Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 29, 2012

WATU WAWILI WATHIBITISHA NJAMA ZA T.I.D KUTAKA KUMUUA ALLY KIBA...!

TID
Jana kumevuma habari kuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Mohamed aka Top In Dar, anashikiliwa na polisi baada ya kushutumiwa kuwa alipanga njama za kumuua msanii mwenzie Ali Kiba.

Leo kupitia chanzo chetu, meneja wa Ali Kiba amezungumza kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo zilizo zagaa mtaani.

Ali Kiba
Anasema ni kweli walipata ujumbe unaosema kuwa kuna watu waliokuwa wametumwa kwenda kumuua  Ali Kiba.

"Baada sasa ya taarifa hizo  kuifikia familia, iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale anapoishi Ali Kiba wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kupeleleza eneo lile.
 Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatilia na kuwaweka chini baada ya kuwakamata. 

Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni kweli wao wametumwa kuja kufanya jambo hilo hapo kwa Ali Kiba na wao sio wenyeji wa Dar es Salaam wametoka mikoani. Walipoulizwa ni nani ambaye amewatuma kuja kufanya hilo jambo wakawa wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja yeye ndio anahusika. 
Basi moja kwa moja gari la jeshi la polisi likaenda kumkamata TID na hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi cha kati ambapo yupo mpaka hivi sasa anashikiliwa."

Ameongeza kuwa TID na watu hao walikutana katika maeneo ya Mtoni Kijichi kupanga mpango huo wa kumuua Ali Kiba.

No comments:

Post a Comment