Halima Kassim aka HK
Mwanadada mahiri katika tasnia ya habari upande utangazaji
anayetangaza na kituo cha radio KILI FM kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro anayefahamika
kwa jina la Halima Kassim aka HK amerejea ofisini baada ya sauti yake
kutokusikika radioni kwa takribani mwezi mmoja. Ukimya huo umezua maswali mengi kwa
wasikilizaji wa radio hiyo na kuwapa mashaka kuwa labda ameacha kazi kwenye kituo hicho cha radio.
Nilifanya juhudi za kumtafuta ili kufahamu ukweli kuhusu
hayo ambayo yanazungumzwa na watu mitaani, nilifanikiwa kumpata na kumuuliza machache.
Kwanza nilimchokoza kumuuliza eti wewe ndio Halima kassim wa radio KILI FM? “kwanza alitabasamu kidogo na kunijibu
haswaaa! mimi ndio Halima Kassim wa radio KILI FM lakini wengi hupenda kuniita HK”
nilitaka kwanza kufahamu mengi kuhusu HK na familia yake na hichi ndicho
alichonijibu “kwetu tumezaliwa watatu na wote ni wadada mimi ni mtoto wa pili
katika familia ya Bw. na Bi. Kassim Lema, chakula ninachokipenda ni ugali na
mboga za majani, kitu nisichokipenda kwenye maisha yangu ni kuumizwa akili au
mtu kucheza na akili yangu, kitu kizuri ambacho kila nikikikumbuka huwa
nafurahia sana ni siku nilipotangazwa kua Mtangazaji bora katika kituo changu cha
radio (Radio KILI FM) na tukio baya ambalo sitaweza kulisahau ni siku
nilipo faint na kuumia baada ya kuambiwa mama yangu amefariki dunia muda mfupi
tu baada ya kuachana nae” Alinijibu HK.
Swali lililofuata ni hili hapa, nimesikia watu wengi
wakizungumza mengi kuhusu wewe kutokusikika radioni kwa takribani mwazi mmoja sasa je
ni nini kinaendelea kwa sasa kuhusu wewe na KILI FM radio? “Namshukuru mwenyezi Mungu kwa uzima nilionao
kiukweli mimi nilikuwa likizo na hivi leo ndio nimerejea ofisini muda si mrefu
wasikilizaji wa KILI FM radio watanisikia hewani maana nimekuja kuwapa
wasikilizaji kile ambacho walikikosa kwa takribani mwezi mzima, Pia nashukuru
nilipata muda wa kupumzika ikiwa ni pamoja na kutembelea ndugu jamaa na
marafiki sehemu mbalimbali kama Dar es salaam, Arusha na Machame kwa bibi” hayo
ndio aliyoweza kunijibu HK.
Team nzima ya www.kingjofa.blogspot.com inakutakia kazi njema.
No comments:
Post a Comment