ASKARI mwenye namba D.8384 CPL Julias Kimathi amefariki dunia mkoani Kilimanjaro baada ya gari alilokuwa aksafiria kugongana uso kwa uso na fuso lenye nambari T.553 AJN .
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema kuwa Agusti 26 mwaka huu majira ya saa 01:45 usiku katika eneo la Ghona Chekereni wilaya ya Moshi Vijijini katika barabara ya Moshi-Tanga magari mawili yaligongana uso kwa uso na kusababisha kifo cha askari huyo papo hapo.
Alisema kuwa Mitsubishi Fuso yenye nambari T.553 AJN lililo kuwa likitokea Arusha kwenda Tanga likiendsha na dereva Seraphin John (38) pamoja na Toyota Pickup yenye nambari .781 AHZ iliyokuwa ikitokea wilayani Mwanga kwenda Himo ambapo ilikuwa ikiendeshwa na askari huyo kugongana uso kwa uso na kusababisha kifo cha askari huyo.
Aidha Boaz alisema kuwa kabla ya ajali hiyo inadaiwa kuwa magari hayo yaligongana baada ya dereva wa fuso alipokuwa akijaribu kulipita Trekta aina ya Messey Ferguson Lenye nambari T.585 AFD na ndipo alipo kwenda kugongana uso kwa uso na gari la askari huyo.
Alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa fuso kutaka kupita trekta hilo bila kuchukua taadhari ya kutosha na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua ziweze kuchukuliwa .
Wakati huohuo kamanda Boaz aliwataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hichi cha zoezi la sensa linaloendelea nchi nzima na kuwataka wananchi ambao bado hawaja hesabiwa kutimiza wajibu huo muhimu kwa amani kwaajili ya maendeleo kwas taifa.
No comments:
Post a Comment