Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 20, 2012

UTAPELI KUPITIA SIMU: MKUU WA MKOA, VIONGOZI WAINGIA KATIKA BALAA HILO...!

Viongozi watatu wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mkoa wa Katavi wametapeliwa na watu wasiojulikana baada ya kuelezwa kuwa wameshinda promosheni ya Airtel ya Shilingi milioni 50.

Waliotapeliwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajabu Rutengwe, Katibu Tawala wa Mkoa, Emmanuel Kalobelo na Mganga Mkuu wa Mkoa, Yahaya Hussein.

Viongozi hao walitapeliwa kwa nyakati tofauti na watu waliojitambulisha kwao kwa simu kuwa ni watumishi wa Kampuni ya simu.

Tukio la kwanza lilikuwa ni la Mkuu wa Mkoa kuambiwa ameshinda zawadi ya Sh. milioni 50 na aliombwa awatumie namba za simu za watu watano aliozungumza nao mara ya mwisho na baada ya kufanya hivyo simu yake ya mkononi ikafungwa na matapeli hao.
Akieleza mkasa huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Yahaya alisema yeye baada ya kupigiwa simu na matapeli hao hakuwa na shaka nao kutokana na kauli yao ilivyokuwa ya ustaarabu.
Alisema baada ya kuwapa majina ya watu watano alizungumza nao mara ya mwisho kwenye simu yake na kuombwa awatajie namba zake za siri za akaunti ya Benki ili wamtumie zawadi ya Sh. milioni 50.
Baada ya kuombwa namba yake ya siri, Dkt. Yahaya hakuwa na shaka yoyote na hivyo akawapatia namba hiyo ya siri.
Hata hivyo hakuweza kuibiwa fedha zozote kwa vile akaunti yake haikuwa na salio la kutosha.

Meneja wa Wawi la bank hiyo Wilaya ya Mpanda, Erick Luhanda alisema alipokea malalamiko kutoka kwa viongozi hao.
Alisema kiongozi wa mwisho kumpa taarifa alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa, Kalobelo.
Luanda alisema tayari taratibu za kibenki zimefanyika hivyo hakutakuwa na hujuma kwenye akaunti za viongozi hao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kida-vashari alithibitisha kutokea matukio hayo.

No comments:

Post a Comment