Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, July 30, 2012

WALIMU WAIBA MITIHANI KUWANIA ZAWADI...!

AHADI za zawadi pamoja na hofu ya kushushwa vyeo kwa walimu wakuu wa shule za msingi, kumewafanya baadhi yao kuiba mitihani, ili shule zao zinaonekane zimefanya vizuri katika mitihani hiyo.
Hali hiyo kwa kiasi kikubwa imeelezwa kuchangia watoto wasiojua kusoma na kuandika wanachaguliwa kujiunga sekondari.
Vyanzo mbalimbali vya habari vilieleza hayo baada ya Tanzania Daima kutaka kujua inakuaje baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanakuwa hawajui kusoma na kuandika.
Tanzania Daima ilielezwa walimu wa shule za msingi ni kikwazo kikubwa na ndio wanaochangia wanafunzi kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wakiwa hawajui kusoma na kuandika kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakiibiwa mitihani na kuwapatiwa majibu.
“Kikwazo kikubwa ni walimu wa shule za msingi wamekuwa wakishindania zawadi zinazoahidiwa na wakuu wa halmashauri pamoja na baadhi ya wanasiasa kama vile kupelekwa bungeni.
“Tuhuma hizo zipo zimesikika katika kikao cha Julai 10, mwaka huu, kilichoketi katika sekondari ya Singe. Kilikuwa ni kikao cha kazi kati ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani, Ndelichako, na wakuu wa sekondari wa mkoa wa Manyara,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilisema wachangiaji mbalimbali walieleza walimu wakuu wanaiba mitihani hiyo, ili wapate zawadi wanazoahidiwa.
Naye Ofisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri ya Mbulu, Michael Hadu alikiri kuwapo kwa baadhi ya walimu sio waaminifu na kwamba hali hiyo imebainika kupitia wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuchaguliwa kujiunga sekondari.
“Hii inaashiria kuwa walimu na wasimamizi wa mitihani wote kwa pamoja wanakiuka taratibu za usimamizi wa mitihani,” alisema ofisa huyo.

No comments:

Post a Comment