Wasanii wa Filamu hapa nchini Aunt Ezekiel,Wema pamoja na Shilole wakiwasikiliza mashabiki wao wanataka nini.
Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Diamond akiwaimbisha mashabiki na
wapenzi wa muziki huo waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta,kwenye uwanja wa Sokoine,mkoani Mbeya.
Shemejiii....Wema Sepetu akiwachetua kidogo wapenzi wa mambo ya filamu.
Msanii
wa bongofleva kutoka THT,Barnaba akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu
kwenye tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Sokoine
mkoani Mbeya.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,Linah akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu
ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye uwanja wa
Sokoine,Mkoani Mbeya.
Mmoja wa wasanii mahiri wanaotikiza kwenye anga ya muziki wa bongofleva hasa katika miondoko ya R&B,Ben Paul akikamua vilivyo jukwaani huku mashabikiwa wake wakishangilia kwa shangwe.
Pichani
kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh. Dkt. Norman Sigallah akimtaja
mshindi wa gari aina ya Vits itolewayo na kampuni ya Push Mobile,ikiwa
ni sehemo mojawapo ya mchakato wa tamasha la Serengeti Fiesta
2012,anayeshuhudia ni Meneja masoko wa Push Mobile Rugambo Rodney na
kulia ni Chiku Saleh kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ,ambapo
katika bahati nasibu hiyo iliyochezeshwa,aliyeibuka mshindi ni Eva B
Mgovani.
ni full kujiachi tuu ndani ya uwanja wa sokoine usiku huu.
Pichani
kati ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh. Dkt. Norman Sigallah akiwa katika
picha ya pamoja na Meneje vipindi wa Clouds FM,na mdau mwingine.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya anaefananishwa na mashabiki wake kama Ray
C,aitwaye Recho kutoka THT akitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya
tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Mashabiki wakishangilia vilivyo usiku huu,huku makamuzi ya wasanii yakiendelea jukwaani.
Msanii
wa bongofleva anaetikisa kwa nyimbo kadhaa ikiwemo,Mama halima,Aifora
na nyinginezo akiwaimbisha mashabiki wake kama waonekanavyo pichani
usiku huu.
Mkali
mwingine anaekuha juu katika mambo ya kuchana a.k.a kughani Stamina
akiamsha kitim kitim kwa wakazi wa mji wa Mbeya usiku huu ndani ya
tamasha la Serengeti Fiesta.
No comments:
Post a Comment