Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, September 9, 2012

AFISA WA UPINZANI KONGO AOMBA HIFADHI AFRICA KUSINI...!


Afisa wa  upinzani Kongo aomba hifadhi A.Kusini
Afisa wa ngazi za juu wa mrengo wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayetafutwa na serikali kwa madai ya kufanya uhaini ameiomba Afrika Kusini impatie hifadhi kupitia ubalozi wake wa Burundi. Lambert Mende msemaji wa serikali ya Kongo ameeleza hayo na kusema kwamba mtuhumiwa huyo Roger Lumbala alikuwa mjini Bujumbura na hivi sasa ametiwa mbaroni na maafisa wa usalama wa Burundi na Kinshasa imetaka akabidhiwe kwa Kongo. Mende amesema wanafikiri kuwa Lumbala ni mfuasi wa kundi la waasi wa M23 wa Kivu kaskazini wanaosaidiwa na Wanyarwanda. Serikali ya Kongo inamtuhumu Roger Lumbala ambaye ni mbunge wa zamani na aliyewahi kuasi kwamba anashirikiana na serikali ya Rwanda katika kuyaunga mkono makundi ya waasi ya mashariki mwa Kongo ambayo yameshadidisha mapigano na mivutano ya kisiasa nchini humo. Maafisa wa Burundi na Afrika Kusini hawajasema lolote kuhusiana na suala hilo.


Chanzo: Iran Swhili Radio.

No comments:

Post a Comment