Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, September 1, 2012

BI KIDUDE BADO YUKO HAI...!

Asubuhi ya leo kumezagaa taarifa kuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab wa  Zanzibar, Bi. Kidude amefariki dunia. Radio ya Zenji FM ya visiwani humo nayo ilitangaza kifo chake. Lakini kutokana na vyanzo mbalimbali vya uhakika akiwemo mjukuu wake, Bi. Kidude bado yupo hai.

Habari zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii kuwa mkongwe wa muziki wa jadi visiwani Zanzibar Bi. Kidude amefariki dunia si za kweli chanzo chetu cha uhakika kimezungumza na watu wa karibu ambao wamesema kwamba Bi. Kidude bado yupo hai na amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal iliyopo visiwani humo. 


Hii si mara ya kwanza kwa Bi. Kidude kuzushiwa kuwa amefariki dunia.

No comments:

Post a Comment