Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 6, 2012

Wema Aponea Chupuchupu...!

Wema akiwa Hospitalin chini ya uangalizi wa Daktari

 
Wema akiwa amepumzika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake
Wema Sepetu alipelekwa katika Hospitali ya Heameda, Upanga jijini Dar akisumbuliwa na magonjwa ya kifua na tumbo. Ndugu zake staa huyo wa filamu za Bongo hawakutaka watu wengine wajue kama Wema yupo hospitalini.
Chanzo hicho kiliweza kutujuza kuhusu kuumwa kwa Wema alisema ndugu, jamaa na marifiki wakiwemo mashabiki wake wa filamu za kitanzania wamuombee Wema kutokana na kuteseka sana na hali ya kushindwa kupumua vizuri.
Chanzo hicho kiliendelea kutujuza kuwa Wema alipoenda Kigoma kwenye tamasha la Kigoma All Stars inawezekana alidhurika na vumbi jekundu na kumfanya asumbuliwe na tumbo na kubanwa na kifua kiasi cha kumfanya ashindwe kupumua vizuri.
Wema amelazwa katika hospitali ile ile ambayo siku chache zilizopita alikuwa amelazwa Diamond Platinum na pia daktari anayemchunguza afya Wema ni yuleyule aliyekuwa akimtibu Diamond ambaye anadaiwa kurudisha uhusiano wa kimapenzi na Wema walipokuwa katika ziara hiyo ya Kigoma.
Pia tulifanikiwa kuongea na Wema na hiki ndicho alichoweza kuongea “Kikubwa ni kifua, nahisi kama vile nina pumu, huwa kinanibana na kunifanya nishindwe kupumua vizuri, hata hivyo namshukuru Mungu naendelea vizuri. Kitu kingine siwezi kuvumilia hali ya vumbi, nilipokuwa Kigoma hali hiyo ilinitokea mara kwa mara kwa sababu ya lile vumbi la udongo mwekundu. Kosa nililolifanya nilivyorudi Dar sikucheki afya hadi imefikia hali hii,” mwisho wa kunukuu.
Kwa sasa Wema amesharuhusiwa kurudi nyumbani na yupo kwa mama yake mzazi kwa ajili ya uangalizi wa karibu wa afya yake.

No comments:

Post a Comment