Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, August 28, 2012

MPAKA SASA KILIMANJARO YAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA YENYE THAMANI YA MILION 447....!

MADAWA ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 447
yamekamatwa katika kipindi cha januari hadi julai mwaka huu mkoani
Kilimanjaro ambapo yana uzito wa zaidi ya kilo 1102.

Akizungumzia kukamatwa kwa madawa hayo wakati akizungumza na chanzo chetu ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoani Kilimanjaro Robert Boaz alisema kuwa aina ya madawa hayo ya kulevya kuwa Bangi,Cocaine, Heriine pamoja na Mirungi.

Alisema kuwa madawa hayo yalikamatwa na jeshi la polisi yote yakiwa na
dhamani hiyo ambapo zaidi ya kesi 383 zimefikishwa mahakamani na kwamba
zaidi ya watu 323 wameshikwa ambapo kati yao wanaume wakiwa 280 na
wanawake wakiwa 43.

Alifafanua kuwa jumla ya madawa ya kulevya yalio kamatwa kuwa ni bangi
kilo 421,238 yenye thamani ya shilingi 42,100,000, Cocaine kilo 7.787 yenye
thamani ya shilingi 371,346,000,Heroine kilo 0.9 yanye thamani ya shilingi
24,800 na Mirungi kilo 673.41 yenye thamani ya shilingi 33,650,000.

Boaz alisema kati ya kesi 383 jumla ya kesi 80 watuhumuiwa walipatikana na
hatia na vifungo na wengine kulipa faini ya jumla ya shingi 2,360,000 na
kwamba watuhumiwa watatu waliachiwa huru.

"katika kipindi cha januari hadi julai mwaka huu tumeweza kupeleka kesi
383 mahakamani na kuwakamatwa wanawake 43 pamoja na wanaume 280 idadi hii
inatisha sana katika hali ya kawaida, ila jeshi la polisi tumejipanga vyema
kukabiliana na biashara hii ya uingizwaji wa madawa nchini" Alisema Boaz

Alisema kuwa uingizwaji wa madawa hayo ni janga kubwa ka vijana ambapo
aliwataka wananchi kushirikiana a jeshi hilo ili kutokomeza biashara hiyo
na kwamba iwapo watamtlia shaka mtu yeyote ambaye anayefanya biashara hiyo
atoe taarifa haraka ili aweze kuchukuliwa hatua.

No comments:

Post a Comment