Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, July 4, 2012

MWANACHUO WA CHUO CHA UALIMU ST.AGREY MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA PIKIPIKI...!


Samahani kwa picha hiziHii ndiyo pikipiki inayodaiwa mwanachuo huyo kuiiba

Hiki ni kitambulisho cha mwana chuo huyoMwananchuo wa chuo cha ualimu cha ST Aggrey kilichopo uyole jijini mbeya
 anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali 
katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma zakuiba pikipiki zakusafirishia abiria
 maarufu kama bodaboda. 

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa
 huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati 25 mpaka 30 . 

Mgonja amesema tukio hilo limetokea mnamo july 2 mwaka huu majira ya saa 8
 za mchana katika daraja lilopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara yakuelekea
 isanga jijini mbeya. 

Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada yakupewa taarifa za
 kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina T-BETTER yenye alama ya
 chama cha Demokrasia na maendeleo mali ya JOSEPH KAPASI(23)mkazi 
wa Ilomba jijini hapa

 
Kwaupande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa
 kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae alipoanza kuendesha vizuri alitokomea
 nayo na marabaada ya hapo alipatikana eneo la isanga akielekea barabara ya
 chunya ili aibe na ndipo akakamatwa na wanainchi wenye hasira kali nakuanza
 kumpa kichapo ambacho kimemfanya azirai

No comments:

Post a Comment