Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, August 4, 2012

Wapiganaji 9 wa Ash-Shabab wauawa nchini Somalia...!


 
Wapiganaji 9 wa kundi la wanamgambo wa Ash-Shabab wa Somalia wameuawa na ndege ya kigaidi isiyo na rubani ya Marekani. Sheikh Adil Muhammad afisa wa Ash-Shabab ameziambia duru za habari kwamba, ndege ya kigaidi isiyo na rubani ya Marekani imefanya mashambulio kusini mwa Somalia na kuwauwa wapiganaji 9 wa kundi hilo na kuwajeruhi wengine kadhaa. Katika siku za hivi karibuni ndege za kigaidi za Marekani zimeshadidisha mashambulizi yake nchini Somalia; mashambulio ambayo yamekuwa yakiwalenga pia raia wasio na hatia yoyote. Ni kwa muda mrefu sasa ambapo Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kushambulia Pakistan, Afghanistan, Yemen na Somalia kwa madai ya kukabiliana na wanamgambo wa al Qaida. Hata hivyo Waislamu wa kawaida ndio ambao wamekuwa wahanga wakuu wa mashambulio hayo ya kigaidi ya Marekani.

No comments:

Post a Comment