuwavurumishia mawe.


Baada ya hapo maafisa hao wakiwa wamejeruhiwa, walifika katika kituo cha Polisi cha kati na kutoa maelezo huku gari yao ikiwa imevunjwa vioo vyote.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Andason Kabenga alisema kuwa alipata taarifa hiyo akiwa katika kata katika shughuli za kukagua Maendeleo na diwani wa kata ya Halungu aliyemtaja kwajina la Hashim.

''Ni kweli nimepata taarifa hiyo ya kuumizwa watendaji wetu lakini ushuru waliokuwa wanadai ni halali mana ulipitishwa katika baraza la Madiwani'' alisema Kabenga
Kikosi kazi cha mtandao wa kalulunga jana jioni kilifika katika kituo kikuu cha Polisi mkoani Mbeya na kulikuta gari likiwa limeegeshwa nje ya kituo hicho huku maafisa hao wakiwa ndani wakitoa maelezo.

Sakata hilo limetokea baada ya wiki moja wakulima wa eneo la Namba One wilaya ya Rungwe kufunga barabara na kuchoma moto Lami wakipinga ushuru wa namna hiyo mpaka pale Mkuu wamkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alipoingilia kati na kusitisha ushuru huyo.

No comments:

Post a Comment