WIZARA ya afya na ustawi wa jamii wamejiwekea mikakati maalumu ya kuunda bodi kwa kila hospitali za rufaa ikiwa ni pamoja na kuboresha usimamizi na utekelezaji wa majukumu ya watumishi lengo likiwa ni kuleta mabadiliko endelevu katika sekta ya afya nchini.
Akizungumza mwakilishi kutoka katika wizara hiyo Januarius Soko, wakati wa ukaguzi wa maeneo mbalimbali yaliokuwa kwenye maboresho pamoja na kujionea changamoto mbalimbali linazoikabili hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawezi.
Alisema kuwa moja ya mikakati hiyo ni kuwashirikisha wananchi katika kusimamia huduma za afya , utekelezaji utawala wa sheria , kukasimu madaraka na uwezo wa kusimamia katika ngazi ya mkoa.
Aidha alisema pamoja na wizara hiyo kuwa makini na kuanzisha bodi za kusimamia huduma za afya pia amewataka wananchi kujitokeza kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika swala zima la kuboresha maendeleo huku wakitambua mikakati na fedha wanazozitoa zinatumika kwa miradi iliyokusudiwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara na wakulima mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boysafi ambaye anatarajiwa kuwa mjumbe katika bodi hiyo aliwataka watumishi katika hospitali hiyo wakiwemo wauuguzi kuwa na moyo wa kizalendo katika kuendelea kutoa huduma ka wagonjwa.
Nao baadhi ya wagonjwa walikuwepo katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu waliipongeza wizara ya afya maendeleo na ustawi wa jamii kwa kuanzisha bodi hizo kwani wananchi wengi wataendelea kupata huduma bora na kushiriki shughuli za maendeleo .
No comments:
Post a Comment