Wanafunzi waliojiunga na masomo ya
kidato cha kwanza mwaka huu katika shule za Serikali na baadaye kubainika kuwa
hawajui kusoma na kuandika kwa ufasaha wanaendelea na masomo yao.
Imeelezwa kuwa katika baadhi ya
shule za sekondari kwa wilaya za Korogwe na Moshi Mjini imebaini wanafunzi hao
kuendelea na shule licha ya walimu kuwachuja na kutoa taarifa sehemu husika
kama walivyo elekezwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Mawenzi, Domin Kweka
amesema kwa mujibu wa vigezo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi kubaini wanafunzi wanaofaulu kujiunga na sekondari, wasio na sifa jumla
ya wanafunzi sita walibainika.
Kweka ameongeza kuwa wanafunzi hao
wameshindwa kabisa kufanya vizuri katika mtihani waliopewa jambo ambalo limeonesha
ulakini katika kujiunga kwao na masomo ya sekondari, japokuwa wanaendelea na
shule hadi sasa.
Aidha ameongeza kuwa tatizo hilo
hujitokeza kila mwaka kwa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza na hadi
sasa katika madarasa mbalimbali wapo wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.
No comments:
Post a Comment