Akiwa ndio mchezaji aliyesajiliwa kwa fedha ndefu kutoka nchini Tanzania, Mbwana Ally Samatta anaishi ambayo ni mcheza soka wa kimataifa anastahili kuishi.
Akiwa ameuzwa kwa dola za kimarekani zaidi ya 100,000, kwenda TP Mazembe kutoka Simba, Mbwana Samatta analipwa kiasi cha dola 5000 kwa mwezi ambayo ni sawa na shilingi millioni 7.5 huku akichukua marupurupu ya kutosha.
Mbwana Samatta amekuwa akicheza na kuperfom kwa kiwango kikubwa katika kila nafasi anayopata anapoichezea klabu yake na kwa kiwango alichoonyesha kuna uwezekano mkubwa mkataba wake utaboreshwa zaidi na kuendelea kuvuna mkwanja mrefu zaidi.
Kwa sasa hivi Samatta amenunua gari la kisasa zaidi Chrysler Crossfire la mwaka 2006 ambalo limemgharimu takribani millioni 50 za kibongo.
Ikiwa Samatta ataendelea kucheza kiwango alichonacho sasa, basi ni dhahiri tutaendelea kuona akiishi kwenye majumba ya kifahari huku akipush magari ya gharama zaidi.


Chanzo: lukemusicfactory