|
![]() “Bodi ya Wakurugenzi wa NBC imepokea malalamiko ya wafanyakazi kuhusu kuwapo ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kiutendaji katika uongozi wa benki.” Alisema Assad katika taarifa hiyo na kuongeza: “NBC ni benki inayoheshimika na kuaminika, kwa hiyo ili ya kulinda taratibu na misingi ya utawala bora, imeanza kufanya uchunguzi wa kina na sahihi juu ya tuhuma hizo. Ili kufanijkisha kazi hiyo, Bodi ya Wakurugenzi imeamua kumpa likizo Mafuru ili kupisha uchunguzi huo kufanyika. Naamini kazi hiyo itakamilika mapema iwezekanavyo.” Naye mafuru kwa up-ande wake alisema; “ Nitatoa ushirikiano kwa dhati kuhakikisha kuwa uchunguzi juu ya tuhuma zinazonikabili unafanyika kwa uhuru na haki.” |
No comments:
Post a Comment