WATU watatu wamefariki dunia mkoani kilimanjaro katika matukio matatu tofauti likiwemo la mtu mmoja kuuwawa kikatili kwa kuchinjwa kama kuku hadi kufa katika kijiji cha Levomoro Kilema Kusini wilayani Moshi jimbo la Vunjo.
Akizungumzia tukio la kwanza kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agusti 29 mwaka huu majira ya saa moja na nusu usiku katika eneo la Kilema Kusini kijiji cha Levomoro kukutwa maiti ya Gasper Nyange (40) nyumbani kwake akiwa amechinjwa kikatili.
Alisema kuwa maiti hiyo ilikutwa nyumbani kwake alipokuwa akiishi marehemu ikiwa imechinjwa kama kuku shingoni katika eneo hilo na kwamba maiti hiyo iligunduliwa na ndugu yake marehemu Matias William mara baada ya kumtembelea kaka yake nyumbani kwake.
Aidha kamanda boaz alisema kuwa mara baada ya ndugu yake huyo kuona hali hiyo alitoa taarifa polisi ambopo jeshi la polisi limewashikilia watu wawili kutokana na kuhusika na tukio hilo na kuwataja kwa majina kuwa ni Jacob Kimaro(40) pamoja na Eliuruma Stephen (19) na kwamba chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi baina yake na watuhumiwa hao.
Boaz aliezea tukio jingine kuwa ni gari kumgonga mtembea kwa miguu akijaribu kuvuka barabara na kufariki dunia papo hapo katika barabara ya Mobogini eneo la kwa Elia wilayani Moshi Vijijini.
Alisema kuwa gari lenye nambari za usaji T 839 APD Toyota haisi iliyo kuwa ikiendeshwa na dereva ambaye hajafahamika ikitokea Moshi mjini kwenda Mabogini ilimgona mtembea kwa miguu Giras Michael(34) na kufariki dunia papo hapo na kwamba jeshi la polisi linamsaka dereva huyo kutokana na kukimbia baada ya ajali hiyo.
Akizungumzia tukio jingine kamanda Boaz alisema kuwa lilitokea agusti 29 majira ya saa sita mchana katika eneo la Ushirika Mansipaa ya moshi mkoani hapa ambapo aliuwawa Hussen Musssa (27) na wananchi wenye hasira kwa kumshambulia na mawe pamoja a marungu wakimtuhumu kuiba begi lenye laptop.
No comments:
Post a Comment