Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, July 7, 2012

MGOMO WA MAGARI YA ABIRIA MOSHI...!

 Hali ilivyokua maeneo ya stannd kubwa ya moshi yamagari yaendayo mikoani

Hali ya usafirishaji ndani ya Manispaa ya Moshi imebadilika kuanzia saa mbili ya asubuhi ua leo baada ya Magari yanayosafirisha abiria katika viungo vya Moshi na Mkoa Kilimanjaro kugoma kutoa huduma hiyo

CHANZO
Chanzo cha mgomo huo ni kutokana na halmashauri ya Manispaa ya Moshi kupandisha ushuru wa Magari kutoka Tsh.1000 mpaka Tsh.1500 kwa gari
Ambapo kwa mujibu wa wenye vyombo vya usafiri wanasema kiwango hicho ni kikubwa sana

WANATAKAJE
Wakiongea na Chalii wa Moshi kwa nyakati tofauti wanasema ili huduma iendelee kama kawaida wanataka Manispaa ya Moshi ipunguze bei ya ushuru kutoka Tsh.1500 mpaka Tsh.500

HALI YA USALAMA
Hali ya usalama kwa sasa ni nzuri tofauti na ilivyokua asubuhi kwani gari za askari wa kuzuia fujo (FFU) zimetanda kila kona kuhakikisha hakuna uvujwaji wa amani

KINACHOENDELEA
Kwa sasa viongozi wa chama cha wasafirishaji Moshi AKIBOA wako katika kikao na viongozi wa Manispaa ya Moshi ili kufikia Muafaka.

ABIRIA
Abiria wanaonekana kukata tamaa ya kupata usafiri
ABIRIA
abiria wengine ilibidi watembee umbali mrefu ili kuweza kufanikisha shughuli zao na wengine walipanda bodaboda kwa kiwango cha Tsh 1000 hadi 1500 inategemea na umbali
ila wengine walitumia nyenzo mbadala kama Baiskeli
Chat Conversation End

No comments:

Post a Comment