Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 31, 2012

SAKATA la umri wa Elizabeth Michael 'lulu' lapelekwa Mahakama ya Rufani, Septemba 17, 2012...!

 SAKATA  la umri wa msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji, sasa limepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Septemba 17, 2012.
Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ,akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba. Anadaiwa kutenda kosa hilo April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu, Sinza jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana kutoka mahakamani hapo na kuthibitishwa na mmoja wa mawakili  wa msaniii huyo, zinaeleza kuwa , shauri hilo litasikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama  ya  Rufani ambao ni January Msoffe, Bernard Luanda na Katherine Oriyo.

Mahakama ya Rufani itafanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuona kama ulikuwa ni sahihi, kukubali kufanya uchunguzi wa umri halali wa mshtakiwa huyo, kufuatia maombi yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka.
Umri wa mshtakiwa huyo umezua utata baada

ya mawakili wanaomtetea  kuomba kesi yake isikilizwe katika Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) wakidai kuwa bado ni mtoto.
 Mawakili hao wanaomtetea mshtakiwa huyo ni, Kennedy Fungamtama (Kiongozi wa jopo), Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tangantyika(TLS) Peter Kibatala na Fulgence Massawe wa Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC). 
Mei 7, 2012, mawakili hao waliiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iruhusu kesi hiyo isikilizwa katika Mahakama ya Watoto wakidai kuwa, mshtakiwa huyo ni mtoto kwa kuwa  ana umri wa miaka 17 na sio 18 kama hati ya mashtaka inavyoonyesha.
Hata hivyo Mahakama hiyo iliyakataa maombi hayo baada ya kupingwa na upande wa mashtaka ulioongozwa na wakili wa Serikali  Elizabeth Kaganda ambaye aliomba wapewe muda zaidi kwa kuwa bado upelelezi ulikuwa ukiendelea na kwamba upelelezi huo unahusisha  suala la umri. 

Wakili Kaganda aliongeza kuwa hata jina la mshtakiwa katika cheti cha kuzaliwa kilichotajwa na mawakili wake, linasomeka kamam Diana Elizabeth wakati mahakamani mshtakiwa anatambulika kama Elizabeth.


Katika uamuzi wake, Hakimu Mkazi Agustina Mmbando alisema kuwa kwa kuwa kesi hiyi ni ya mauaji na upelelezi haujakamilika, mahakama haiwezi kuamua hoja yoyote, badala yake aliutaka upande wa utetezi kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu.


Kufuatia uamuzi huo, Mei 15, 2012 upande wa utetezi uliwasilisha maombi Mahakama Kuu ukiomba mahakama hiyo iamuru kuwa Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kufanya uchunguzi wa umri halali wa mshtakiwa huyo au Mahakama Kuu yenyewe iamue  kuchunguza umri wa mshtakiwa.


Juni 11, Mahakama Kuu ilikubali maombi ya mawakili wa mshtakiwa huyo kufanya uchunguzi wa umri sahihi wa mshtakiwa huyo, baada ya Mahakama ya Kisutu kuyakataa.

Mahakama Kuu ilitarajiwa kuanza uchunguzi huo wa umri halali wa mshtakiwa huyo Juni 25, 2012, kwa kusikiliza hoja za kila upande na kupitia vielelezo mbalimbali kuhusu umri wa mshtakiwa huyo.

Hata hivyo hatua hiyo ilikwama na kulazimika kusimama baada ya upande wa mashtaka  kuitaarifu kuwa umewasilisha Mahakama ya Rufani  maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu kukubali kufanya uchunguzi wa umri wa mshtakiwa huyo, kama ulikuwa sahihi. 

Vielelezo vilivyowasilishwa Mahakama Kuu na upande wa mshtakiwa ambavyo ni hati za viapo vya wazazi wa mshtakiwa (mama, Lucresia Augustin Kalugila na baba, Michael Kimemeta), cheti cha kuzaliwa na cha ubatizo vya mshtakiwa vinaonesha kuwa ana umri wa miaka 17. 

Vinaeleza kuwa mshtakiwa huyo alizaliwa April 16, 1995  katika kituo cha Afya Muhimbili na kupewa cheti cha kuzaliwa namba B.0318479 cha Julai 23, 2004. 

Lakini vielelezo ya upande wa mashtaka navyo vinaonyesha kuwa mshtakiwa huyo ana umri wa zaidi ya miaka 18 yaani miaka 21.  Vielelezo ni pamoja na maelezo ya mshtakiwa huyo aliyoyatoa polisi wakati alipohojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili, maombi ya hati ya kusafiria (Passport) na maombi ya leseni ya udereva. 
 Pia kuna mkanda wa video aina ya CD ya mahojiano kati ya mshtakiwa huyo na mtangazaji wa kituo kimoja cha runinga nchini.

No comments:

Post a Comment