Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 8, 2012

Dude Avamiwa na Majambazi Nyumabani kwake.....!

Dude
Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania Kulwa Kikumba almaarufu kama DUDE amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo tareh 8/8/2012 kwake anapoishi Uwanja wa ndege jijini Dar es salaam....akiongea na thisisdiamond dude alisema kua yeye alikua yuko Kinyerezi katia harakati zake za kushut muvie usiku huo ambapo alimuacha mkewe na watoto wake watatu wakike wakiwa nyumbani usiku huo... alisema kua baada ya familia yake kula daku na kwenda kulala mida ya saa 9 usiku ndipo Majambazi hao waliingia na kupulizia sumu ndani ya nyumba hiyo ili waendelee kulala wasishtuke waanze kuiba... wezi hao walifanikiwa kuiba kila kitu ikiwemo Nguo,Muziki,Tv,Baloo la nguo la duka la dada yake kutoka china alokua akiweka kwake kwaajili ya usalama na kadharika.... alisema wezi hao waliiba hadi vyakula vilivyobaki na gunia la mchele....asubuhi ya saa moja ndipo familia hiyo iliamka na kukuta kila sehem kweupe watu wamekomba na milango yote iko wazi, ndipo bwana mkubwa wakampigia na kumpa taarifa hizo.....

No comments:

Post a Comment